Simba inakuja na historia mpya

Simba inakuja na historia mpya

mansoorsaid

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Posts
1,498
Reaction score
286
timu ya simba imewahi kuleta rekodi mpya ya kutofungwa mwaka mzima wa ligi.mwaka huu naona itatuletea rekodi mpya kwa kutoka sare msimu mzima

hongereni uongozi
 
timu ya simba imewahi kuleta rekodi mpya ya kutofungwa mwaka mzima wa ligi.mwaka huu naona itatuletea rekodi mpya kwa kutoka sare msimu mzima

hongereni uongozi



haaaa....hhi simba karibu inatangaza ajira mpya kwa kocha....pamoja na kwenda bonden lakin bado sare?
 
haaaa....hhi simba karibu inatangaza ajira mpya kwa kocha....pamoja na kwenda bonden lakin bado sare?
Kibadeni na Julio wajiandae kuwa makocha wapya simba sc,,,
Phiri muda si mrefu atarudi kwao Zambia....
 
Ndiyo madhara ya kusajili kwa kukomoana bila kuangalia mahitaji ya timu..sasa wamepata somo.
 
timu ya simba imewahi kuleta rekodi mpya ya kutofungwa mwaka mzima wa ligi.mwaka huu naona itatuletea rekodi mpya kwa kutoka sare msimu mzima

hongereni uongozi
Kwa nini tuangalie upande mmoja tu wa kutofunga? Hatuoni pia kwamba Simba ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa kwenye ligi ya msimu huu? Huo ni mwanzo mzuri iwapo litaangaliwa swala la Simba kwa jicho zuri (optimistically). Tukumbuke kwamba 'Half empty = Half full'.
 
Nyie bado munaikumbuka tu hiyo timu?
Nani anaweza kuisahau timu iliyo: twaa kombe la Vilabu la CECAFA kwa mara ya kwanza na kuendelea kulitwaa mpaka kufikia rekodi ya kulitwaa mara nyingi zaidi, toa wachezaji wa uwezo uliotukuka na adimu kama King Kibaden na Zamoyoni Mogela, shika nafasi ya pili kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Taifa, miongoni mwa timu mbili zenye idadi kubwa zaidi ya wapenzi nchini, miongoni mwa timu chache nchini zilizoasisiwa zamani zaidi na ikaendelea kuwapo tangu wakati huo, toa viongozi bora wa kandanda nchini wanaoendelea kukumbukwa hadi leo, chimbuko la timu kadhaa nchini zikiwamo Nyota Nyekundu na Azam, shirikiana na mtani wake Yanga kutandika mindombinu ya kiushabiki wa mpira nchini, ya kwanza kwa ukanda huu kuifunga timu ya Misri nyumbani kwao na kuitoa kwenye mashindano ya Vilabu vya Afrika, shiriki kikamilifu kuwaunganisha Watanganyika kupitia kandanda katika harakati za kugombea Uhuru wao, shirikiana na wenzao wa Zanazibar hasa Timu ya Kikwajuni katika kujenga Utanzania hata kabla Zanzibar na Tanganyika hazijawa Tanzania, endelea kuwaunganisha Watanzania kupitia matawi yao yaliyoenea Tanzania nzima, sehemu muhimu ya Jiji la Dar-es-salaam mpaka kufikia watu kudhani kwamba Simba ndiyo Msimbazi na Msimbazi ndiyo Simba, zipa rangi nyekundu na nyeupe tafsiri mahsusi ndani ya Tanzania, tengeneza matukio mengi ya kukumbukwa hadi kuwa ni sehemu ya historia ya nchi (kama maajabu ya kuifunga Mufulira Wonderers 5-0 kwao licha ya yenyewe kutanguliwa 4-0 nyumbani), toa mechi zisizosahaulika kwa usisimuzi wake (kama ile dhidi ya Yanga iliyochezwa Nyamagana 1974, ........... ? Anayeyajua hayo ataisahauje?
 
Kwa nini tuangalie upande mmoja tu wa kutofunga? Hatuoni pia kwamba Simba ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa kwenye ligi ya msimu huu? Huo ni mwanzo mzuri iwapo litaangaliwa swala la Simba kwa jicho zuri (optimistically). Tukumbuke kwamba 'Half empty = Half full'.

Si kweli mkuu. Sare mbili ni point mbili. Bora kushinda moja na kupoteza moja-point tatu
 
Si kweli mkuu. Sare mbili ni point mbili. Bora kushinda moja na kupoteza moja-point tatu
Nini tafsiri rahisi ya kuwa timu hiyo haijafungwa hadi sasa? Tafsiri rahisi ni: kwa sababu haifungiki. Nini tafsiri rahisiya kuwa haijafunga hadi sasa? Tafsiri rahisi ni: haifungi. Nini jawabu rahisi ya kuondokana na hali hiyo? Ni kubaki na jawabu ya kwanza (iendelee kuwa haifungiki) na kuondokana na jawabu ya kwanza (iwe inafunga). Kwa waliosoma hesabu za 'simultaneous equations', ni kwamba ufumbuzi wa isiyojulikana (unknown) moja umeshapatikana. Kwa kuitumia hiyo, ni rahisi kumalizia ufumbuzi wa iliyobaki. Hiyo ilikuwa ndiyo hoja yangu ya msingi.
 
Mwendo wa tano tano wakuu!
Simba ina herufi 5
Phiri ina herufi 5
Imecheza game 5
Imedroo game 5
Imevuna point 5
Imefunga goli 5
Imefungwa goli 5.
Si mwendo wa tanotano huo?
 
Rekodi nyingine tunayoenda kuweka, ni kuwa mechi zilizobaki tutashinda zote, na mwisho wa siku tutachukua ubingwa bila kupoteza mechi.
 
Rekodi mpya msimu huu kwa simba! Point 26 mechi 26
 
Mwendo wa tano tano wakuu!
Simba ina herufi 5
Phiri ina herufi 5
Imecheza game 5
Imedroo game 5
Imevuna point 5
Imefunga goli 5
Imefungwa goli 5.
Si mwendo wa tanotano huo?

Hongera mkuu! Kwani upo juu.
 
Pili arudi kwao kwenye shughuli zake za kienyeji.nasikia kule kwao ni chifu mzuri tu.
 
Mwendo wa tano tano wakuu!
Simba ina herufi 5
Phiri ina herufi 5
Imecheza game 5
Imedroo game 5
Imevuna point 5
Imefunga goli 5
Imefungwa goli 5.
Si mwendo wa tanotano huo?

Kabla ya mechi ya Mtibwa ya jana Simba ilikuwa na sifa nyingine

Nafasi: 5 x 2 = 10
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom