barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,375
- 29,732
Habari zenu!
Wana Simba SC, kuna kitu LAZIMA tukubali. Kuna ule msimu tulienda bila kufungwa mechi hata moja na kutwaa ubingwa, pia tulimpa kipigo cha paka mwizi mtani wetu wa jadi Yanga, ila toka huo msimu, YANGA wame-raise the bar ya standard ya mpira hapa bongo, na sisi Simba tumebaki kuongelea historia tu huku Yanga ikiendelea kung'aa nchini. Bahati mbaya Azam nayo licha ya rasilimali ilizo nazo, imejikuta ikiachwa na Yanga.
Yanga wenzetu wanatutania kwa rekodi za hivi karibuni za kutufunga nje ndani na pia kuchukua ubingwa back to back ila sisi Simba ni kukumbushia tu historia ya 2012 kushuka. HAIPENDEZI HATA KIDOGO.
Kufanya vizuri kwa Yanga ilitakiwa iwe chachu kwetu kufanya vizuri zaidi yao. Yanga wanasajili vizuri, na wana kikosi kipana na kocha mzuri na HAMNA fukuza fukuza na simamisha simamisha ya wachezaji sababu kuna nidhamu. Ni tofauti na Simba!
Na ukweli ni kwamba Yanga afadhari washinde VPL maana ndo timu pekee itayoweza angalau kupeperusha bendera ya taifa. Smba hii KIMATAIFA bado sana.
Viongozi wa Simba mjipange, la sivyo Yanga itaendelea kutawala DAIMA. Tulipo chukua ubingwa unbeaten na kuwafunga tano, wenzetu walikaa wakaangalia tatizo liko wapi na kulitatua. Sisi bado tunacheza mpira wa 2010 mwaka 2016, hii haitaleta matokeo chanya hata kidogo.
Na huu ndo ukweli, Yanga wako vizuri sana zaidi ya Simba na pia zaidi ya Azam.
Kutoka kwa shabiki wa Simba ila msema ukweli.
NOTE:
UONGOZI WA SIMBA IMEFIKA WAKATI MPENI TIMU MO DEWJI. Washabiki tunachotaka ni raha, imefika wakati hawa wanaoitwa wazee wa Simba na friends of Simba kina Hans Pop waiache timu, tunataka VIKOMBE na Simba irudi ktk hali yake.