Silinde ajifunze ''busara'' za Lijualikali

Hapana mkuu ninafahamu mengi sana kuhusu CHADEMA na kuna mazito sana yameshatokea huko nyuma ila kuna watu walivumilia mnoo sio kuja kuropoka.

Mnyika amewahi hadi megewa mpenzi wake rasmi kabisa na kiongozi wake mkubwa ila kesho yake tu baada ya fumanizi alipotezea utadhani hamna kilichotokea!! Na amekua mtiifu mnoo kwa huyo kiongozi mpaka leo.

Huo ukomavu ndio naoongelea, changamoto zipo vyama vyote na kila taasisi duniani muhimu ni uvumilivu na utulivu kabla ya kutafuta suluhu.

Sio kejeli kwa chama kilichokubeba ukiwa huna hata mia mfukoni
 
Kwani hujui kuwa jamaa amefanya maamuzi ya kuwakomoa wachache. Wote walikuwa wanakosa la kutotii amri ya mkulu wao. Mambo ya kuongea na media ni kisingizio tu.
 
Kwani hujui kuwa jamaa amefanya maamuzi ya kuwakomoa wachache. Wote walikuwa wanakosa la kutotii amri ya mkulu wao. Mambo ya kuongea na media ni kisingizio tu.
Awakomoe kwa faida ya nani sasa? Unajua gharama waliotumia kushinda jimbo la Momba baada ya kugawanywa kutoka Tunduma? Silinde manusura aporwe jimbo kma sio nguvu ya wanachama. Kumtimua ni kuliweka jimbo rehani.

Lakini message inayotumwa hapo ni kwamba insubordination haiwezi kuwa tolerated popote pale. Na unaweza ona hta Lijualikali kaongea kwa adabu sana.

Ukilea huu upuuzi unajenga precedence mbaya sana, toka zitto atimuliwe kuna nidhamu ilikuwepo maana the message was clear hakuna mkubwa kuliko chama.
 
Mkuu zitto junior,kama kuna mtu ataendelea kubisha kuhusu hoja yako hapo juu,huyo atakuwa na ama ana tatizo la akili,au ni mbishi wa kulipwa.
Kongole na ubarikiwe.
 
Yaan hapo lumumba mkimchukia Tundu Lissu ndo una conclude eti wengi tunamchukia kwa taarifa yako Tundu Lissu anapendwa kuliko hata huyo mliomgeuza mungu wenu hapo lumumba
 
Kama huna cha kuchangia kuwa observer tu kma wengine.

JF ya 2009 huwezi kuta comment ya hvi.


Mkuu, JF ya sasa, hakuna KUSHAWISHIANA KWA HOJA. Mtu mwenye msimamo fulani, hata aeleweshwe kwa ujuzi wa kiasi gani, ATAJIFANYA HAKUELEWI ulichosema.

Ukifuatilia karibia wote wanaomuunga mkono Silinde, ni wale siku zote wakitakiacho mabaya chama chake.

Kwa ufupi, hizo adhabu walizopewa, wanastahili. Hivi Wabunge wa CCM, wangekubaliana makubaliano kama hayo, kuna mtu angekiuka?

Sina shaka inakumbukwa msukosuko walioupata wale wabunge wa CCM waliotaka kwenda kumtembelea Mheshimiwa Lema kule gerezani, tofauti na matakwa ya Mwenyekiti wao.

Kwa kifupi, anaponzwa na hayo maneno maneno kwenye vyombo vya habari, pamoja na Bungeni.

Alivyokuwa MJINGA, anadai alipelekwa na WAPIGA KURA huko Bungeni. Kama ingekuwa ni hivyo, JPM bila Chama kutumia nguvu, asingepata nafasi ya kuwa mgombea, bali angekuwa Lowassa, ambaye alikuwa na kundi kubwa lililokuwa linamuunga mkono.
 
Nini maoni yako kwa sasa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…