Mara alama tano.....mara alama nane nyuma ya Simba.....Nahodha wa Simba, John Bocco, amesema watapambana kufa na kupona kesho Jumatano kuhakikisha wanaifunga Azam wanayokimbizana nayo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Bocco aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Azam, amekuwa moto katika mechi za karibuni akifunga mabao matano katika mechi nne za mwisho hivyo kufikisha mabao tisa, matatu tu pungufu ya kinara, Emmanuel Okwi wa Simba pia.
“Tunakwenda kucheza na Azam, ni timu nzuri ndiyo maana ipo nafasi ya pili. Watakuwa wanajiandaa kwa nafasi yao na sisi tunafanya maandalizi mazuri zaidi, ninachokiamini Simba ni timu kubwa na tutacheza nao kuhakikisha tunachukua pointi tatu muhimu,” alisema Bocco ambaye ni miongoni mwa wachezaji wachache wazawa wenye uwezo mkubwa kifedha.
Simba itaingia kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ikiwa na kumbukumbu ya sare mchezo wa ligi uliopita na kupoteza kwa bao 1-0 kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi.
Ushindi utaifanya iongoze kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Azam FC ambayo sasa iko nafasi ya pili, alama tano nyuma ya Simba yenye alama 38
Dar24
hahha Unawaandaa kisaikolojia hawachelewi kuvunja viti!Mpira una matokeo matatu.
Mkubali kupokea lolote ili mashabiki wenu wasije kung'oa viti tena. Teh teh teh.
Tunahofia viti kuharibiwa. Maana Haji anawaaminisha kuwa lazima washinde. Ikienda kinyume wengine hawaelewi kabisa.hahha Unawaandaa kisaikolojia hawachelewi kuvunja viti!
Na hapa ndo umbumbumbu wa mashabiki wa FIFA fc unapojidhihirisha mana kila asemalo manara wao wanalibeba kama lilivyoTunahofia viti kuharibiwa. Maana Haji anawaaminisha kuwa lazima washinde. Ikienda kinyume wengine hawaelewi kabisa.
MbaoMpira una matokeo matatu.
Mkubali kupokea lolote ili mashabiki wenu wasije kung'oa viti tena. Teh teh teh.
Nahodha wa Simba, John Bocco, amesema watapambana kufa na kupona kesho Jumatano kuhakikisha wanaifunga Azam wanayokimbizana nayo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Bocco aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Azam, amekuwa moto katika mechi za karibuni akifunga mabao matano katika mechi nne za mwisho hivyo kufikisha mabao tisa, matatu tu pungufu ya kinara, Emmanuel Okwi wa Simba pia.
“Tunakwenda kucheza na Azam, ni timu nzuri ndiyo maana ipo nafasi ya pili. Watakuwa wanajiandaa kwa nafasi yao na sisi tunafanya maandalizi mazuri zaidi, ninachokiamini Simba ni timu kubwa na tutacheza nao kuhakikisha tunachukua pointi tatu muhimu,” alisema Bocco ambaye ni miongoni mwa wachezaji wachache wazawa wenye uwezo mkubwa kifedha.
Simba itaingia kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ikiwa na kumbukumbu ya sare mchezo wa ligi uliopita na kupoteza kwa bao 1-0 kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi.
Ushindi utaifanya iongoze kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Azam FC ambayo sasa iko nafasi ya pili, alama tano nyuma ya Simba yenye alama 38
Dar24
Kalia msumariSimba akshinda Leo nalala juu ya kiberiti!
Watakuwa wako mezani kuandika, mbona mechi haichezwi?Andaeni barua ya rufaa FIFA