Sikuwa shabiki wa Mayweather ila ubaguzi aliofanyiwa UK nahamia team yake

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,125
8,628
Sikuwa naumiza akili zangu kuhusiana na ubaguzi wa ngozi kwani sikuona umuhimu wowote na faida yeyote. Kuna pambano la ngumi litafanyika August 26 kati ya mwana masumbwi kijana Mayweather na Conor McGregor. Wameanza kulitangaza onyesho hilo kwa ubunifu na maandalizi ambao kwa kweli wezetu wako juu sana. Matangazo yao ni live wakiambatana na wanamasumbwi hao pamoja na timu zao. Walianzia Las Vegas na ukweli hapakuwa na ubaguzi wowote (Hongera USA). Jana walikuwa London na hapo ndipo nilishuhudia kila ishara za ubaguzi toka kwa kadamnasi huku Mayweather akiwa amempa nafasi kubwa McGregor kuongea bila kuingilia hadi alipomaliza. Si hivyo tu McGregor alitumia lugha za kukashifu Uafrika (rangi nyeusi) huku akishangiliwa kama vile anafanya jambo sahihi. Nilikuwa Team Manpac sasa nahamia kwa black mwezangu Mayweather.
NB; Mugabe usilegeze kamba.

Sukumaland
 
Dah

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini wengine hawabagukiwi why yeye ?


Mayweather nyodo zake ndio zinakera haki yake kubaguliwa

Sent from my IK-644 using JamiiForums mobile app
Umeelewa nilichoandika? Sifa mojawapo ya wanamasumbwi au wanamieleka ni kuwa na mdomo mchafu (maneno ya kuudhi) sasa nyondo za Mayweather na ubaguzi wa rangi vinaingiliana vipi? Ingia hata YouTube kama hukuangalia live uone yaliyokuwa yanaendelea. Baloteli amekuwa akikubwa na ubaguzi je nayeye ni Mayweather?

Sukumaland
 
Video: Mayweather, Siwezi kusaidia Afrika kwa sababu haina mchango wowote kwenye mafanikio yangu

Mtoa thread umesema utamshabikia mayweather sababu amepata kadhia ya ubaguzi UK nakukumbusha huyo mayweather aliongea shit kuhusu Africans wakati yeye ni Black

Huyu jamaa nyodo zake ,misifa zake haki yake kubaguliwa
Siwezi kumjaji mtu kwa kauli zake, Mayweather ashawahi kukorofishana na kutaka kuzipiga na baba yake Gym. Nazungumzia kauli za kukashifu Uafrika na sio tabia ya TMT ya Mayweather

Sukumaland
 
Siwezi kumjaji mtu kwa kauli zake, Mayweather ashawahi kukorofishana na kutaka kuzipiga na baba yake Gym. Nazungumzia kauli za kukashifu Uafrika na sio tabia ya TMT ya Mayweather

Sukumaland
Napata ukakasi kuhusu huo ubaguzi unaouzungumzia,mayweather alibagua wengine kwa kauli,na yeye kabaguliwa kwa kauli hilo tu.

bichwa la kambale
 
Sijawahi acha kumshabikia na hajawahi kubebwa jamaa ngumi anazijua kumbuka ngumi kama mpira tu unaweza kupiga chenga nyingi ila kama hakuna goli sio ushindi May amekuwa akifunga goli na sio chenga hawezi pendelewa kwa mashindano yote hayo aliyoshinda lazima hata wanao pigana nae wangekataa maana kila mtu anataka kushinda

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Hizo ni tambo tu ,katika masumbwi hilo ni jambo la kawaida kabisa.Chukulia mfano mzuri tu hapa bongo jinsi wana masumbwi wanavyo pigana vijembe ,ingekuwa kwenye netball/volleyball n.k mwenyewe ningeliamsha dude!.

Task Force12
 
Pamoja na kuangalia mapambano kadhaa, bado sijaiona ngumi inayompa Meywether ushindi.
Ni mjanjamnjanja mwenye vingumi vya kudokoadokoa
tu.
Kitu ambacho mabingwa wa ngumi nzito kama Mike Iron Tyson huwa wanaondoka katikati ya pambano la Meywther.
Hawauoni mchezo wa ngumi kama unavyotakiwa kuwa.

Pale ni Pesa Zaidi.
 
Sijui kwann sisi waafrika tunajipendekezaga kwenye mambo yasiyotuhusu ...... Huyo may hawapendi waafrika kweli kweli ......sio May tuu Bali hawa wenzetu waliokuwa huko mda mrefu ukifika ww unatoka afrika watu watakaokupokea ni watu waliofikia ......naomba aliyopo huko au ambaye amefika USA atueleze ...... Na mm napenda UFC na mshabiki namba moja Wa Conor .....PIGA uyooo ata ngekua Wa blue ......

Sent from my A0001 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na kuangalia mapambano kadhaa, bado sijaiona ngumi inayompa Meywether ushindi.
Ni mjanjamnjanja mwenye vingumi vya kudokoadokoa
tu.
Kitu ambacho mabingwa wa ngumi nzito kama Mike Iron Tyson huwa wanaondoka katikati ya pambano la Meywther.
Hawauoni mchezo wa ngumi kama unavyotakiwa kuwa.

Pale ni Pesa Zaidi.
kumbe...jamaa mjanjamjanja tu
 
Halafu huyp nguruwe pori kaenda mbali kamuhusisha mbishi, mtoto pori 50 cent. Navomjua 50 halazagi damu, namsubiria amchane, ampe makavu live.

Hata mimi nimehamia team money maker, na kwa jeuri zaidi katema shit while. Myweather karusha ela jukwaani.

Uuuuuuwiiiiiiiih
 
Back
Top Bottom