Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,566
Mhu 3:20 SUV
[20] Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
Kuongelea kifo sio jambo linalopendwa na wengi, sio jambo tunalolipenda, na ukiona mtu anapenda kifo basi ujue mafundisho fulani yamemfanya awe hivyo, au ana shida ya akili.
Kutopenda kifo hakujawahi kuondoa kifo, na kutopenda kufa hakujaondoa kutokufa, tunashuhudia hili likitokea kila mara kwa watu tunaowafahamu na tusiowafahamu.
Tunakumbushwa na neno kuhusu kifo, bila kujali una hadhi kubwa hapa duniani, uwe huna elimu au uwe na elimu kubwa, uwe maskini au uwe tajiri mkubwa, bado kifo kitakufikia tu.
Tulitoka katika mavumbi na tutarudi katika mavumbi, tuna muda mchache sana hapa Dunia, baada ya muda wa kuwepo hapa dunia huwa tunarudi tulipotoka.
Hii inatutaka tuishi vizuri tukiwa hapa duniani, na tumtegemee Mungu sana, tuache tabia ya kutegemea vitu vya dunia hii, tukijua sisi ni wapitaji.
Hatuna maisha ya kudumu hapa duniani, ukubali au ukatae, ujue hapa duniani sio mji wetu wa kudumu, tutakufa siku moja, kama utakufa umejiandaaje na maisha ya umilele.
Tumeshajua mwili unarudi mavumbini, roho itarudi kwa Mungu, inaporudi huko upo usalama au itapokelewa? Hili kwa mwamini anaweza asiwe na ubishi.
Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu, tusiwe sehemu ya watu kujuta kupitia matendo yetu mabaya tunayowafanyia katika maisha yetu hapa duniani.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana