muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
Tukiwa tunaadhimisha kilele cha siku ya mama duniani, hapa kwetu Tanzania kuna mambo hatuna budi kuwapongeza wanawake lakini vilevile kuna changamoto kwa wanawake pia.
Siku hii nairudisha nyuma ingawa sikumbuki ilikuwaje siku ambayo naingia duniani kwa mara ya kwanza, baada ya kutunzwa na mama miezi tisa tumboni mwake, wakunga na madaktari walivyoshirikiana na hatimaye mwenyezi akaweka baraka zake na kufanya mi leo niwepo hapa. "Ahsante mama"
Lakini vilevile naangalia wakina mama ambao wamekatisha maisha ya viumbe kama mimi ambao baada ya kuwatunza miezi tisa tumboni na kuvumilia changamoto zote lakini bado baada ya kuzaa watoto aidha waliwaua au kuwatupa chooni wakiwa hai na kusababisha watoto kufa kifo cha kikatili sana, naumia sana, kwa wakina mama waliowahi au wenye matarajio ya kufanya ukatili huo.
Bado kuna wakina mama wanasaidia au wenyewe wanaiba watoto wa wenzao mahospitalini, mtoto ambaye ametunzwa na mwanamke mwenzake miezi tisa tumboni alafu kirahisi tu anaiba dahhhh!!! Inauma sana.
Bado kuna wakina mama wamekosa huruma ya kike kabisa wameingia kwenye makundi ya kijambazi na kufanya matukio makubwa ya kikatili, mimi nafahamu watu pekee walioumbwa na huruma ni mwanamke kwasababu ndiye kiumbe pekee anaemjua vizuri binadamu kwasababu alimtunza kuanzia tumboni hadi duniani na hadi pale binadamu yule atakapoanza kujua baya na zuri ndipo kidogo atatoka kwa mama lakini bado ni mlezi wa kipekee kwa mtoto hadi mwisho wa maisha yake, inauma kuona mama huyo anajiingiza kwenye makundi ya kikatili kwa binadamu wenzake.
Ingekuwa vizuri pangekuwa na makongamano ya kutosha kwa wasichana wanaokuwa kufundishwa utu wa mwanamke kwa jamii, hii ingesaidia sana wasichana ambao wanaokuwa wawe kwenye misingi iliyobora, waishi kwenye makuzi ambayo wataepukana na mazingira hatarishi ambayo wengi wanajikuta wanakutana nayo na kupata mimba wasizotarajia na kusababisha kutoa mimba hizo na wengine kupata ulemavu na kutozaa tena na kujikuta wanakuwa makatili na wengine kufikia hatua ya kuiba watoto wa wenzao.
Wakati nakuwa mama yangu alipenda kuniambia msemo flani "mwanangu kuwa uyaone" nashukuru kuna mambo nayaona hususani kwenye nchi yangu, nashukuru mungu sioni maghorofa tu 'lah asha' nimeona hadi ma ubunifu ya binadamu kule baharini shilingi ndogo inazama lakini meri kubwa inaelea, nashukuru nimeona mama yangu.
Sina budi kushukuru kwa kuona mambo mengine ambayo ni nadra kuyaona nchi nyingine, hapa kwetu Tanzania sehemu nyeti ambayo ndiyo inapanga bajeti ya nchi, ambayo ndio inatunga sheria za nchi na ndiyo wananchi wote wanawakilishwa hapo, sifa ya huyo mwakilishi anahitajika ajue kusoma na kuandika tu na tuna imani na bunge kuwa litakuwa bomba kwa maendeleo ya watanzania.
Ndiyo nchi pekee ambayo imewatoa watumishi wenye vyeti feki makazini na wenye dhamana ya kufanya mambo hayo imetafsiri watumishi wa serikali sio wa wakuu wa mikoa na wilaya kwahiyo katika uhakiki huo hawajahusishwa ingali Rais wa jamhuri ya muungano wakati anawateua alihitaji wote waende na vyeti na alivihakiki na kuna habari kuna wengine hawakupata hizo nafasi kwasababu ya matatizo yao ya vyeti, naendelea kuyaona mama yangu ndani nchi yangu ambayo umenizaa kwenye ardhi yake, Rais ana mambo yake na waziri anàkuja na tafsiri yake.
Mama yangu nimeona pia jinsi ulivyoangaika mwanao nipate elimu kwa kujibana sana ukiwa unaamini siku moja niwe mtu mkubwa serikalini au ikiwezekana nishike nafasi za juu ndani ya nchi yangu naomba nikuambie mama yangu mambo yamekuwa tofauti sana, ndani ya nchi hii kusoma sio dili tena unaweza ukaghushi, ukatumia jina ambalo sio lako ukachaguliwa kuwa mkuu wa mkoa tena mkoa mkubwa wenye wasomi wengi kama dar es salaam ilimradi ujue kusoma na kuandika lakini wakati huohuo wale waliotafsiriwa kuwa ni watumishi wa umma kuna wengine wamefungwa na wengine wamefukuzwa kazi bila kupata kiinua mgongo wala mafao yoyote, mama yangu haya yote yanafanyika ndani ya nchi moja.
Mama kuna wakati nilikuwa nashangaa mambo yanavyoenda nakumbuka uliniambia "nikishangaa ya mussa nitayaona ya firauni" ehhhhhhh nayaona kila kona watu wanalalama wanaongelea mambo ya rambi rambi, mara wanakumbusha like tetemeko kule kagera na maneno mengi lakini mama yangu ngoja niendelee kukua ahsante mama yangu [HASHTAG]#ntabakitanzania[/HASHTAG]
Happy mother's day