Sikia kauli ya 'Vijana wa CCM Imani' wawajibu Mbatia na Tundu Lissu

Simon Templar

Member
Mar 3, 2016
18
21
Katika kipindi ambacho makundi ndani ya CCM yanaonekana kupwaya, lakini inaonekana kama kuna vita ya chini kwa chini inayoendelea ndani ya chama hicho. Kutokana na figisu za chini kwa chini, hivi sasa wameibuka vijana ambao wanajipambanua kama 'CCM Imani' ambao wanasema wamedhamiria kupambana na wasaliti ndani ya chama pamoja na wale wanaopinga jitihada za serikali ya awamu ya tano.

Vijana hao leo wametoa tamko hili hapa chini:

===============

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

02/07/2016

Ndugu wanahabari, poleni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa.

Wakati Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ikiendelea na utendaji wake, kumejitokeza mambo kadhaa ambayo yamezua mijadala miongoni mwa Watanzania. Tukiwa miongoni mwa Watanzania wenzenu nasi tumeona hatuna budi kujaribu kueleza hayo kwa uchache.
  1. TEUZI ZA MHE RAIS
Kumekuwa na baadhi ya Watanzania VIJANA ambao wanatumia teuzi za Mheshimiwa Rais kupandikiza chuki na ubaguzi wa kikabila, pamoja na kikanda. Ni haki ya Kikatiba ya kila Mtanzania kutoa maoni yake, lakini inaonekana kwamba uhuru huo umevuka mipaka ambapo vijana hawa wakichagizwa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakikosoa kila teuzi zinazofanywa na Rais.

Mfano mzuri ni teuzi za hivi karibuni za wakuu wa mikoa na wilaya ambapo mara tu baada ya kutangazwa kwa wateule, watu hawa wanaopinga kila jema linalofanywa na serikali wakaanza kukosoa na kusema kwamba kuna upendeleo huku wengine wakieleza kwamba kuna ukanda, ukabila na utabaka, jambo ambalo siyo kweli.

Serikali ina utaratibu wake wa kufanya uteuzi, na inaangalia sifa na uzoefu, siyo shinikizo wala upendeleo kama baadhi ya watu wanavyotaka. Kama watu hawa wangekosoa kuhusu uwezo wa wateule ingekuja hoja mujarabu, lakini wao wanapinga hata pale wanapoteuliwa watu wenye sifa na uwezo.

Tukumbuke kwamba, hawa wote walioteuliwa ni Watanzania wenzetu, hawakutoka ng’ambo. Wamesoma na kupata elimu muafaka na wengi wana uzoefu wa kutosha wa uongozi, bila kujali maeneo walikotoka. Rais hawezi kuacha kumteua mtu eti tu kwa sababu anatoka katika kanda yake ama ni wa kabila lake, bali atamteua kulingana na sifa zinazotakiwa. Hatuelewi wanaopinga kama wanataka Watanzania hawa waende wakateuliwe katika nchi jirani au wapi, lakini tumaamini kwa sababu wanazo sifa, basi wanastahili kuteuliwa.

Sisi Vijana wa ‘CCM IMANI’ na Watanzania wazalendo tunasema anachofanya Mhe. Rais Magufuli ni sahihi na hakina chembe ya ubaguzi wala chuki kwa mwananchi yoyote wala upendeleo. Tunawaonya hao wanaoeneza hizo taarifa na propaganda, hususan wale vijana wanaojiita 4uMovement, kuacha kufanya hivyo kwani huo ni uchochezi na wanajikaanga wenyewe kwa mikono na midomo yao na watambue kwamba siku ambayo nchi itaingia katika vurugu hakuna atakayepona kwani wananchi wote tunakutana na adhabu kali kutokana na dhambi ya ubaguzi tunayoifanya.

Pia kuna taarifa za kikundi hicho ambacho wengine bado wamo ndani ya CCM wanajiandaa kufanya vurugu wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wakiungana na wale wa BAVICHA ili kuleta taswira mbaya ya taifa katika mataifa ya nje. Tunawaonya kuachana na mipango hiyo.

2. KAULI YA JAMES MBATIA
Wiki kadhaa tumesikia Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia akitamka kauli ambazo hazina kichwa wala miguu kwamba wanaendelea kukusanya ushahidi wa vitendo vya ubakaji wa demokrasi na haki za binadamu na hatimaye kumfikisha rais mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Tunamshauri James Mbatia aanze na Edward Lowasa pamoja na Freeman Mbowe kwanza kuwapeleka mahakama ya kivita ambao ndio vinara wa kuasi demokrasia kwani hata utaratibu aliotumia Freeman Mbowe kumkabidhi chama Edward Lowasa na kuwa mgombea haukufuata kanuni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wala maridhiano ya UKAWA yam waka 2014.

Sisi Vijana wa CCM IMANI tunamtaka James Mbatia na yeye ajipeleke mahakama ya kivita kwa kutumiwa na Mbowe kuua chama cha NCCR-Mageuzi na kufanya mali yake mwenyewe na familia yake.

Tunamtaka pia James Mbatia afute kauli yake mara moja kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, asipofanya hivyo tutatoa siri zake nje ili wananchi wajue namna mbunge huyo wa Vunjo alivyo na asivyofaa kuwa hata kiongozi wa nyumba kumi.

James Mbatia tunajua namna serikali ya CCM kupitia mwenyekiti wa sasa wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alivyombeba na hatimaye kumpa ubunge wa kuteuliwa ambao ulizaa kuwa mbunge wa kuchaguliwa kwa hiyo tunamtaka afunge mdomo wake kwani tunayo mengi yake na yasiyofaa kufanywa na kiongozi kama yeye.

3. TUNDU LISU
Vijana wa CCM Imani tunaomba mamlaka zinahusika kumwadhibu Tundu Lisu kwa kauli zake za uchochezi na kumdhalilisha rais ambaye amechaguliwa kihalali na wananchi wa Jamhuri ya Watu wa Tanzania kwa kumwita rais ‘dikteta uchwara’ kwani huu ni uhaini kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo ndiyo Sheria Mama.

Ikumbukwe kwamba, ni wapinzani hawa hawa ambao wakati wa awamu ya nne walinukuliwa wakitamani Tanzania ipate Rais atakayesimamia misingi ya utawala bora ambaye wao walisema ‘wanamtaka rais dikteta’. Rais Magufuli si dikteta, bali ameamua kwa dhati kabisa kusimamia utawala bora na kufumua mifumo yote dhalimu ndani ya sekta ya umma ikiwemo rushwa na ufisadi pamoja na matumizi mabaya ya madaraka na ukwepaji kodi, jambo ambalo limejenga Imani ya wananchi kwa serikali yao. Leo hii haiingii akilini kuwaona wale waliotakamani kutawaliwa na ‘dikteta’ kwa sababu mambo ‘yalikuwa hayaendi’ wanathubutu kumwita rais anayesimamia ipasavyo utawala bora ati ‘dikteta uchwara’. Labda pengine waseme kwamba Rais Magufuli anatakiwa kuongeza kasi zaidi ya utendaji wake kuliko hii ya sasa.

Lakini wasichokijua Watanzania ni kwamba, Rais Magufuli siyo dikteta na kamwe hawezi kuwa dikteta kwa sababu hata yeye anachukia udikteta. Rais Magufuli ni mkali. Anapenda kusimamia kwenye misingi ya utawala na hataki visingizio, kwa sababu hivyo ndivyo vilivyofanya wananchi walalamike kutokana na uzembe wa watendaji. Sisi Vijana wa CCM Imani tungependa aendelee kuwa mkali ili kuwanyoosha wazembe, wala rushwa na mafisadi pamoja na wale ambao wanakiuka misingi ya utendaji. Katika kipindi hiki ameonyesha kwamba anaweza kufanya yale yaliyowashinda baadhi ya watangulizi wake na tuna Imani kubwa kwamba katika kipindi cha utawala wake atafanikisha kwa sababu ya ukali wake, kama dalili zilivyoanza kujionyesha sasa.

Lakini pia tunaiomba serikali kumfungulia shauri Tundu Lissu kwa namna alivyomdharirisha kiongozi na mwaasisi wa taifa la Tanzania hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere mwaka juzi wakati wa Bunge la Katiba kwa kumuita dikteta. Hansard za Bunge zipo na zitumike kama ushahidi wa kumfungulia mashtaka mengine.

Tunaziomba mamlaka husika zichukue hatua kali dhidi ya mbunge huyo ili iwe fundisho kwa wabunge, wanasiasa na na wananchi wengine wenye tabia kama hiyo ya kutukana Serikali na waasisi bila staha.

TUNAWASHUKURUNI KWA KUJA, ASANTENI NA KAZI NJEMA.

Imeandaliwa na:
DAVID MANOTI - Mwanasheria
DOTTO NYIRENDA - Mwanadiplomasia
NYAMAGAMBILE CHIKAKA - Mtafiti/Mwandishi
DANIEL MAHELELA – Mtafiti
JUMA CHIKAWE - Mwanasheria na Mtafiti
 
Tamko zuri sana vijana wa CCM Imani aka nitoke vipi. Lakini sasaa mbona hakuna citation yaani hata kutaja kifungu kidogo chichote cha sheria zilizovunjwa au kipande cha katiba kutilia nguvu hoja zenu..alafu kuna wanasheria wawili hapo nadhani..duuh. Haya wasomi wetu wa Chama. Ila ndio mshaingilia kesi ya msingi dhidi ya Tundu Lissu pia m
meshamhukumu na hii itampa faida mtuhumiwa. Bora msingemtaja na kesi yake iko mahakamani...
 
Naona njaa imewatoa shimoni,hakuna lolote hapo
 
Tamko zuri sana vijana wa CCM Imani aka nitoke vipi. Lakini sasaa mbona hakuna citation yaani hata kutaja kifungu kidogo chichote cha sheria zilizovunjwa au kipande cha katiba kutilia nguvu hoja zenu..alafu kuna wanasheria wawili hapo nadhani..duuh. Haya wasomi wetu wa Chama. Ila ndio mshaingilia kesi ya msingi dhidi ya Tundu Lissu pia m
meshamhukumu na hii itampa faida mtuhumiwa. Bora msingemtaja na kesi yake iko mahakamani...
Mkuu hao ndio vijana wa lumumba na tegemeo la ccm
 
Njaaa Kali sana sbr bado hajamaliza kuteua wenyevit wa mashule.
 
Kama lissu hashitakiwi na kuchukuliwa hatua inayostahili kwa kumtukana rais wa jamhuri jpm na baba wa taifa itaeleweka ni kwa kua ni mteja wa hospitali ya Mirembe.
 
Safi sana CCM imani ,

Mmenifurahisha kwa kuwapa ukweli vijana Wa ufipa.

Chadema ni janga kwa taifa
 
Naona ni watafiti na wanasheria! Tutawaangalia kwenye u-DC ujao.
 
Pia kuna taarifa za kikundi hicho ambacho wengine bado wamo ndani ya CCM wanajiandaa kufanya vurugu wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wakiungana na wale wa BAVICHA ili kuleta taswira mbaya ya taifa katika mataifa ya nje. Tunawaonya kuachana na mipango hiyo.

KAMA HABARI HII NI YA KWELI MBONA MNAMTAFUTA NGWAJIMA! ALIKOSEA NINI? Kiwango chetu ni kidogo mno kuweza kuzima haya mambo! Binafsi sijaona kabisa!!! bado kazi mnayo!!!!!
 
Back
Top Bottom