Sijui cha kumshauri Kikwete.

Sijui cha kumshauri Kikwete.

Joined
Jan 5, 2013
Posts
47
Reaction score
9
Leo (kwa bahati) nilikuwa naangalia kipindi cha TBC asubuhi kabla hawajajiunga na matangazo ya mojakwamoja yalihusu uzinduzi wa jengo la Mikutano la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nikakutana na jambo lililonishtua kidogo.Sir George Kahama, waziri wa kwanza Tanzania wa viwanda na biashara, pia balozi wa zamani wa Tanzania nchini China na Zimbabwe alitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo historia ya mahusiano kati nchi yetu na uchina.

Kwa mtazamo wake aliusifia uhusiano wa nchi hizi mbili na kusema unafaa(kitu ambacho hata mimi nakiamini hivyo), akitaja baadhi ya vitu kama reli ya TAZARA achilia mbali misaada ya kijeshi na kiuchumi ambayo Tanzania tuliipokea kutokana na urafiki wetu na taifa la China.

Pamoja na kukosoa serikali zilizofuata (kwa ujanja sana) baada ya awamu ya kwanza kwa kuua na kutekeleza sekta ya viwanda na kuonesha namna serikali hizo zinavyokosea kwa kubadli vipaumbele karibu kila mwaka, muheshimiwa huyu wa zamani alikosa cha kumshauri Kikwete 'bwana maendeleo'. Hiyo ilitokea baada ya kuulizwa kwamba kwasasa anaweza kumshauri nini raisi Kikwete, kabla ya kujibu alitafakari kwa takribani dakika mbili akaja na jibu la SIJUI.

Kwa mtazamo wangu, sir George Kahama ni kiongozi msomi, mzoefu na mwenye nafasi kubwa katika historia ya Tanzania, kwa sifa zake hizo je ni kweli alikosa cha kumshauri 'bwana maendeleo'? au alikuwa na mengi ya kumshauri lakini alihofu kwamba itatafsirika kwamba anamkosoa muheshimiwa, kama ilivyotikea kipindi cha nyuma walivypthubutu akiana Mzee Butiku?
 
Kama washauri wake wanaolipwa kwa kodi zetu wameshindwa kumshauri sidhani kama huyu wa nje na ameshakuwa mstaafu ataweza kumshauri.Pili integemea kama yeye mwenyewe rais wetu ni mpokeaji wa ushauri,kwa maana kuwa je anashaurika?Kama la basi hataakija malaika kutoka mbinguni haitasaidia.Kama ndiyo basi hata mimi na wewe twaweza kumashauri kupitia wabunge wetu.
 
Mzee Kahama kwa kujibu kuwa hajui kitu cha kumshauri ,alikuwa na maana kuwa asingepoteza muda wake kutoa ushauri kwa mtu asiyeshaurika!!! Hii ni ajabu na kweli, uliona wapi kiongozi wa nchi anamuweka mtoto wake katikati ya state picture na kiongozi wa nchi kubwa kama China na yeye Rais wa nchi anajiweka pembeni mwa picha hiyo? Diplomatically hiyo haikubaliki na baba MwanaAsha having been in the foreign service for so long alitakiwa alifahamu hilo!!Jamaa haambiliki wala hashauliki; imekula kwetu.
 
Anaogopa kung'olewa kucha, macho na meno endapo atatoa ushauri ambao hautamfurahisha
 
Ukitoa ushauri wenye maslahi kwa nchi kwa viongozi wetu wa sasa unaonekana mbaya kwao na kana kwamba unawazalau, watakuchukia, watakuundia mizengwa na kukupa majina ya kejeli nk.

Sishangai sana kwa Mh sana Sir George Kahama kusita kufanya/kutoa ushauri wake, maana anajua matokeo yake. Viongozi wa sasa, wao ushauri mzuri kwao ni kuwasifia tu hata kama ni kwa mambo ya ovyo wanayofanya.
 
Sir Kahama alikuwa sahihi kusema kuwa hana cha kumshauri bwana maendeleo kwasasbabu huyu jamaa hashauriki wala haambiliki. Kama unataka kuwa adui wa huyu jamaa basi mshauri mambo mazuri yahusuyo maendeleo ya nchi yetu.
 
mwenye kushauriwa hashauriki bora kukaa kimya, liwalo na liwe
 
kwakweli bora miaka miwili ipite fasta fasta tuachane na huyu jamaa, ningekuwa na uwezo ningefoward (nipeleke mbele) hii miaka iishe haraka.
 
Kama zaid ya 75% ya mambo makuu nchi hii hayaendi sawa, udhan hata wewe ungeulizwa una ushaur gan ungejibu nin..!?

Mzee yupo sawa mana ni ngumu sana kutoa ushaur wa mafungu katika mambo yasiyoenda sawa kwenye mfumo kama hama huu wa Jk.
 
Labda alitaka amshauri aachie ngazi, ambao ungekuwa ushauri bora kabisa, lakini akasita labda angedhani anamuonea wivu, kama hali hii itaendelea dnani ya miaka 100 ijayo Taifa la Tanzania litakuwa limepotea, au limemengwa sana. take it from me, tukianza na loliondo, Kigamboni, bagamoya. taratibu tukija kushtuka hatuna chetu
 
Back
Top Bottom