Hii simba kwa uchezaji huu walahi itatuongezea vidonda vya tumbo, wanachocheza wakifika eneo la mwisho mbele wanajua wenyewe na kocha wetu. Timu haina hamasa kabisa ya kupambana, wanatumia muda mwingi kuchezea mpira kuliko kucheza mpira wa malengo. Hatuoni mashambulizi yoyote ya maana. Wakifika mbele pasi 700 halafu zote hazina mashiko. Mpaka dakika hii ya 31 hakuna hata off target hata moja kwa Simba, hii inahuzunisha