Siku ya Mwisho / The Last Day - Part 2

Siku ya Mwisho / The Last Day - Part 2

Joined
Jan 15, 2013
Posts
77
Reaction score
28
Katika zile dalili kubwa kumi za mwisho za kuashiria ukaribu wa siku ya mwisho/Judgment Day/Qiyamah (Rejea part 1 ikiwa haukupitia), kuna dalili kubwa kadhaa ambazo zimesha jitokeza kulingana na tafsiri/mtazamo, dalili hizo ni;
  1. Kuchomoza jua Maghrib na kuzama Mashariki
  2. Ujio/Uwepo wa Ant Christ/Mpinga Kristo/Masih Dajjar - itaelezewa katika Part 3
  3. ...
Jua lilisha chomoza Maghrib muda mrefu kwa wenye upeo wa kufikiri na kwasasa bado liko njiani katika msafara wake kuelekea kuzama mashariki,

Kwa mtizamo huu; jua lililokusudiwa hapa sio Jua kwa maana ya Sun ila ni Jua kwa maana ya utamaduni/ustaarabu,

Katika mtizamo huu; upeo wa akili unakataa kuwa jua lililokusudiwa ni Jua kwa maana na Sun kwasababu Muumba aliliumba Jua=Sun na akaliwekea utaratibu wa Kuchumoza mashariki na kuzama Maghrib kama ilivyonukuliwa na kitabu chake Qur 2:258 nae hana sifa ya kubadilisha badilisha kwani huumba katika namna iliyobora siku zote Qur 30:30 hivyo hadithi ikitafsiriwa Jua lililo kusudiwa ni Sun basi hadith itakuwa imepingana na aya na si sifa ya hadith kupingana na aya na kama hivyo ndivyo tafsiri ya hadithi inakuwa na mantiki zaidi ikiwa tafsiri sahihi ya Jua ni Utamaduni/Nidhamu/Mwenendo wa maisha,

Kwa mujibu wa historia, baada ya Yesu/Issa kuondoshwa katika uso wa dunia na kupita kipindi, dunia ilikuwa katika kiza kikubwa, kiza kwa maana ya kuwa na tamaduni/ustaarabu mbovu na usiopaswa kuigwa (Dark ages/Jahiriya period) baada ya hapo Muumba akaleta nuru nyingine Qur 03:184, 61:08, ... nuru=mwanganza=kinyume cha kiza=Jua, kwa mujibu wa aya kadhaa nuru=Qur an, nuru = Uislamu.

Jua lililo tabiriwa kuchomoza magharibi ni utamaduni wa kimagharibi/western civilization atamaduni ambao ni sawa na Jua lisilo la kawaida na mwangaza wake si wa kawaida, mwangaza unaobadili halali kuwa haramu, mwangaza wa kuakisi haramu kuonekana halali, mfano wa mambo yaliyo letwa na jua/ustaarabu wa magharibi ni;
  1. Uchumi wa tajiri kuwanyonya masikini - Capitalism,
  2. Elimu ya mazingira inayofundishwa kwa mtazamo wa kumkanusha muumba - Circular education
  3. Ndoa za Jinsia moja,
  4. Kutembea uchi/nusu uchi - wanaume na wanawake,
  5. Utowaji wa mimba kiholela - Nchi zilizoendelea kwa kiasi kikubwa,
  6. Wanaume kujipamba mapambo ya kike - kusuka na kuvaa herini,
  7. Mengineyo...
Maovu haya/utamaduni huu wa kimagharibi ndio utamaduni ambao unaonekana unafaa na wengi katika jamii na huonekana ndio njia ya mafanikio na utamaduni huu ndio jua lililo tabiriwa kuchomoza magharibi.

Katika kiswahili; Jua lilizozungumza katika hadithi limetajwa kama NAHAU na maana halisi ni utamaduni/utaratibu wa maisha katika jamii.

Muumba ndio mjuzi zaidi...
 
Wenye imani za utabiri wa mambo ya jua kuchomoza magharibi ndio mnaongoza kuwaogofya watu msivyoweza kubadili chochote!

Utabiri huo unaotokea sasa ulikuwa kwa mamlaka ya nani?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom