Simba noma Jumapili 20/10/2013

Simba noma Jumapili 20/10/2013

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
simbamashabiki.jpg

Mashabiki wa Simba wakishangilia katika moja ya michezo ya timu yao katika Llgi Kuu msimu huu.
===
Dar es Salaam. Huku zikiwa zimesalia saa chache, rekodi za miaka 13 iliyopita, zinaonyesha Simba imeibuka na ushindi mara nyingi zaidi ya Yanga katika mapambano baina ya timu hizo iliyopigwa siku ya Jumapili.
Simba na Yanga zitashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho kukabiliana katika pambano la Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza.
Mwananchi lilifanya uchunguzi wake unaoonyesha kuwa kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka huu Simba ina rekodi nzuri zaidi ya kushinda siku ya Jumapili kuliko wapinzani wao, Yanga.
Rekodi hizo zinaonyesha kuwa katika kipindi hicho Simba na Yanga zilikutana mara 20, ambapo kati ya hizo Simba iliibuka na ushindi mara saba, wakati Yanga ilishinda mara mbili, huku mara 11 zikitoka sare.
Mechi zilizochezwa Jumapili baina ya Simba na Yanga Juni 25, 2000 (Simba 2-1 Yanga), Agost i 18, 2002 (Simba 1-1 Yanga), Novemba 10 (Simba 1-0 Yanga), Novemba 12, 2000 (Simba 0-0 Yanga), Septemba 28, 2003 (Simba 0-0 Yanga), Novemba 2, 2003(Simba 4-1 Yanga).
Machi 31, 2002 (Yanga 3-0 Simba), Aprili 20, 2003 (Simba 1-1 Yanga), Aprili 17, 2005 (Simba 2-1 Yanga), Machi 26,
2006 (Simba 0-0 Yanga), Oktoba 29, 2006 (Simba 0-0 Yanga), Julai 8, 2007 (Simba1-1 Yanga), Aprili 27, 2008 (Simba 0-0 Yanga).
Oktoba 26, 2008 (Yanga 1-0 Simba), Aprili 19, 2009 (Simba 2-2 Yanga), Aprili 18, 2010 (Simba 4-3 Yanga).
(Julai 27, 2008) Yanga haikutokea uwanjani, Simba ikapewa ushindi wa chee. Rekodi hizi zinajumuisha mechi za mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu Bara, Kombe la Mapinduzi, Tusker Cup, lililokuwa Kombe la Chama cha Soka Tanzania (FAT) na Kombe la Kagame.
Hata hivyo, ukiondoa michezo baina ya timu hizo iliyofanyika Jumapili, Yanga inaendelea kushikilia rekodi ya jumla baada ya kuibuka na ushindi mara 38, Simba 32, huku mara 32 zilitoka sare.
Katika hatua nyingine, Kocha wa Yanga, Ernest Brandts alisema, matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 iliyopata kikosi chake katika pambano la kirafiki dhidi ya Chipukizi ya Pemba yamekoleza morali ya wachezaji wake kuhakikisha wanaibwaga Simba keshokutwa.
“Unapocheza mechi ya kirafiki huku ukiwa na mechi nyingine ngumu wakati mwingine inaweza kuleta matatizo hasa kama utafungwa, kwani unaweza kushusha morali ya wachezaji,” alisema Brandts na kuongeza:
“Lakini kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chipukizi ni wazi umeongeza morali ya wachezaji wangu kuhakikisha tunapata matokeo mazuri Jumapili dhidi ya Simba.”


Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/Michezo/Simba-noma-Jumapili/-/1597534/2037720/-/vi7vuxz/-/index.html
 
Hiyo inafahamika j2 ni siku ya mnyama.. ndo maana huwa games zote za mnyama esp za kimataifa zinachezwa j2
 
Usiishi kwenye enzi hizo J2 lazima afungwe 3 bila
 
Daa bahat mbya takwimu ni mechi za j2 tu...ile 5-0 wameibania..
 
Mkuu kuwa makini sana nachaya maneno yako!

Hawa jamaa wa Simba ni wa ajabu sana. Ingekuwa WanaYanga wameyazungumza haya wangesema ni porojo, sasa hizi zao sijui tuziiteje, labda piroji. CC. kadoda.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kbm, issue hapa siyo Jumapili, ni matokeo ya mgogoro kati ya Yanga Kampuni na Yanga Asili. Hivi sasa huo mgogoro haupo hivyo mnyama ategemee kichapo tu. Huyo mwandishi ni kanjanja, Jumapili haina effect yoyote kwenye matokeo, angeweka wazi Yanga ilikuwa kwenye hali gani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom