Simba Na Yanga Ndio Wachawi Namba 1 Wa Soka Letu Tanzania

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Katika timu zinaongoza kwa kuuwa vipaji na ndoto za watanzania ni Simba na Yanga.
Nasema haya maana hata Mbwana thamata leo hii angekuwa anachezea timu hizo,Asingekaa aonekane wala kuthaminiwa kipaji chake
Wapo kina Samata wengi tu,Ila uyanga na Usimba unawapotezea muda na hatime wanazeeka bila vipaji vyao kuvuka mipaka
Ni Lini Simba, Yanga, Azam or Mtibwa zitakua kama TP Mazembe?
Hizi Club lazima zibadilike,Zijiimarishe na zifike mahali zicheze mashindano makubwa kwa uhakika zaidi.
Mchawi mkuu wa soka la Tanzania ni Simba na Yanga
 
ni kweli hivi vilabu vina tabia ya kuua vipaji. nina uhakika mbwana samata angekuwa leo bongo angekuwa anacheza aidha kwa mkopo coastal union kwa kupelekwa na simba au tayari kashaachwa kaenda kusajiliwa mwadui na julio maana yeye peke yake ndio kocha mwenye kujua na kutunza vipaji kwa muda mrefu. Lakini pia wakati mwengine wachezaji wa kibongo nao wanapaswa kulaumiwa wao wakishasajiliwa simba au yanga wanalewa sifa. Unakuta mchezaji yupo radhi kuondoka katikakti ya majaribio nje ya nchi kuja kuwahi mechi ya simba na yanga, au mchezaji anaacha kwenda nje kufanya majaribio kisa simba au yanga wamempa mkataba mpya. chakuchekesha wakifisha miaka 28 na kuendelea ndio utawasikia eti wanatafuta timu kwa nguvu nje ya nchi wanataka kwenda kucheza soka la kulipwa.
 
Kuna uzi upo humu, first eleven ya Yanga wachezaji 5 tu ndo wa ndani. Kati ya hao 4 wapo nyuma (kipa na mabeki 3), mbele yupo Msuva tu. Hii ni hatari sana kwa timu ya Taifa.
 
Sijaelewa, embu fafanua.
Namaanisha Yanga inaua vipaji vya watanzania. Uwanjani kwa wakati mmoja wanacheza wachezaji 11. Kati ya hao 11, ni 5 tu kutoka Tanzania. Hao 6 waliobaki ni mapro nao ni mizigo tu.

Nimesema kati ya hao watano, anayecheza mbele ni Msuva, waliobaki ni golikipa Dida, Yondani, Mwinyi na beki 2 jina limenitoka. Nchi yetu ina tatizo la forward, hawa Yanga wanawaweka benchi wazawa na kuwahujumu. Yanga ndio wachawi wanaua soka hapa nchini.
 
Machawi mwengine ni TFF kwa kuvilea hivyo vilabu na usimamizi mbovu wa mpira wa Tanzania.
 
Tumechoka na haya maneno ya kila siku. kwa hiyo timu zinazokuza vipaji ni zipi na tupe mifano? samata asingechezea simba tp mazembe wangemwona wapi? si kila siku ili uonekane umechambua basi ni lazima uziponde Simba na yanga. hii ni aina ya uchambuzi wa kitumwa kabisa .kama kuna mchezaji mzuri toka TZ unadhan hizi timu zitataka kumsajili wa nje? ili iweje? wachezaji wazuri TZ wapo ila wengi hawataki kucheza kaa profesheno wanataka kucheza kama wachezaji wa ridhaa. wakija wenzao wanakuja kupiga kazi hasa na hili lipo sana kwa watanzania wengi hata sehemu nyingne za kazi. hatuna haja kila siku kukaa kupiga kelele kuwa simba na yanga zinaua vipaji na wakati wachezaji wenyewe wanazikimbilia hizo hizo. wakachezee stand united na kariakoo lindi kule ndo kunakuza vipaji.
tuacheni ujinga wa kudhani ili uonekane unajua kuchambua soka basi unapaswa uziponde simba na yanga kila wakati. taja wachezaji wa 5 ambao wameendelea kuwa wazuri kwenye team zao hizoa ambazo si simba na yanga na baadaye kucheza soka la kulipwa . nitajie hao wachezaji wengine ambao wamezifanyia team zao mazuri makubwa kiasi kwamba simeshiriki mashindano makubwa.
ni ujinga kila siku kukaa kuimba habari za simba na yanga kuua mpira pasipo kutoa suluhisho ni nini na wala tusidhani ni sifa au kuonekana tunajua zaid tunaonekana ni mbumbumbu. tunashabikia team za nje kuliko zetu za ndani. ule ule unyani wa kuona vya nje ni vizuri kuliko vya ndani. nambie chelsea,man u, liverpool, barca, inter etc zina wachezaji wa nje wa ngapi na inakuaje.
 
Zanzibar hakuna simba na yanga,wamefika wapi,kenya ,uganda,hakuna simba na yanga, wamechukua kombe gani la afrika?,no research no rights to speak....nafkiri ungezungumzia mfumo zaidi kuliko timu
 
Back
Top Bottom