albuluushiy
JF-Expert Member
- Oct 2, 2013
- 1,404
- 687
HATIMAYE ile ndoto ya
kuunganisha Vyama vya
Tanganyika African National
Union [TANU] cha Tanganyika
na Afro-Shirazi Party [ASP] cha Zanzibar, ikatimia; Februari
tano5, 1977. Wazo la kwanza
la kuvunja TANU na ASP
lilitolewa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Septemba 1975 mjini Dar es
Salaam katika kikao cha
pamoja cha Kamati Kuu za
TANU na ASP, zilipokutana
kujadili suala la uchaguzi wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano. Rais wa Awamu ya Pili
Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe
Mwinyi, alikubali wazo hilo
kimsingi, lakini akasema
chama chake kilihitaji muda
zaidi kufikiria. Wazo hilo lilijadiliwa Bara na Visiwani
hivi kwamba, mwaka mmoja
baadaye, Oktoba 1976,
Vyama hivyo viwili
vikakubaliana kuungana.
Chama kipya kilichozaliwa kiliitwa Chama cha
Mapinduzi [CCM] bila kuwa
na tafsiri ya Kiingereza, baada
ya Wazanzibari kusimama
kidete kwamba,
wasingekubali bila neno Mapinduzi kuonekana
kwenye jina la chama kipya ili
kuendeleza historia ya
Mapinduzi yaliyoleta uhuru
wao, Januari 12, 1964. Ilikuwa ushindi pia kwa
Wazanzibari kushinikiza na
kufanikiwa kwamba, chama
kipya CCM, kizinduliwe
Februari 5, 1977, mwezi na
tarehe ya kuzaliwa kwa ASP, kilichotokana na Muungano
wa Vyama vya African
Association [AA] na Shirazi
Association [SA], kuunda
Afro-Shirazi Party ASP.
Kuundwa kwa CCM kulirekebisha Katiba ya Pili ya
Muda [Second Interim
Constitution] ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar,
kuipa Serikali ya Muungano
kinadharia, mamlaka makubwa kwa mambo ya
Nje, Ulinzi, Polisi, Mabenki,
Biashara ya Nje na Mikopo,
Kodi na Ushuru wa Forodha;
lakini kivitendo, Zanzibar
iliendelea kivyake kwa mambo hayo bila kujali Katiba
wala matakwa ya Mkataba
wa Muungano. Hii ilionesha dhahiri kwamba
Wazanzibari waliingia
kwenye muungano na
kuunganisha vyama shingo
upande. Ikumbukwe, Baraza
la Mapinduzi na ASP vilikuwa na kauli turufu kwa Serikali,
Wazanzibari na kwa
Muungano kiasi cha
kuonekana kero kwa
mustakabali wa Muungano
hivi kwamba, kuunganishwa kwa TANU na ASP ilikuwa
mkakati na mbinu muhimu
kwa Mwalimu kuleta udhibiti
na utulivu kwa Muungano
Visiwani. Kuanzia Februari 1977 hadi
Aprili 1983, fungate ya CCM
ilikuwa ya furaha; lakini pale
Mwalimu Nyerere alipoleta
pendekezo lingine la
marekebisho ya Katiba, kuliibuka zahama na tafsiri
hasi Visiwani juu ya
Muungano, kwamba
Mwalimu alikuwa na nia ya
kuimeza Zanzibar. Matokeo yake, Wazanzibari
wakaanza kulalamika na
kuelezea hisia zao kupitia
vyombo vya habari, ikiwamo
redio mashuhuri ya mafichoni
Kiroboto tapes, iliyomwaga matusi na kashfa mbali mbali
kwa Muungano,
Watanganyika na kwa Rais
wa Muungano. Kufuatia
tafrani hiyo, na kwa
kuzihurumia sauti za Wazanzibari, Jumbe aliomba
mawazo ya Makatibu Wakuu
wa Wizara zote Visiwani juu
ya Muundo wa Muungano
unaotakiwa, ambapo karibu
wote walipendekeza Muundo wa Serikali Tatu ili kulinda
maslahi ya Zanzibar ndani ya
Muungano. Kwa kuzingatia malalamiko
hayo, Rais Jumbe alimrejesha
kwao Tanzania Bara,
aliyekuwa Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar, Jaji
Damian Lubuva [sasa Mwenyekiti, Tume ya
Uchaguzi nchini NEC]; badala
yake akamwita na kumteua
raia wa Ghana, Kway Swanzy,
na kumpa uraia kwa njia ya
usajili. Mwalimu Nyerere aliona Jumbe akiupa kisogo
Muungano na kuamua
kutumia umahiri wake
kuokoa jahazi. Alijua vyema
udhaifu wa Wazanzibari
ulikuwa kwenye umoja dhaifu na utaifa legelege
kuweza kufananishwa na mti
usio na mizizi. Itakumbukwa pia kwamba,
katika kipindi cha fungate
mpya ya CCM, Jumbe alikuwa
mstari wa mbele katika
kutetea Muungano, akawa
kipenzi cha Mwalimu, aliyetumika kwa uhuru zaidi
ikilinganishwa na enzi za
utawala wa mkono wa
chuma wa hayati Abeid
Karume. Kwa sababu hiyo,
Jumbe alijiona ni mrithi mtarajiwa wa Nyerere asiye
na mpinzani kwenye Serikali
ya Muungano. Na kwa sababu
ya kuelekeza nguvu na juhudi
kubwa kwenye Muungano
kuliko nyumbani, alijitengenezea maadui wengi
Visiwani kiasi cha
kutuhumiwa kaolewa
Tanganyika Mji Mwema,
Dar Es Salaam. Kufikia mwishoni mwa 1983,
Jumbe alikuwa amepoteza
imani na hadhi kwa
Wazanzibari na Wasaidizi
wake wa karibu; uongozi
wake ulijenga vikundi vyenye uhasama ndani ya Serikali. Ni
kwa sababu hizi, Jumbe
alipoonekana kutaka
kuchokoza Muungano kwa
mbinu za Kizanzibari, ilikuwa
rahisi kwa Nyerere kumngoa madarakani. Hatimaye, saa ya kumngoa
Jumbe kwa kuthubutu
kukanyaga patakatifu
ikawadia, Januari 1984.
Kwenye Kikao cha
Halmashauri Kuu ya Taifa [NEC] ya CCM mjini Dodoma,
kilichoitishwa kwa dharura
kujadili agenda ya Jumbe
kuhoji uhalali wa Muungano
kwenye Mahakama Kuu;
Jumbe alielezewa kuwa kiongozi dhaifu na msaliti;
akavuliwa nyadhifa zote za
kichama na kiserikali katika
Jamhuri ya Muungano na
Zanzibar. Tetemeko hili la kisiasa
liliwakumba pia Wasaidizi
wake wa juu; wakiwamo
Waziri Kiongozi, Ramadhan
Haji; Waziri wa Nchi, Aboud
Talib; na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali wa zamani, Wolfgang
Dourado, akatiwa kuzuizini
kwa miezi sita. Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Ulinzi, Seif
Bakari, na ambaye alimtetea Jumbe kwenye NEC kufa na
kupona lakini bila mafanikio,
aliwekwa chini ya ulinzi Bara,
na baada ya hapo alipelekwa
Geita kuwa Mkuu wa Wilaya.
Bakari alikuwa chaguo la Wazanzibari kumrithi na
kuendeleza sera za Karume,
kama Nyerere asingeingilia
kati na kumteua Jumbe
badala yake. Nafasi ya Jumbe
ilichukuliwa na Ali Hassan Mwinyi; na Seif Shariff Hamad
akateuliwa Waziri Kiongozi. Kutunguliwa kwa Jumbe
pamoja na Waziri Kiongozi
wake mjini Dodoma,
kulijenga hali ya kutoelewana
miongoni mwa viongozi wa
Zanzibar kwa kundi moja kuunga mkono hatua hiyo
kama njia ya kuondoa
vikwazo kuelekea
maendeleo; na kundi jingine
kuona kama mbinu ya kisiasa
ya kujitwalia madaraka bila haki ili kuirejesha Zanzibar
enzi za kabla ya ukoloni. Kwa
sababu hii, uongozi wa
Zanzibar uligawanyika kwa
misingi ya Washindi na
Washindwa, huku kundi la Washindwa likitupa
lawama kwa Mwalimu kwa
kucheza mchezo mchafu. Mgawanyiko huu ulizaa
makundi mawili: kundi
lililofanikisha kungolewa
kwa Jumbe likijiita The
Frontliners [Wanamstari wa
mbele] kwa maendeleo ya Zanzibar, na lile lililopinga
kungolewa kwake likijiita
The
Liberators [Wakombozi],
kwa maana ya wakombozi
na walinzi wa Mapinduzi ya Zanzibar, huku likiapa
kulipiza kisasi kutikisa
mhimili Nyerere. Hatimaye muda wa kufanya
hivyo ukawadia, pale Nyerere
alipowauma sikio
wapendwa wake kwamba,
muda wake wa kungatuka
ukifika, angependelea Rais atoke Zanzibar. Mchakato wa
kumpata mrithi ulipoanza,
idadi ya wagombea
ilidhibitiwa kuwa watatu tu:
Ali Hassan Mwinyi, wakati
huo akiwa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa
CCM Taifa na pia Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya
Muungano; Rashid Kawawa;
na aliyekuwa Waziri Mkuu na
Mwanadiplomasia wa Kimataifa, Salim Ahmed
Salim. Kati ya watatu hao, ni
Kawawa pekee hakuwa
Mzanzibari; kuingizwa kwake
kulionekana ni mchezo wa
karata wa kisiasa. Kufumba
na kufumbua Mwalimu akaanzisha mchezo wa
karata ya kisiasa kupitia NEC
na Kamati Kuu [CC] ya CCM
kumpata mrithi aliyemtaka. NEC na CC ziligubikwa tangu
mwanzo na makundi mawili
hasimu, yenye kuwania ukuu
kwenye siasa za Zanzibar.
Kundi la Frontliners
liliundwa na wanasiasa wa mrengo wa kimaendeleo na
usasa, kama kina Salim
Ahmed Salim, Seif Sharrif
Hamad [Waziri Kiongozi],
Adam Mwakanjuki, Isaac
Sepetu, Shabaan Mloo, Ali Salim na Ali Haji Pandu, wote
Wajumbe wa NEC. Kundi la Liberators,
watetezi wa sera za hayati
Abeid Aman Karume,
liliongozwa na Brigedia
Abdullah Said Natepe;
wengine wakiwa ni Ali Mzee, Hassan Nassoro Moyo,
Mohamed Seif Khatib na
Salmin Amour. Kundi hili
liliendesha pia kampeni za
kutolewa kizuizini kwa Seif
Bakari na Hafidh Suleiman kwa jeuri yao ya kutetea
Jumbe asingolewe. Kwenye Liberators
walikuwamo pia
Wanausalama na Wanajeshi
wastaafu. Mashuhuri
miongoni mwao walikuwa ni
aliyekuwa Waziri Kiongozi enzi za Jumbe, Brigedia
Ramadhan Haji na Brigedia
Khamis Hemed. Kundi hili
lilikuwa na chuki dhidi ya
Salim tangu mwanzo. Kwa mfano, mwaka 1982
wakati Salim alipoteuliwa
kuwa Waziri wa Mambo ya
Nje, Natepe [wakati huo
Waziri katika Ofisi ya Rais
mwenye dhamana ya Usalama wa Taifa] na Ali Mzee
[Waziri, Ofisi ya Makamu wa
Rais], walikwenda kwa
aliyekuwa Waziri Mkuu,
Edward Moringe Sokoine,
kudai walikuwa na maagizo kutoka kwa Jumbe na Seif
Bakari kusimamisha uteuzi
wa Salim. Walitoa sababu
mbili: moja kwamba
kulikuwa na makubaliano ya
siri tangu enzi za Karume, kwamba Wanachama wa
zamani wa Vyama vya Siasa
Visiwani mbali na ASP,
wasipewe uongozi wa juu
wa kisiasa katika Serikali ya
Mapinduzi wala Serikali ya Muungano. Salim Ahmed Salim alikuwa
mmoja wa Viongozi Wakuu
wa Chama cha Umma Party,
kilichoratibu kwa mafanikio
Mapinduzi ya Januari 12,
1964. Kufuatia kuundwa kwa Serikali ya mseto wa Vyama
vya Afro-Shirazi na Umma
Party mwezi huo, aliteuliwa
kuwa Balozi wa Zanzibar
nchini Misri, akiwa na umri
mdogo wa miaka 22 tu. Sokoine hakukubali kumeza
upuuzi huo, akawatimua
Natepe na Mzee wasionekane
mbele yake; nyota ya Salim
ikazidi kungara. Na Sokoine
alipofariki kwa ajali ya gari mwaka 1984, Mwalimu
alimteua Salim kuwa mrithi
wake. Kitendo hicho kilifanya
Liberators wavimbe kwa
hasira na chuki; wakaanzisha
kampeni nzito Bara wakidai kwamba Salim hakuwa na
ushawishi wa kisiasa
Visiwani, na kwamba
angeshirikiana na Ma-
Sheikh wa Kiarabu wa
Ghuba kurejesha ubepari nchini; wakijua kwamba
Salim alikuwa Msoshalisti wa
kutupa tangu enzi za ZNP na
Umma Party kusababisha
baadaye akose kushika nafasi
ya Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kura [moja
tu] turufu [veto] ya Marekani
katika kinyanganyiro cha
nafasi hiyo. Hawakujua pia kuwa siasa na
sera za Tanzania wakati huo,
zilikuwa zimeanza kufungua
milango kwa Mataifa ya
Kiarabu. Kwa mfano, kwa
mara ya kwanza, Saudi Arabia ilikuwa imefungua Ofisi ya
Ubalozi Jijini Dar es Salaam;
na vivyo hivyo kwa Tanzania
katika nchi nyingi za Kiarabu. Kuona hoja yao haikuwa na
mashiko, wakageuza kibao
kwamba, Salim alihusika
katika kifo cha Karume,
wakati wakijua kipindi hicho
alikuwa Balozi nchi za nje, na kamwe jina lake halikuwamo
katika orodha ya
walioshitakiwa. Mkakati wa
kumchafua Salim uliandaliwa
na kusimamiwa kwa ustadi
mkubwa na Nassoro Hassan Moyo kwa kushirikiana na
Natepe na kuwashirikisha pia
Ramadhan Haji, Ali Mzee na
Aboud Talib. Moyo aliratibu mkakati huo
kwa kushirikisha pia
Wajumbe wa NEC wa Bara,
kwa kuunda kambi
iliyoongozwa na hayati Paulo
Bomani na Getrude Mongella. Nyerere alipendelea Salim
amrithi; alijua pia hujuma
aliyokuwa akifanyiwa na
kambi ya Liberators, lakini
hakutaka kuonesha kumpigia
kampeni. Mwinyi aliombwa na Kambi
ya Front liners kumuunga
mkono Salim siku ya uteuzi,
wakadhani wamemshawishi
vya kutosha asiingie kwenye
kinyanganyiro. Ahadi yake iligeuka shubiri kwao siku
Kamati Kuu ilipokutana,
Agosti 12, 1985 kuteua
wagombea wa nafasi ya Rais
wa Muungano na wa
Zanzibar. Kawawa, kama ilivyotarajiwa, alijitoa katika
kinyanganyiro; Mwinyi na
Salim wakatolewa nje ili
wajadiliwe kwa faragha. Ilivyotokea, majadiliano
yalijikita kwenye sifa za
Mwinyi pekee na Salim
hakujadiliwa kabisa, pengine
kwa kuona kwamba alikuwa
na sifa zilizotakiwa na za ziada. Liberators
hawakulazia damu ukimya
huo juu ya Salim; huku Moyo
na Natepe wakiongoza kwa
hoja. Akazungumza Getrude
Mongella; kwamba, kumruka
Mwinyi ambaye alikuwa
Makamu wa Rais na pia
Makamu wa Mwenyekiti wa
CCM Taifa, ili kumteua Salim, kungetafsiriwa vibaya kisiasa
nchini na kimataifa. Kwa mlio
huo wa ngekewa ambao
haukutarajiwa, Mwinyi
akawa mteule pekee wa
Kamati Kuu kugombea Urais. Alitarajiwa kujiengua
kutekeleza ahadi yake, lakini
hakutaka tena; badala yake
akasema: Kama hayo ndiyo
matakwa ya wananchi,
nakubali [uteuzi huu] kwa moyo mkunjufu. Nyerere, akiwa Mwenyekiti
wa Kamati Kuu hiyo,
hakupinga; Liberators
wakashangilia na kucheza
kufurahia ushindi. Lakini
mambo hayakuwa laini kiasi hicho majina yalipopelekwa
kwenye NEC, Agosti, 15, 1985
ambako kambi ya
Frontliners ilipinga vikali
uteuzi wa Kamati Kuu na
kuungwa mkono na msiri na mshauri mkuu wa Nyerere,
Mzee Thabit Kombo. Kombo
hakutaka kuona Mwinyi
akiondoka Visiwani kwa hofu
ya kupotea kwa hali ya amani
na utulivu aliyoijenga katika miezi 18 ya uongozi wake. Sauti za kuzomea kutoka kwa
Wajumbe wa Bara
[waliopandikizwa] zikasikika.
Khatib Hassan wa kundi la
Frontliners, kwa ujasiri
mkubwa, akamuunga mkono Kombo; mjadala mkali
ulioishia bila kupata mshindi,
ukaanza. Nyerere, aliyekuwa
na kauli turufu, akaahirisha
kikao na kuwaita pembeni
kwa mazungumzo washauri wake wakuu, wakiwamo
Mwinyi, Kawawa na Kombo. Kufuatia mazungumzo hayo,
Kombo, katika hali ya
kushangaza, alikubali uteuzi
wa Mwinyi. Na kufuatia hatua
hiyo, Wajumbe walipiga kura
ya Ndiyo au Hapana kwa Mwinyi, ambapo ni kura 14 tu
zilimkataa kati ya Wajumbe
1,746 waliopiga kura. Kambi
ya Frontliners ililipuka tena
kwa nderemo na vifijo kwa
ushindi, safari hii wakidai kufanya Mapinduzi
makubwa kuliko yale ya
1964, wakiimba Salim
amekwisha. Moyo na marafiki
walisherehekea ushindi huo
kwa kucheza hadharani, huku
Mongella akipiga filimbi kuwa
ni yeye aliyependekeza jina la
Mwinyi na Abdul Wakil kwa Urais Visiwani kwenye
Kamati Kuu na hivyo kuokoa
jahazi. Tunapotazama
nyuma kuona kipindi cha
miaka 10 [1985 1995] cha
uongozi wa Rais Mwinyi kwa Jamhuri ya Muungano, na
kipindi cha Rais Idris Abdul
Wakil Nombe Visiwani; tuna
kipi cha kujivunia kwa
Muungano na kwa Zanzibar
kwa jahazi kuokolewa?. Mambo yangefananaje kama
matokeo yangekuwa ni
kinyume chake?.