kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 735
Naomba wanawake na wanaume kwa pamoja humu jf tujadili changamoto zinazowakumba hawa jinsia ya kike hasa wanapokuwa hedhini, kwani baadhi wamekuwa wakiteseka sana kinapofika kipindi hicho pia kumekuwa na changamoto za miundombinu kwa walioko mashuleni hata makazini wapo hadi wanaoachishwa kazi kwa sababu za kupunguza ufanisi wanapofika hedhini kila mwezi.
Kama kutakuwa na maoni, mapendekekezo, ushauri wa namna ya kupunguza hizi changamoto kwa jinsia ya kike pia unaweza sema ili taasisi au watu binafsi waishi vizuri na hii jinsia ya kike popote pale kutokana na maumbile yake ki bailojia.