Simba na Yanga Derby iliyopooza haswa

Ayenda M

Member
Jan 4, 2018
97
132
Maisha yanaenda kasi sana. Miaka mitatu au mmoja nyuma mchezo wa Simba na Yanga ulikuwa ni moja kati ya michezo inayowavutia wengi sana kuitazama. Mida hii kila sehemu pangekuwa pamezizima kwa sababu ya ukubwa mchezo huu. Mwaka huu ni tofauti kidogo.

Wachambuzi na wadau wa soka wakiongozwa na vyombo vya habari wanajadili Udhamini wa GSM kwenye ligi na mapinduzi Cup. Ni mada iliyofukia kimuhemuhe cha mchezo huu.

Kauli ya Mhamasishaji yule aliyenunuliwa imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hamasa ya watu kuongelea mchezo huu.

Kuelekea mchezo huu kuna upande unajiamini sana huku ukiwa na tambo za kila aina, huku upande mwingine ukiwa kimya sana. Ni vita ya saikolojia kutoka kwa upande wa Timu ile ambayo CEO ni Ndugu yake na Malkia wa Uingereza.

Unadhani ni jambo gani ambalo linapelekea mchezo huu kuonekana umepooza?
 
Maisha yanaenda kasi sana. Miaka mitatu au mmoja nyuma mchezo wa Simba na Yanga ulikuwa ni moja kati ya michezo inayowavutia wengi sana kuitazama. Mida hii kila sehemu pangekuwa pamezizima kwa sababu ya ukubwa mchezo huu. Mwaka huu ni tofauti kidogo...
Usisahau, nakukumbusha tu mechi ni tarehe 11 saa 11.

Waulize mikia wenzanko wanaelewa hii ina maana gani ndio maana mnatapatapa tu halafu na timu hamna.

Elekezeni vichwa vyenu kibra kabisa, ndio utaelewa kwa nini Simba inajificha kwenye kimvuli cha GSM.
 
Leo orodha ya vilabu bora Africa imetoka ,Simba ni club ya 6 kwa ubora ikizidi hata mazembe,Zamalek na giants wengine . Kwa mantiki hiyo derby ya Simba na yanga inaenda kufa maana haina umuhimu huwezi kuwa derby na mtu ambaye yupo nafasi zaidi ya 100 Africa ,kwahiyo derby mpya ni Yanga na Azam
 
hiyo mechi Simba wanaenda kucheza kama mechi zingine za kina Dodoma Jiji ,kwahiyo hamna jipya
 
Leo orodha ya vilabu bora Africa imetoka ,Simba ni club ya 6 kwa ubora ikizidi hata mazembe,Zamalek na giants wengine . Kwa mantiki hiyo derby ya Simba na yanga inaenda kufa maana haina umuhimu huwezi kuwa derby na mtu ambaye yupo nafasi zaidi ya 100 Africa ,kwahiyo derby mpya ni Yanga na Azam
Takwimu za uongo chief
 
Kwa mujibu wa takwimu za CUF au caf ya buza?
 
Hii Match mashabiki wa Simba ndo wamepooza.. obvious wanafahami kuwa kipigo kipo palepale.. Yanga hatuna presha Kwan hii ni mechi ndo tu kwetu kama tunacheza na Mbeya kwanza kushinda ni kama binadamu kuingia kaburini tu.

Hiii mechi tushaimaliza kipindi Cha kwanza tu then kipindi Cha pili tunawaonesha soka jinsi linavyochezwa
 
Yanga haina hadhi ya kuwa kwenye derby na Simba. Derby za Dar ni Yanga, Azam na KMC.

Simba ni next level.
 
Simba sio wa kuwaza kucheza na Yanga wakati analisaka taji la shirikisho , ni kujidhalilisha , hiyo ni mechi ya kawaida tu now
 
Darby ni Yanga na Azam,Simba keshatoka huku matopeni
Darby za Simba ni Al ahly,Mazembe,Zamaleck wakubwa wenzie ambao wako pamoja top ten ya club bora Africa.
Kukosekana kwa neno "Derby" kwa kiswahili kumefanya watu wengi wasijue nini hasa maana yake kamili. Kila mtu anajiongelea tu.
 
Kukosekana kwa neno "Derby" kwa kiswahili kumefanya watu wengi wasijue nini hasa maana yake kamili. Kila mtu anajiongelea tu.
Kikubwa ni kueleweka mambo mengine ni kujipa kazi tu.Rais wa nchi hajui lugha sahihi sembuse anaowaongoza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom