G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,290
- 38,948
Ni ukweli usiofichika kwamba CCM haibebwi na wanachama wema (kama wamo), matendo ambayo imefanya nchini wala hazina ya viongozi ambao wameshawahi kuitawala nchi(ukimuondoa marehemu baba wa taifa ambaye kimsingi kabisa hayumo tena)
CCM inabebwa na jina 'CCM' hiki ndicho kilichobaki kuwa hazina pekee ya hiki chama! Kuna baadhi ya wazee na akina mama hujisikia fahari sana kutaja neno 'CCM' bila hata kujua ndani ya hiyo CCM kuna nini!
Nitawapa mfano mmoja........Mwaka 2010 nikiwa kituo kimojawapo cha kupigia kura jimbo la Kawe alikuja mama mmoja wa makamo ambaye hajui kusoma wala kuandika.Alinikuta kituoni nikamuamkia kisha akaniambia na hapa namnukuu "mwanangu naomba uniwekee tiki katika kila mgombea wa CCM kwenye karatasi ya kura akimaanisha kuanzia diwani, mbunge na rais.! Nilimtazama sana yule mama ambaye alionekana dhahiri ni fukara na anayeishi maisha duni mno! Kwa hasira nilimtazama kisha nikafuatiwa na moyo uliojaa huruma na majonzi na nikaamua kufanya maamuzi juu ya kura ya yule mama.! Niliyofanya naomba yabaki kuwa siri yangu kwa sasa.!
Ndiyo maana nasema kuwa siku CCM ikiamua kubadili jina na kujiita jina lingine lenye wanachama na viongozi walewale basi itakufa haraka sana!
"Chagua chama na siyo mtu"-Mkapa