Siku kama leo, Yesu atakua akiwashukia watu walio kifungoni!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Pengine wengi hawaelewi undani wa siku ya Pasaka, zaidi tu ya kujua kuwa siku kama ya leo Yesu Kristo alikufa kwa kusulubiwa msalabani!
Lakini there is a bigger picture watu ambao hawaielewi... Tukio zima la kufa kwa Yesu lilizungukwa na 'vibweka' vya kila aina ambavyo vilizua taharuki kubwa...
Swali kubwa ambalo watu wanajiuliza ni kuwa hizi siku tatu ambazo Yesu 'alipotea ulimwenguni' alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini?
Maandiko Yanesema kuwa Yesu alishuka mpaka kuzimu na kuwakomboa wale waliokuwa KIFUNGONI...
Je kuzimu aliyoshuka Yesu ni ipi? Na ni kina nani hao waliokuwa kifungoni?
Mada yangu itajikita katika kuelezea haya mambo mawili...
Kuzimu aliyoenda Yesu ni mahali pa wafu ambapo walikuwa wakikaa watu waliokufa huku Duniani... Wafu waliotenda mema na mabaya wote walikuwa wakikaa kuzimu, sema tu kati kati yao walikuwa wametenganishwa na shimo kubwa sana lililokuwa likiwazuia watenda dhambi kuwafikia watenda mema and vise versa...
Sasa kazi ya kwanza kubwa baada ya Yesu kushuka mpaka kwenye ufalme wa Shetani, Malango ya kuzimu yalikuwa yakifunguka Yenyewe. Shetani akayakaripia malango hayo kwa nini yanafunguka, na malango yakamjibu kuwa yanawezaje kustahimili juu ya uwepo wa mfalme wa ulimwengu? Shetani akayauliza tena ni nani huyo mfalme wa ulimwengu? Ndipo malango yakamjibu juu ya ujio wa Yesu Kristo...
Sasa sio kwamba kulikuwa na mpambano kati ya Yesu na Shetani kule kuzimu... Yesu alipofika kuzimu kila kitu kiligive way na shetani alikimbia kwenda kujificha.
Yesu Kristo alizitumia siku hizo tatu kuwahamisha kina Ibrahim na watakatifu wote mpaka Paradiso... Hivi sasa kuzimu hakuna tena watakatifu, watakatifu wote walikwisha hamishwa na Yesu ndani ya zile siku tatu alizoshuka kuzimu...
Kuzimu aliyoshuka Yesu isichanganywe na Jehanam ya moto hii ikiwa ni sehemu ambayo watenda mabaya wanasemekana kuwa watapewa adhabu humo. Kuzimu hii ni yale makao makuu ya shetani ambayo kwa jiografia ya kibinadamu yanasemekana kuwepo chini ya Dunia...
Huku ni mahali ambako shetani na malaika zake hukaa... Pia inasemekana kuwa wale wafu ambao wamekufa kwa mazingara na siku zao za kufa katika kitabu cha Mungu hazijatimia, wako huko kuzimu ndio makazi yao ya muda...

Kama una swali na unataka kuelewa zaidi juu ya matukio makuu yaliyotokea katika kipindi cha Pasaka karibu...
 
Once upon a time, there was a virgin who gave birth to biologically fatherless kid.

The Fatherless kid had to die so as to save the people of his father whom is himself as well.

The fatherless kid restored to life three days after his death and forty days later rose to heaven, home of his father who is himself as usual.

The Fatherless kid is expected to come and judge the living and the dead and those whom will found guilty will suffer the eternity fire in the hell created by the most loving being.

......What a ridiculous story from the best selling fiction book in the history of humankind?
 
Back
Top Bottom