SIMIYU: Mkuu wa Mkoa amfuta kazi Mhandisi wa Mkoa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amsimamisha kazi mhandisi wa mkoa baada ya kunabainika alimdanganya Rais kuhusu ujenzi wa Hospitali.

=====
Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka matatu.

Akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi huyo anashtakiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewakwa kiwango cha kuridhisha.

Alisema akiwa mtumishi wa umma kinyume na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya jedwali la kwanza la kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003; mtumishi huyo alishindwa
kuandaa makadirio ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa yenye uhalisia.

Aliandaa makadirio ya Tsh46,1 yaliyosomwa mbele ya Mhe. Rais tarehe 11 Januari,2017 ambayo ni juu kuliko uhalisia.

Shtaka la pili ni kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi iliyopewa kinyume na kipengele cha 13 cha sehemu "A" ya jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la Serikali na 168/2003;

Alitaja (1) kuandaa makadirio ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa Tshs.46,106,456,000 hali iliyosababisha Mhe Rais kusomewa taarifa ya gharama zisizo na uhalisia na(2) Kuandaa michoro ya taswira (3 D)isiyoendana na michoro halisi ya Hospitali ya Mkoa iliyooneshwa mbele ya Mhe.Rais

Shtaka la tatu ni kufanya kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yake wakati wa utekelezaji ya kazi aliyopewa kinyume na kipengele cha 14 cha Sehemu "A" ya Jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003:- kwa (1) Kuandaa makadirio ya shilingi 46,106,456,000 ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa bila kuzingatia mita za mraba za eneo, michoro na kusababisha gharama kubwa zisizo na uhalisia
(2) Kuandaa makadirio ya shilingi 3,009,640,000 yasiyo na uhalisia ili kugharamia ujenzi wa majengo ya msingi kuwezesha Hospitali kuwa "functional" kwa kupiga simu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Pichani ni Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (mwenye koti jeusi) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mwenye tai wakizungumza na viongozi na watumishi wa Sekretatieti ya Mkoa wa Simiyu katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
 
Mkuu hii habari yako umeisoma kweli au umebandika tu? kichwa cha habari amfuta kazi ndani amemsimamisha kazi tena katibu Tawala Mkoa.
 
Mheshimiwa sana mkuu wa Mkoa kwa hiyo taarifa ilikua haijaletwa kwanza kwako ili uipitie ilisomwa moja kwa moja tuu mbele ya Mh. Raisi? kwahiyo Raisi asingesema chochote wewe pia ungepiga kimya au ungeibua kua mhandisi kaongopa kama ulivyo ibuka sasa hivi kwa kumtumbua, mie naona hata wewe mkuu wa Mkoa wa Simiyu unatakiwa kutumbuliwa make hukutimiza majukumu yako hadi Raisi kakusaidia au ulimendea ten % katika huo mradi ila sasa hivi umeamua kumuangushia jumba bovu mwenzio
Siku zote mdogo ndiyo huumia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amsimamisha kazi mhandisi wa mkoa baada ya kunabainika alimdanganya Rais kuhusu ujenzi wa Hospitali.

=====
Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka matatu.

Akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi huyo anashtakiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewakwa kiwango cha kuridhisha.

Alisema akiwa mtumishi wa umma kinyume na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya jedwali la kwanza la kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003; mtumishi huyo alishindwa
kuandaa makadirio ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa yenye uhalisia.

Aliandaa makadirio ya Tsh46,1 yaliyosomwa mbele ya Mhe. Rais tarehe 11 Januari,2017 ambayo ni juu kuliko uhalisia.

Shtaka la pili ni kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi iliyopewa kinyume na kipengele cha 13 cha sehemu "A" ya jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la Serikali na 168/2003;

Alitaja (1) kuandaa makadirio ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa Tshs.46,106,456,000 hali iliyosababisha Mhe Rais kusomewa taarifa ya gharama zisizo na uhalisia na(2) Kuandaa michoro ya taswira (3 D)isiyoendana na michoro halisi ya Hospitali ya Mkoa iliyooneshwa mbele ya Mhe.Rais

Shtaka la tatu ni kufanya kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yake wakati wa utekelezaji ya kazi aliyopewa kinyume na kipengele cha 14 cha Sehemu "A" ya Jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003:- kwa (1) Kuandaa makadirio ya shilingi 46,106,456,000 ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa bila kuzingatia mita za mraba za eneo, michoro na kusababisha gharama kubwa zisizo na uhalisia
(2) Kuandaa makadirio ya shilingi 3,009,640,000 yasiyo na uhalisia ili kugharamia ujenzi wa majengo ya msingi kuwezesha Hospitali kuwa "functional" kwa kupiga simu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Pichani ni Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (mwenye koti jeusi) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mwenye tai wakizungumza na viongozi na watumishi wa Sekretatieti ya Mkoa wa Simiyu katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Huyo mkuu wa mkoa alikuwa wapi kabla ya safari ya raisi?
Hakukuwa na maandalizi ya nini kitakuwa presented kwa mkuu wa nchi?
Huyo RC hakupitia taarifa hiyo kabla haijasomwa?
Kwa nini raisi asianze na RC kwanza?
Taarifa ya uongo imetolewa kwa raisi RC ukiwepo halafu unaanza sanaa...collective responsibility hivi inakuwaje?
 
Serekali ya aina hii inanikumbusha enzi za Amini!!!! Yeye ilikuwa kufuta kazi, kusimamisha, kuua, kutia ndani na kuteua!
Kwahiyo hata wakijenga barabara ya lami inayodumu miezi sita poa tu?
 
Ana muda gani katika urc wake? Je anayejenga ni hiyo mhandisi au ni mzabuni aliyepata? Mkurugenzi yuko wapi?
 
Kwahiyo hata wakijenga barabara ya lami inayodumu miezi sita poa tu?
Peleka ujinga wako huko huko ulikozoe? Unadhani wote ni wajinga kama ulivyo wewe!! Miaka inaisha mmebaki na simamisha, fukuza, shtukiza, kamata, weka pingamizi, tumbua, teua Taja majina, kamata mashoga hadi hamjui mnatakiwa kufanya nini sasa mnaona muda wa kurudi kwa wananchi umekaribia mnaona kikaango mnaanza Kuja na propaganda za kuchafua upinzani na kuwaweka ndani!
 
Ujinga tena? Hoja inajibiwa na hoja sio kama milipuko ya baruti. Unafanya kazi serikali ni? Maana kuna watu walizoea kuvuna wasipopanda....Sasa hivi wamegeuka mbogo wakujitakia kama wewe
 
Back
Top Bottom