MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mienendo ya kisiasa inayochagizwa na chaguzi mbali mbali za kisiasa ni mchezo katika mahusiano kati ya wanasiasa na wapiga kura. Mienendo hii ya kisiasa hutegemea sana mahusiano kati ya wanasiasa na wapiga kura.
Katika nchi kama Tanzania ambazo siasa hazijadili masuala bali matukio na watu, inakuwa ni kawaida kuhama kwa haraka kutoka tukio moja kwenda jingine au kutoka kumjadili mtu mmoja mpaka mwingine huku yale ya nyuma yakisahaulika kwa haraka sana.
Katika nchi ambazo ni masikini wa elimu, viongozi wa kisiasa ndiyo huweka agenda za kisiasa katika jamii huku wananchi wakibaki kama wasikilizaji au waimba mapambio ya kisiasa kinyume na nchi ambazo ni matajiri wa elimu ambapo wananchi ndiyo huweka agenda za kisiasa huku kazi ya kujibu ajenda hizo kivitendo huwa niya wanasiasa.
Kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015, wanasiasa wetu walituambia tatizo kubwa la nchi yetu ni ufisadi. Wengine walienda mbali zaidi na kudai kwa sasa ufisadi umekuwa kama kansa huku wengine wakisema kama hautapata tiba mapema kuna uwezekano taifa letu likasambaratika.
Kama lilivyotakwa la Katiba ya Tanzania, Vyama vikatuletea wagombea ambao viliamini watapambana na ufisadi pindi wakishinda. Wananchi wakachagua kwa kura nyingi zaidi mgombea ambaye walidhani au kuamini atapambana na ufisadi. Kwa sababu siasa zetu hazijadili masuala, wengi hawakujiuliza au kufahamu ni njia gani wagombea watatumia katika kupambana na ufisadi pindi wakishinda.
Kwa sasa tumeanza tena kuaminishwa na wanasiasa kwa nguvu kuwa tatizo la Tanzania siyo ufisadi bali ni udikteta huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai wako tayari kufa katika mapambano ya kuondoa udikteta.
Tunaambiwa Rais Magufuli ameleta udikteta nchini na kwa sasa anaingilia kazi za mihimili mingine ya nchi (Mahakama na Bunge).
Kwa sababu siasa za Tanzania hazijadili masuala bali hujadili matukio na watu, kwa sasa baadhi ya watu hawaulizi au kujiuliza kwa namna gani anaingilia utendaji wa bunge wakati bunge lina uwezo wa kumfuza kazi Rais Magufuli kupitia Ibara ya 46A(1-2) ya Katiba ya Tanzania, kwa maana nyingine, Rais Magufuli hawezi kuingilia kazi za bunge bila ridhaa ya wabunge.
Kwa sababu siasa za Tanzania hazijadili masuala bali hujadili matukio na watu, hakuna anayeuliza huu ufisadi ulitoka wapi wakati kuna bunge lisiloingiliwa ambalo kazi yake ni kuisimamia serikali. Hili bunge huru lilishindwa vipi kuisimamia au kuiwajibisha serikali wakati limepewa madaraka kikatiba. Huwezi kusema serikali haikufanya kazi zake wakati wewe kama bunge ndiye unatakiwa kuisimamia serikali.
Kwa sababu siasa za Tanzania hazijadili masuala bali hujadili matukio na watu, kwa sasa tumejikita katika mijadala ya kujadili matukio na watu badala ya masuala yanayobainishwa ndani ya taratibu, kanuni na sheria mbali mbali kuhusu madaraka ya bunge na serikali.
Kwa sababu siasa za Tanzania hazijadili masuala bali hujadili matukio na watu, kwa sasa hatuwezi kuchambua uimara wa serikali na udhaifu wa bunge.
Ninaamini siyo muda mrefu tutaacha kujadili udikiteta na tutahamia kwenye tukio lingine ili kuendeleza mahusiano na wanasiasa ambao hawajadili masuala bali matukio na watu!