Simba hafi, analala

Simba hafi, analala

Mwinatanzania

Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
18
Reaction score
19
Salaam Wana wa Simba,

Nilibahatika kuzaliwa katika familia ya kichifu upande wa BABA yangu na Mama yangu,kwa upande wa BABA yangu.

Ili uwe mtu maarufu ilikuwa ni lazima uwe na mashamba ya kutosha na kuyalima ili uwe na chakula cha kutosha na Ziada hasa, pia nyumbani pasikose mifugo ya kutosha , hasa ng'ombe,mbuzi na mifugo mingine pamoja na uchawi,kwa familia za kawaida hiyo ilitosha.

Lakini kwa kuwa BABU yangu alikuwa chifu wa kabila letu na ni mtu mkubwa alilazimika awe na ukwasi mara mbili au tatu ya mtu wa kawaida.

NGUVU ya Babu yangu ya kutawala ilitokana na jeshi la watu wakakamavu na misuli imara wakitumia silaha imara za jadi, na kama ungepata bahati mbaya ya kukutana askari hao wa Babu yangu usingelistahimili kusimama,ungetimua mbio.

Hilo halikutosha kwani Babu yangu alikuwa na jeshi lingine la siri, jeshi hili lilikuwa la wazee wasiopungua Kumi wenye nguvu za hali ya juu kabisa za kichawi, jeshi hili liliendesha oparesheni zake kwa usiri mkubwa sana.

Kwani kama kuna mtu anapanga jambo lolote baya zidi ya Babu yangu basi wazee hawa wataalamu wa maangamizi walipata habari na kumshambulia adui yule kwa silaha kali kabisa yenye uwezo wa kuangamiza ukoo mzima.

NGUVU na umaarufu wa jeshi hili ulimfanya Babu yangu aogopwe Sana na watu wote,hali iliyompelekea ajione kama Mungu.

Wakati mwingine wapambe wake walitapanya maneno kuwa chifu wao ana fimbo ya Nabii Musa inayompa siri zote za nchi hiyo ni mtu wa kuogopwa sana na watu wake au jamii ya kabila langu hawakuamini kama kuna Mungu mwingine zaidi yake kwani wapambe wake humuita majina mengi matakatifu yanayopatikana katika vitabu vya dini za sasa.

Ilitokea Mzee Babu alipatikana na maradhi ya mnyololo wa akili yaliyomfanya asiwe na kumbukumbu ya matukio, maradhi hayo yamjiapo kwa nguvu Babu alikuwa akizimia, tendo lile liliwastajabisha sana wale wazee wa oparesheni maalum, mwisho walisema chifu amechukuliwa na Ya tatakwazimu kupewa maono.

Baada ya siku kupita na mwili kuanza kuharibika ndipo wale wazee waliamua kuitambulisha jamii ya kabila letu kuwa chifu amekufa.

Kwa kuwa Mzee Babu alikuwa mtu wa tambo na kutosha hakuna mtu aloyetia akilini mwake kuwa chifu aweza kufa,hivyo watu wengi mno walijitokeza kwenda shuhudia kama kweli Chifu wao amekufa.

Mipango ya mazishi yalifanyika na ikaonekana chifu hawezi kwenda peke yake apewe mtu wa kumsindikiza, hivyo alitafutwa binti mzuri mrembo wa kumzika pamoja na BABU, Ukweli ni kuwa hata Mimi sikuamini kama kuna nguvu na mamlaka mengine katika kabila letu iliyozidi ile ya Babu,kumbe ndiyo DUNIA, nawaomba makabila yote mlie nami.
 
The Lion sleeps, Never dies! Forever in our hearts! Pumzika kwa amani Mwana wa Mama Tanganyika!
 
Back
Top Bottom