Simba kushuka dimbani na Al Masry ya Misri tarehe 6 na 16 Machi 2018

Naipenda sana simba lakini nikiwaza hiyo mechi naona kazi nzito mbele yetu,ukiangalia mechi za hao majamaa YouTube ni shida
 
Mechi ya kwanza itakoyochezwa dar simba anaweza kushinda ila marudio kule misri ni bora simba muende na vikapu
 
Mechi ya kwanza itakoyochezwa dar simba anaweza kushinda ila marudio kule misri ni bora simba muende na vikapu
naona ndo mtindo mpya wa waarab, wakija kwako ukimfunga iwe 1-0, 2-1 au 1-1 ili ukienda kwake akushindilie 4-0, 5-1.
ili simba ivuke hatua inayofuata inabd mwarab ale 4-0 taifa
 
Kuitoa timu maramoja ndo unakuwa kiboko yao?

Mbali ya Zamalek mwaka 2003 Simba imeshazitoa timu za waarabu wa Algeria mara 2, moja wapo ambayo nina data kamili ni USM Al Harrach mwaka 1993 kombe la CAF robo fainali, tuliwapiga 3 - 0 bila Dar uwanja wa taifa sasa uhuru, na wao wakashinda 2 - 0 kwao 1993 CAF Cup - Wikipedia lakini hata timu za Misri ni kubebwa tu, Mwaka 1974 Africa Club Champions Nusu Fainali Mehalla El Kubra walipigwa 1- 0 Dar lakini washabiki wao walifanya vurugu kubwa sana ikiwemo kumrushia mawe kipa Mambosasa na kumtishia kisu, hatimaye nao walipata bao 1 hivyo mpira kwenda kwenye penalti 5, ambapo washabiki wa Mehalla walikaa nyuma ya goli wakati wa mikwaju ya penalti wakimfanyia vurugu Mambosasa na hatimaye Simba ikatolewa, sio hivyo tu Simba ya Joseph Kaniki ilipigwa 1 kule Misri kombe la washindi, na Arab Contractors lakini marejeo Dar Hadi halftime tayari waarabu walishapigwa 2 huku Kaniki akiwa hakamatiki yaani zaidi ya Okwi na katika hali ya kushangaza wakati wa kuanza kipindi cha pili refa akavunja mpira kwa kisingizio cha mvua ndogo sana, mechi ikarudiwa siku ya pili, demoralized Simba wakatolewa. Hata 1984 kwenye Africa Club Champions hawa National Al Ahly ni marefa tu waliibeba, baada ya kupigwa bao 2 - 1 Dar, mabao ya Mtemi Ramadhani na Zamoyoni Mogella huku mshambuliaji wao hatari no 1 kwa Africa wakati huo Mohamed el Khatib akiwekwa mfukoni kabisa na beki chipukizi wakati huo Twalib Hilal, ilibidi refa akafanye kazi ya ziada Cairo kuwabeba Al Ahly na kushinda bao 1 hivyo kusonga mbele kwa advantage ya goli la ugenini. Kwa Simba hii ya sasa El Masry out, labda Okwi au Boko moja wao awe majeruhi.
 
Back
Top Bottom