Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 255
"Ili tuendelee tunahitaji mambo makakuu manne, Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi Bora" Mwl. J.K. Nyerere.
Kutokana na hayo mambo manne, nitaongelea hilo la siasa safi! Hayo mengine ntayaongelea katika andiko langu lingine hasa hilo la raslimali Watu ambalo ndo kada yangu ya kitaaluma.
Watanzania waliowengi hawajui maana ya siasa. Kwao:
1. siasa ni mchezo mchafu
. au
2.siasa ni kutengeneza
genge la walaji, mafisadi...
au
3. siasa ni uwongo.
Ukweli ndivyo tulivyozoea. Kudanganywa, kuibiwa, kuchezewa, kumasikinishwa, kuzugwa, kudunishwa, kulogwa,...
Kwa nmna yoyote ile, ni vyema ijulikane kuwa siasa ni MAISHA. Siasa ni namba moja ya kila kiti. Siasa ni kufa, kupona, dini, chakula, sukari, nyumba, nguo za mtumba, Watu..... Siasa ni maendeleo, elimu, chakula.... Kila kitu..... Siasa ni barabara bora, uchumi wa nchi,.....
Siasa si kitu cha kawaida. Ni kazi. Kazi kubwa inayobeba kazi nyingine zote nchini na duniani. Siasa ndio huamua kima cha Chini, mishahara, makato, KODI... Siasa huamua nani aajiriwe, nani astaafu, nani atumbuliwe, nani awe speaker, nani awe naibu, Mkuu wa mkoa, waziri, siasa husimamisha ajira, hupanga ajira, husitisha kabisa ajira....
Siasa safi ni IPI? Ile ya kidemokrasia, inayosikiliza matakwa ya wananchi na kujali maoni ya waliowengi bila kutupilia mbali yale ya wachache.
Katika nchi yetu siasa imejikita na kumpa nguvu MTU mmoja, Rais. Anateua mawaziri, majaji, makatibu wakuu, wakuu wa mashirika, ....
Rais wetu Mpya Dk. J.P.Magufuli yeye ndiye rubani wa siasa yetu. Mwl. J.K. Nyerere aliwahi kusema hivi, kwa jinsi katiba yetu ilivyo , naweza muda wowote kuwa dictator! So katiba inamweka J.P.M karibu na Mungu kwa nguvu alizonazo. Akizitumia zote basi balaaa.
Ni zao la minyukano ya muda mrefu ndani ya CCM na nje ya CCM pia. Ni minyukano hii sasa imemleta rais imara katika chama duni kabisaa. Kilichojaa wanachama wenye kuhodhi uchumi wa nchi kinyume cha sharia, ufisadi, wizi, utapeli na Kilango aina ya Ubaya.
Minyukano kati ya Membe na Lowassa katikati akiwemoJK na familia yake, tukapata rais bomba. Ni zao la minyukano, ni SIASA ya muda mrefu. Ni baada ya kupima upepo wa timu Membe na Lowasaa wakaona sasa hamna jinsi, wakaamua kupata mtu neutral. Ni siasa za muda mrefu, magazetini, mitandao ya kijamii, kila kona.... Makongamano, mikutano, OPERATIONS za vyama vya upinzani, OPERATION SANGARA ilifanya kazi kwa kuiteka kanda ya Ziwa na namna pekee ilikuwa kumpata mgombea toka Kanda hiyo ambaye ni JPM.
Siasa ikisimama mpaka 2020, JPM atakwama, atadanganywa, hakutakuwa na misigano, ushindani utaisha, maendeleo yatafifia... Uoga utatamalaki... itakuwa hataree. Zaidi na zaidi police watatawala nchi kuliko mamlaka halali!
Watawala wanajua. Wako nondo. Watawaliwa waliowengi, Africa hasa kisini mwa jangwa la Sahara, ndio hao IQ below 75 kwa maana wana metal retardations kwa zaidi 90% ya wananchi wote.
So, siasa upinzani sio uadui, ni nia njema. Ni mboni ya rais. Ni kioo cha Takukuru, ni mwangaza wa mahakama, ni sehemu ya waoga kupeleka kero zao. Ni sehemu ya wabunge kukusanya kero za wananchi! .... Ukizuia makongamano na mikutano maana yake mbunge atembee nyumba kwa nyumba kusikiliza Watu wake. Ni hataree sana. Kudhibiti wabunge wa upinzani Bungeni. Inaleta chukia na dharau kwa serikali tawala.
Siasa ni kila kitu, siasa ni dawa hospitalini..... Siasa ni maisha ni kazi, ni uhai, ni mapigo ya moyo......