Sijawahi kushusha uzi mapema kiasi hiki, wakuu nahisi yamenikuta makubwa

Chief Kumbyambya

JF-Expert Member
Jun 16, 2022
490
1,462
Natumai mumeamka salama wakuu!

Wazee juzi Jumapili nipo kwenye pub moja hivi napiga bia na nyama choma kiasi kwaajili ya kumalizia wikiendi yangu vizuri sikutaka kutoka na mwanamke siku hiyo ili niamke Jumatatu nikiwa sina uchovu kabisa. Ilipofika mida kama ya saa tano na nusu usiku hivi si unajua zile pilika pilika za bar wanywaji watanielewa, mara huyu kapita kaenda huku, mara yule kabambia huyu, mimi nawachora tu huku kinywaji kikiwa kimeshaanza kunichota vyema.

Ghafla akapita binti mmoja miaka kama 20 hivi siyo zaidi ya hapo, kimo cha wastani, mweusi wa kawaida, ana umbo la kati zuri kweli, mavazi yake hayafanani na wahudumu yaani kavaa kiheshima. Alivaa gauni la kijani toka juu mpaka maeneo ya ugoko lakini pamoja na kujaribu kujistiri kashepu kake kazuri kalionekana vyema. Alipita mbele yangu akiwa anaelekea nje nikasubiri kafungua tu mlango na mimi nikamfuata huko huko nje.

Alikuwa kama anaondoka nikamuita akageuka na kusimama, nikamsalimia vizuri sana kwa kujiamini vizuri ya kilevi, nikamchana kuwa nimemuelewa na nimemfata yeye hadi huku nje na kama amepanga kuondoka ahairishe anipe kampani kisha tutoke wote. Binti akasema anajisikia usingizi anajisikia kulala hivyo kama nitamuhitaji nichukue namba yake ili nimtafute kesho yaani juzi Jumatatu.

Nikachukua namba yake nikajaribu kuipiga pale pale ili kuthibitisha kama ni ya kweli ama la, nilipopiga ikaita nikamwambia bibie hiyo ndiyo namba yangu na kesho nitakucheki. Jumatatu ya juzi nikamcheki lakini binti hakuwa hewani kabisa kutwa nzima.

Jana Jumanne nikamcheki mtoto akapatikana, nikampanga ila akasema yuko mbali. Nikamuuliza mbali wapi bibie maana tulionana kwenye pub moja tukuyu mbeya. Akaniambia yeye anaishi Kyela kama nitamuhitaji nimtumie nauli ili aje na nikafanya hivyo, nilimtumia 5000 maana nauli toka Kyela hadi Tukuyu ni 3000.

Nilimtumia pesa mida ya saa saba jana na kumuuliza ehe bibie nauli hiyo hapo unakuja saa ngapi? Akasema nakuja jioni ili nilale au hautaki? Nikamwambia hiyo itakuwa safi sana bibie ili nitulie na wewe usiku wa leo, akasema poa basi muda huu nalala nikiamka jioni najiandaa nakuja.

Nikasema sawa mamaa ila baada ya saa kama moja hivi akili ikakaa sawa na ikaniambia "Aisee kaka, tayari umepigwa, huyo haji wala nini hiyo pesa umempa atanunulia bando aingie zake Tik Tok huko kutingisha matako."

Nikajipa moyo potelea pote asipokuja ni kama nimetoa sadaka tu. Kwani tumepoteza vingapi mpaka nihofie hako ka 5,000 tu ambako naweza kukakata kwa kifungua kinywa moja tu. Na akili ikaniaminisha kuwa huyo haji we endelea na ratiba zako tu hivyo nikasahau kabisa kuwa leo nilipanga kupata mgeni. Kwenye mida ga saa kumi na moja jioni nikazima simu nakuiweka chaji kisha nikalala.

Inafika mida ya saa moja jioni nikaamka nawasha simu baada tu ya dakika mbili nakuta namba ya binti inanipigia akilaumu amefika stendi toka saa kumi na mbili ananipigia mimi sipatikani, ndiyo nakuja kupatikana saa hizi. Kama sikuwa na mpango wa yeye kuja bora nisingemtumia nauli na kumuita na hajui atafanyaje kama nikimtelekeza maana hata nauli ya kurudia Kyela hana.

Nikasema "Shit" ni nini hiki nimefanya? Nikamwambia mamaa nakuja nipe dakika mbili tu maana nilizima sima nikaiweka chaji ndiyo maana sikupatikana wakati unafika, na pia nilijua wewe ndiyo wale wale tu wala nauli hivyo nikaondoa kabisa imani ya kwamba kweli utakuja.

Nikafika kweli namkuta mtoto amependeza vibaya mno, mavazi yake yale yale ya heshima, sasa kwa mazingira niliyomkuta siku ya kwanza nikajua huyu atakuwa mnywaji tu kama mimi. Nikamuuliza twende sehemu tukapige bia kisha twende zetu geto binti akasema yeye bia hatumii kabisa, nikasema nini?

Sasa siku ile ulikuwa unafanya nini pale mida ile mibovu? Akasema alikuwa na kaka yake wametoka Mbeya na gari ya kaka yake kufanya manunuzi flani na wakati wanarudi ndiyo kaka yake akasema wapite pub tukuyu, kaka yake apige bia na yeye alikuwa anakunywa tu juice.

Na ule muda aliponiambia anaenda kulala, alikuwa anaenda kwenye gari ya kaka yake kumsubiri ili akimaliza bia waondoke kuelekea Kyela. Nikasema poa basi twende mimi napiga bia wewe nitakununulia juice zako sawa? Akasema sawa.

Tukaingia Laxmi pub iko Tukuyu mjini hapa. Mtoto nikamchukulia kitimoto nusu na ndizi, mimi nikapiga supu nzito ya kuku. Baada ya kumaliza kula mtoto akadai nimchukulie Apple Punch tatu za baridi, mimi nikaagiza Safari zangu tano kubwa huku tukiendelea kufahamiana zaidi na binti.

Katika stori akaniambia kuwa ana miaka 19, dooh hafanani kabisa na umbo lake! Maana ana umbo zuri la mwanamke aliyepevuka ila ukimcheki chuchu ni saa sita na pia ukimcheki usoni ana kasura kakibinti binti kalikomaliza form four kama mwaka 2019 hivi, nikasema kama kadanganya umri atajua yeye, siyo biashara yangu.

Baada ya kumaliza vinywaji tukachukua boda hadi geto. Mtoto nilimchakata vilivyo na ni mtamu haswa, yaani haswa. Saa kumi na mbili asubuhi nikamtoa nakumsindikiza stendi akapanda gari na kurudi Kyela mimi nikarudi geto kumalizia usingizi. Sasa kimbembe kimeanza wakati nimelala ule usingizi wa asubuhi na ndicho kilichonifanya nilete huu uzi.

Nikiwa katika usingizi mzito wa asubuhi kutokana na shughuli ya usiku nikaota ndoto. Kwenye ndoto nikaona sura zote za mademu niliowahi kuwapitia ambao wengi sana walikuwa ni wahudumu wa bar na wachache sana wa uraiani.

Yaani wengine mpaka niliwasahau maana niliwagonga miaka mingi sana imepita, ila kwenye hii ndoto niliwaona wote na kuwatambua kuwa huyu nilikutana naye bar fulani, na huyu nilikutana naye bar fulani, na huyu bar flani, bar za Mbeya pamoja na za mikoani nilikowahi kuishi.

Baada ya sura za hao wanawake wote kupita nikaanza kukabwa nakosa hadi pumzi, kugeuka nashindwa na wala kupiga kelele siwezi. Na katika kukabwa huko sura ya mtu anayenikaba namuona ni yule binti niliyetoka kulala naye usiku wa kuamkia leo, yaani huyu niliyetoka kumsindikiza asubuhi.

Binti ananikaba huku akiwa amevaa chupi ambayo ndiyo aliyoivaa wakati anatoka geto kwangu, ghafla nikashtuka huku jasho jingi likinitoka na kuhema kwa nguvu sana kama mtu aliyetoka kukibizwa. Nikashangaa ni nini hiki?

Wakati nikiendelea kushangaa na kutafakari juu ya yule binti, najiuliza mbona wakati tuko wote hakuonesha viashiria vyovyote vinavyohusiana na mambo ya kishirikina, yaani hata dalili za kufanya mtu ukahisi kwamba huyu sio wa kawaida?

Ninachokumbuka tu ni wakati tuko bar pale mara nyingi alikuwa ananiangalia sana usoni, yaani kama mtu anayetaka kunikariri na nilivyoona anaiangalia sana nikataka kumhamisha mawazo nikamwambia, unajua nilifikiri utanidanganya na hautokuja, binti akatabasamu na kusema, hapana siwezi kumdanganya mtu ninayempenda hata siku moja. Hayo ndiyo ninayo yakumbuka. Labda kwa wataalam watanisaidia kama hapo kuna kiashiria chochote.

Baada ya kutafakari hayo ya kwenye ndoto ya kwanza ghafla ukanichukua tena usingizi mzito sana, na ile ndoto ikajirudia tena. Safari hii nilimuona yeye mwenyewe na chupi ileile aliyoivaa wakati anaondoka geto, alinibana mikono nisiweze kufurukuta, miguu ikakosa nguvu kabisa, napiga kelele majirani wasikie lakini sauti hata haitoki. Safari hii alinikaba haswa nikiwa namuona kabisa nikashtuka tena huku nikivuja jasho jingi sana. Nikasema ama kwa hakika leo nimeyakanyaga.

Wazee kwa wajuzi wa haya mambo naomba mnisaidie, sijawahi kuleta uzi mapema kiasi hiki ila imenibidi nilete ili niweze kupata msaada wa haraka kwa wenye uelewa wa haya mambo waniambie nimefanywa nini na ili kujinasua nifanye nini kabla usiku wa leo haujaingia.

Kama asubuhi tu tena kukiwa kumeshaanza kukucha imekuwa hivi, je, ikifika usiku itakuwaje wazee?

Hapa natamani kulia kwa majuto kumuomba Mungu anisamehe dhambi zangu nilizowahi kuzifanya ila machozi hayatoki hata kidogo. Najaribu kuyakamua lakini wapi. Usiku wa leo naona kabisa utakuwa mrefu sana kwangu, morali ya kwenda kazini yote imekata nawaza tu juu ya hili tukio la leo.

Nimepanga nikanunue biblia leo nilale nayo akija aikute akimbie, au nikiona vipi nitaenda tu kulala kanisani maana hapa geto pashakuwa pachungu.

Wazee nahitaji sana msaada kwa wajuzi wa haya mambo, mwenzenu nimeyakanyaga.

Narudia tena NIMEYAKANYAGA.
 
Acha mawazo mgando, huyo Binti Hana shida yoyote, mpigie msalimie muulize safari ilikuaje Kisha mtoe chochote Cha kula mchana. Baada ya hapo mwambie aje Tena uichakate na mkiwa wawili msimulie ndoto Yako Kisha soma reaction yake au body language yake utajua TU Kama anahusika au la!

Ulishindwa hiyo, basi unapolala hakikisha umejipigia ndimu ya unga kakipakiti kamoja Kwenye maji nusu glass na ulale.
 
Mkuu pole sana! Umejaribu kumpigia simu tena huyo binti na kuongea nae chochote hata salamu?
Kama bado jaribu kumpigia katika maongezi yake labda unaweza kufahamu kua kuna lolote anajua kuhusu mambo yanayokutokea.
Asante mkuu, wakati tunaagana nilimwambia akifika anitext, akinitext kuwa kafika nitamueleza juu ya yaliyonitokea
 
Acha mawazo mgando, huyo Binti Hana shida yoyote, mpigie msalimie muulize safari ilikuaje Kisha mtoe chochote Cha kula mchana. Baada ya hapo mwambie aje Tena uichakate na mkiwa wawili msimulie ndoto Yako Kisha soma reaction yake au body language yake utajua TU Kama anahusika au la!

Ulishindwa hiyo, basi unapolala hakikisha umejipigia ndimu ya unga kakipakiti kamoja Kwenye maji nusu glass na ulale.
Sijamwacha hivi hivi mkuu, nimempatia pesa kiasi kama shukrani kwa huduma nzuri aliyonipatia na alishukuru kwa futaha sana ila daah ndiyo mauza uza haya yananitokea sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom