Siasa za upinzani Tanzania

huko kwenu vipi

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
1,519
1,462
Habari wanajamvi.....

Maana halisi ya neno "upinzani"ni kuisimamia na kuikosoa serikali iliyopo madarakani....

Lakini sambamba na hilo upinzani kama upinzani lazima waje na mpango mbadala wa namna ya kuisimamia na kuikosoa serikali kwa kutoa mpango mbadala wa namna ya kuiongoza nchi endapo serikali iliyopo madarakani haitimizi wajibu wake vizuri....

Upinzani wa kweli ni ule unaojisimamia,upinzani usiotetereka kwa namna yeyote ile,upinzan unaotumia mbinu nyingi za kisiasa,kuwa wabunifu ili wananchi wawaamini na hatimaye kuwachagua kuwa viongozi wao....

Upinzani unatakiwa uimarishwe toka ngazi ya chini kabisa kuanzia ngazi ya mitaa,kijiji,kata,tarafa,wilaya,mikoa na hatimaye Taifa kwa ujumlaaaa kwa kuwa na viongozi wanaojituma na kuwaelimisha jamii toka ngazi ya chini kabisa,viongozi ambao ni wabunifu.....

Upinzani ili ujiimarishe vizuri lazima kuwe na ofisi ya chama kuanzia mitaa,kijiji,Kara,tarafa,wilaya,mikoa na hatimye Taifa amabazo wanatakiwa wazijenge wenyewe kwa nguvu zao wenywe na kuwa na miradi nyingi kwa ajili ya kujiingizia pesa ili chama ikue kiuchumi bila hata kutegemea ruzuku,huo ndo utakuwa upinzani wa kweli na wananchi watawaamini zaidi kwa sababu maendeleo ya chama wanaiona wenywe na hata siku wakiwachagua wataongoza nchi vizuri...

Lakini upinzani wa Tanzania maneno kibao,kuwa mpinzani unatakiwa ujitoe kwa wananchi wako hata ikiwezekana utumie pesa yako kama ufadhili ili kutimiza miradi ya maendeleo...


Upinzani kaeni chini upya,mjitathmini upya na kujitafakari upyaaa ikiwezekana kuchukua ushauri huu wa kujenga ofisi za chama kila sehemu kwa nguvu zao,

Karibuni tujadili.....

Mods msiitoe hii thread....
 
Ungelikuwa ndio wewe umepanga kihalali na landlord wako miaka zaidi ya 35 lakini ghafla wanakutupia vyombo nje eti hujalipa kodi na jengo linavunjwa kwa muda wa wiki moja tu, kuuliza kulikoni unagundua ni kukiongoza chama pinzani basi ungeelewa upinzani unapitia hali gani katika historia yake!
 
Ungelikuwa ndio wewe umepanga kihalali na landlord wako miaka zaidi ya 35 lakini ghafla wanakutupia vyombo nje eti hujalipa kodi na jengo linavunjwa kwa muda wa wiki moja tu, kuuliza kulikoni unagundua ni kukiongoza chama pinzani basi ungeelewa upinzani unapitia hali gani katika historia yake!

Ndo maana nimesema wajenge ofisi zao
 
Back
Top Bottom