Sifa mpya za nyumba Bora

josam

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
2,241
1,031
Ndg wasomaji,

Kuna tabia ya Watanzania kuona kwamba kila mmoja kujenga na kumiliki nyumba ni ufahari! Binafisi siamini hivyo, na ndiyo maana makazi yetu ni full kizungumkuti, afya zetu zinazungukwa na mazingira hatarishi ya hali ya hewa kisa kila mmoja kutafuta kuishi kwake!

Binafsi najua ujenzi si kazi rahisi, lakini kadri watu wanavyotafuta makazi yao ni kama ujenzi ni rahisi sana. Ila bado watu wengi wanatakiwa waelewe kuwa kati ya sifa za nyumba bora, si tu nyumba kuwa na choo, jiko na bafu pekee! Sifa za nyumba bora ni zaidi ya hapo, lazima nyumba bora iwe na yafutayo japo kwa uchache;

1. Ijengwe katika kiwanja kilichopimwa.

2. Ijengwe mahali ambapo huduma muhimu zipo ama zimepangwa kufanyika mfano barabara, maji, umeme, shule, hospitali, n.k.

3. Mazingira mazuri yanayozunguka nyumba, hii ni pamoja na hali nzuri ya hewa na mzunguko safi wa hewa. Lazima nyumba ya makazi iwe mbali na viwanda, kumbi za starehe (music, sinema, vilabu), masoko, n.k.

4. Ijengwe sehemu zenye mfumo wa maji taka, uratibu mzuri wa utupaji na ukusanyaji taka etc.


Hakika Wizara ya Ardhi /Makazi, mipango miji, NEMC!

Mfano kupanga jiji la Dar es Salaam kuwa la kisasa au maboresho, kunahitajika kufanyika yafuatayo:

1. Serikali kuhamisha makao makuu ya nchi na shughuli zake zisizo husika na Bandari. Nasikia Serikali imeimarisha TEHAMA katika tasisi zake hii maana yake ni kuwa hata Afisa akiwa Dodoma atafanya kazi sawa na yupo DSM. Magufuli kwa nini usihamie Idodomia?? Hii itasaidia kupunguza msongamano wa watu katika jiji la DSM.

2. Kuhamisha majengo yenye huduma muhimu za Serikali kuzipeleka nje ya jiji mfano kutenga eneo kwa ajili ya mji mpya Kibaha. Watu watahama wenyewe kufuata huduma hizo

3. Mpango mwingine ambao ni mgumu kuutekeleza ni wa kuhamisha Wananchi kutoka maeneo ya jiji na kupelekwa sehemu iliyotengwa maalum kwa makazi. Hapa Taifa linatakiwa kujipanga na fidia na maandalizi ya makazi mapya!

Karibu kwa mjadala!
 
maelezo haya hayajakidhi nyumba bora bali unaitaftia dodoma sababu ya kupelekwa adminstrative setup kule
 
kwamba Dodoma ndio kuna makazi bora zaidi kuliko dsm....?
Sijawahi kukaa Dom lakini kwa kupita tu naona mji ule una mipango endelevu ya makazi.... suruba za maji pengine ni changamoto
 
Jerhy, tutajie sifa za nyumba bora ili utusaidie mawazo zaidi katika jukwaa hili
 
mkuu yaan tuna fikra sawa mpaka najishangaa. mawazo yako yamegongana na yangu 100%.
 
Back
Top Bottom