Baada ya mimi na kikosi i mean marafiki na baadhi ya ndugu zangu kufika katika mji wa stone town Unguja, ikabidi tutafute hotel ya kufikia, tukapata hoteli moja kubwa na maarufu kisiwani humo, baada ya kila mtu kuridhika na chumba alichopata tukasema ngoja tutoke nje tuangalie mazingira jinsi yalivyo, kutokana na uduni wa sehemu za kuuza vinywaji vilivyochachushwa yaani namaanisha pombe ikabidi tuagize pale pale hotelini, story zikawa zinaendelea mizaha ya hapa na pale, kwa mbali kutoka mezi tuliyokuwa tumekaa mimi na wenzangu nilimwona kijana mmoja ambae yeye ni mtangazaji maarufu sana katika kipindi cha mitindo kinachorushwa na channel moja hapa nchi ambayo inasifika kwa kuwa na burudani nyingi.
Hiki kitu ndicho kilichonishawishi mpaka niandike huu UZI, huyo kijana ambaye ni mtangazaji alikuwa na kampani ya mzee mmoja wa kizungu japo kwa bahati mbaya sikuweza kujua ni raia wa nchi, walikuwa wamekaa pozi la kawaida kama marafiki ambao wameshibana, kusema kweli sikujali kile kitendo ingawa siku za nyuma niliwahi kukutana na huyu mtangazaji maeneo ya break point pale K'nyama na kusalimiana nae kwani alikuwa na mtu ambaye ninayefahamiana nae, ile siku ya kwanza jamaa yangu aliyekuwa naye wakati ananitambulisha nilitia shaka kutoka na jinsi alivyokuwa anaongea na kingine body language yake ilinipa mashaka yaani kwa kifupi nilimhisi kama mtoto si ridhiki lakini nikajisemea moyoni kwamba inaweza ikawa ni malezi na makuzi tuu aliyokulia huyu mtangazaji.
Kwa kuwa nilikuwa sehemu ile ya ugenini nikaona sio mbaya nikamsalimie ili tuweze kukumbushana, nikafika kwenye meza yao na kuwasalimia na yeye pia alinisalimia kwa kunichangamkia, akanitambulisha kwa yule mzee wa kizungu kwamba ni rafiki yake, basi na mimi pia nikamkumbusha kidogo akasema kwamba ananikumbuka, baada ya hapo mimi nikarudi kwenye meza ilikuwa na kampani yangu na story zikaendelea lakini mimi binafsi taa nyekundu ikaanza kugonga kutoka na mazingira na pia ile siku ya kwanza nilipomuona, ikabidi nimtafute mhudumu mmoja nifanye kama kumpeleleza kuhusiana na yule jamaa, basi nikamuagizia kinywaji dada ambaye ni mhudumu kisha nikasogea pembeni mwa meza niliyokuwa na kuanza story nae, nikamweleza kwamba anawafahamu wale watu wawili ila wakati huo nilihama eneo ambalo wao haikuwa rahisi kuweza kuniona mimi, sio siri yule dada aliniambia bila chenga kwamba huyo baba ninayemuona ndiye bwana wake na huyo kijana na akasema sio mara yao ya kwanza kuja katika hoteli japo huwa ni vipindi tofauti lakini wahudumu wa hapo wameshawashuhudia nyakati za usiku wakipeana mahaba utafikiri ni mtu na demu wake, sio siri nilihisi kama MOYO wangu umepasuka kutokana na maneno ya yule dada, basi nikamwambia dada nashukuru japo alitia shaka akadhani mimi ni mpelelezi au mwandishi wa habari kwaiyo nikamtoa shaka. baada ya hapo mimi nikaendelea kusherehekea sikukuu ya wapendanao na company yangu ila nikasema lazima niwasilishe hili suala jukwaani.
Huyo mtanganzaji jina lake linaanziwa na D pia katika hicho kipindi hicho cha Fashion anatangaza na mwanamke ambaye ana asili kama ya kenya ambapo katika hiyo Channel moja ya majina yake kuna NAMBA katikati, nimeona nicmtaje hadharani kutokana na sababu za kiusalama pia ila najua wafuatiliaji wa channel zetu hapa nchini watakuwa wameshajua ni nani nayemzungumzia. Ni hayo tuu wapendwa nawatakia jioni njema.