YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,992
Katika wabunge wa UKAWA mbunge pekee niliyemwona kuwa yuko vizuri ni Silinde.Nimemwona katika mahojiano mbali mbali ya TV akiongea unaona kuwa anao uwezo mkubwa kuliko wabunge wengine wote wa UKAWA.
Anaongea ametulia,hana jazba na anajitahidi kuenda na maada husika tofauti na watu wanaopenda kuongea sana kama Mbatia,Mbowe,Tundu Lissu,Mnyika,Mdee,Msigwa,Godbless Lema na Kubenea.
Staili yake ya utulivu,ujengaji hoja bila jazba na kujitahidi akiwa kwenye mijadala mfano ya TV kwenda na maaada husika badala ya kuzagaa huko na huko kama hao wenzie niliowataja wanavyofanya.
Staili hiyo alikuwa nayo zamani Zitto Kabwe wakati akianza mambo ya siasa kabla ya kubadilika na kujiunga na staili za akina Mbowe nk ambazo zimeanza kumzamisha kisiasa.
Ninadhani Silinde asipokuwa mfuata mkumbo akabaki kama yeye na akajipambanua kama yeye kisiasa aweza kuja kuwa mwanasiasa mzuri tena sana na mwanasiasa bora wa kupigiwa mfano.