Sierra Leone inatarajiwa kuwa nchi ya 23 katika bara la Afrika kufuta adhabu ya kifo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Wabunge katika taifa hilo la Afrika Magharibi walipiga kura kwa kauli moja siku ya Ijumaa kupiga marufuku adhabu ya kifo na kuibadilisha na kifungo cha maisha au kifungo cha chini cha miaka 30 kwa uhalifu kama mauaji au uhaini na kuwapa majaji nafasi ya kutumia busara zaidi wakati wa kutoa hukumu.

Sierra Leone haijaua mtu yeyote tangu 1998, wakati wanajeshi 24 waliuawa na kikosi cha risasi kwa kushiriki jaribio la mapinduzi mwaka uliotangulia.

Wakati huo nchi hiyo ilikuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomwaga damu tangu 1991 hadi 2002. Lakini zaidi ya watu 80 wamehukumiwa kunyongwa tangu wakati huo.Rais Julius Maada Bio anatarajiwa kutia saini muswaada huo kuwa sheria.

Nchi zaidi za Afrika zimefutilia mbali adhabu ya kifo, ambayo vikundi vya haki za binadamu vinachukulia kama mabaki kikatili ya karne za utawala wa kikoloni. Mahakama kuu ya Malawi iliamua kitendo hicho kuwa kinyume cha katiba mnamo Aprili, wakati Chad ilipiga marufuku mnamo 2020.

Voa Swahili
 
Mimi binafsi naunga mkono adhabu ya kifo.
Lengo hasa la adhabu ni kumbadilisha mtu ili aache matendo/tabia mbaya.

Kifo hakiwezi kumsaidia mhusika kubadilika kitabia/matendo hivyo kuiita ni adhabu naona kama Kuna mapungufu kidogo.
 
Adhabu ya kifo inatakiwa iendelee kuwepo,,,,kwa mfano hawa wanaoua Albion wafanyweje,,,inatakiwa wauwawe ili iwe fundisho kwa wengine
 
Lengo hasa la adhabu ni kumbadilisha mtu ili aache matendo/tabia mbaya.

Kifo hakiwezi kumsaidia mhusika kubadilika kitabia/matendo hivyo kuiita ni adhabu naona kama Kuna mapungufu kidogo.
Yeye akijifunza akabadilika ama akabadili tabia mbaya inasaidia nini wale aliowaua? Yaani yeye kubadilika inawasaidia nini wale aliowaua?

Mfano, mtu anaweza kuamua kuvamia nyumba akabaka wanawake wote, mama na watoto kisha akawaua wote na kuteketeza uzao wa hiyo familia. Mtu kama huyo tumpe muda wa kujifunza na kubadilika itasaidia nini wale aliowaua?

Ni ujinga mkubwa kuingiza jamii kwenye gharama za kumtunza mtu kama huyo wakati yeye hakujali maisha ya binadamu wengine, mtu ambae hajali thamani ya maisha ya watu wengine, hakuna haja ya kujali kuhusu maisha yake.

Jamii ina mahitaji mengi ya msingi na muhimu, kuna watu wengi wana matatizo wanahitaji msaada, hizo gharama za kutunza wauaji magereza zielekezwe kwenye shughuli za msingi za kuboresha maisha ya watu na sio kutunza watu wapumbavu kama hao.
 
Kwani ukiwaua hao wauaji inawasaidia nini wale waliouawa?
 
Back
Top Bottom