S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Uwe Mama wa Familia ukikosa hekima na busara familia utaisambaratisha. Uwe Baba mwenye nyumba ukikosa hekima na busara familia inasambaratika. Kiongozi yoyote yule anatakiwa awaongoze wenzake kwa hekima kubwa na busara ya juu kabisa.
Kiongozi yoyote yule akikosa Hekima na Busara kuna uwezekano mkubwa kuwaona nyie hamna akili na yeye ndo ana akili kuzidi wote. Na mambo haya mawili yaani Hekima na Busara akiyakosa kuna uwezekano mkubwa wa kukiuka utaratibu mliojiwekea hata na kuona walioweka ni Majuha. Sifa ya mtu ambaye hana busara haogopi kuzalilika na kuwazalilisha wenzake popote pale.
Na bahati mbaya zaidi kwa nchi zetu hizi za Afrika, tumepata na tunaendelea kuwapata viongozi wengi sana wenye tabia hizi. Bahati mbaya sana viongozi hawa hupata wafuasi wengi zaidi hasa wanaofaidika na mfumo wa kukosa hekima na busara. Tunawashangilia mno kwa sababu nasi tunataka kuingia kwenye mfumo rasmi. Na viongozi wengi ambao hawana hekima na busara hupenda watu wenye kuwasifu kila mara, hawapendi kushauriwa na ukimshauri na ikitokea jambo hilo halijamfurahisha tegemea kuondolewa haraka kwenye nafasi hiyo. Lakini viongozi wasio na busara hupata wafuasi wengi sana, na wale ambao wanajua kuwa wanaongozwa na mtu asiye na busara hukaa kimya, wengine hupinga kwa nguvu zote. Kuna wale ambao hujitolea kabisa na wako tayari kwa chochote kile.
Usiombe kwenye Taasisi unayofanyia kazi upate kiongozi asiye na hekima na busara utatamani kuacha kazi maana anaweza kukuzalilisha kwa kosa dogo sana ambalo linahitaji kuambiwa tu kuwa ungefanya hivi. Kwa mfano, wewe ni Mwalimu, Mkuu wa shule yako hana hekima na busara, hakika utaiona kazi chungu. Hashindwi kukufuata darasani mbele ya wanafunzi na kukuzalilisha. Viongozi hawa hupenda kusifiwa sana, na bahati mbaya wafuasi wao nao huiga vitabia hivyo, wako tayari kukuzalilisha kumtetea Mkuu wao ambaye hana hekima na busara.
Kwa mfano, dalili ya kiongozi ambaye hana hekima na busara ni hii hapa; wewe ni Mwalimu unafundisha darasa fulani ikatokea mwanafunzi mmoja akakuuzi, badala ya kumshughulikia mwanafunzi huyo ugonvi unauhamishia darasa zima, hii ni dalili ya kukosa hekima na busara.
Afrika tumekumbwa na tatizo hili kubwa la kuwa na viongozi ambao hawana hekima na busara. Ukifuatilia vita vinavyoendelea Afrika, ukiacha kuingiliwa na mataifa ya nje, kwa sehemu kubwa sana husababishwa na viongozi kukosa hekima na busara.
Pamoja na kutuhumiwa kuwa hana hekima na busara, Donald Trump, Rais mteule wa Taifa kubwa la Marekani katika kitabu chake cha "NEVER GIVE UP" alichokiandika na mwaka 2008 alisisitiza kuwa sifa kuu ya kiongozi ni Vision and Discipline. Kama kiongozi hana maono na busara hafai, anasisitiza Donald Trump katika kitabu chake.
Julius Nyerere naye alisisitiza mno viongozi kuwa na hekima na busara katika maamuzi yao. Na alienda mbali kwa kusema kuwa kwa katiba hii 1977, akiamua inampa mamlaka makubwa hata ya kuwa Dikteta. Lakini alitumia hekima zaidi na busara kuamua mambo mengi ya nchi. Ndiyo maana alifanikiwa kutuunganisha vyema Watanzania mpaka leo, unaweza kuishi sehemu yoyote ile bila ubaguzi.
Yanayoendelea Gambia chanzo kikubwa ni kuwa na watu wasio na hekima na busara, yanayoendelea Burundi ni ukosefu wa hekima na busara, yanayoendelea Sudan ni kukosa hekima na busara. Kwa mfano, mmekubariana kuwa nchi itakuwa na mfumo wa vyama vingi na katiba inasema hivyo, na wewe kiongozi umeapa kuilinda Katiba ya nchi hiyo. Sasa kwa nini usikubariane na demokrasia hiyo ambayo ulikubariana kuilinda???.
Na mtu ambaye hana hekima na busara kama nilivyosema hapo juu, hujiona kuwa ni yeye tu ndiyo ana akili kubwa kuliko wengine wote. Yeye huzani anajua kila kitu. Huzani kuwa anajua maswala ya uchumi, kijamii, siasa na mazingira pia. Ni hatari sana Taifa lolote likiwa na kiongozi wa namna hii. Wakati wowote hujikuta limetumbukia kwenye machafuko, na ikifika hapo, ndipo hata mliokuwa mnashangilia mtaelewa kwa nini kukosa hekima na busara ni hatari kwa ustawi wa nchi.
Sikukuu njema ya Mapinduzi.
12/01/2017