Siasa za kutamba pasipo kujitambua

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Watanzania wengi waliupokea utawala wa awamu ya tano kwa matumaini makubwa sana japo kwa mujibu wa NEC saisa za mwaka jana zilikuwa na mchuano mkali sana kiasi cha kutoleta utofauti mkubwa sana kwenye matokeo ya mwisho hasa nafasi ya juu kabisa. Walioshinda ni dhahira kwamba wanatamba huku na kule kwani hata Jana Taifa Stars ingeshinda ni dhahiri Watanzania sasa tungekuwa tunatamba tena zaidi tungewatambia wamisri ambao walikuwa washindani wetu.

Hilo ni jambo la kawaida sana kutamba baada ya kushinda kikwazo fulani. Tatizo linakuja pale unapotamba pasipo kujitambua. Mfano, endapo Taifa Stars ingesonga mbele nakuanza kutamba pasipo kuelekeza nguvu na juhudi katika michuano ijayo ningeweza kusema wanatamba lakini hawajitambui! Yaani wanalewa sifa, kule kushangiliwa kila kona kumewapumbaza na sasa wamejisahau, hawajielewi! Hiyo ni kwa Taifa stars endapo ingeishinda jana Misri kwa hayo magoli manne na kufudhu kwenda mbele, lakini bahati haikuwa yao na hivyo hata huu mfano hauwahusu tena. Kwa upande wa siasa, mwanasiasa fulani anaposhinda uchaguzi halafu asitimize aliyowaahidi waliomchagua pia mfano huu waweza kumuhusu. Hivyo ni jambo jema kwa wanasiasa kutamba huku wakijitambua.

Wanaweza kufanya lolote wawezalo kufanya kwa uwezo na nguvu walizo nazo lakini wasiache kujitambua. Mfano :kutofautiana kwa kauli za kuwafukuza wanafunzi UDOM wa kozi maalum halafu unawaambia wakatafute vyuo vya size yao wakati Afisa uhusiano wa chuo anasema sifa walikuwa nazo, ni sehemu ya kutamba pasipo kujitambua kwani hao ndo walioahidiwa maisha mazuri! Kuendelea kufokea watu na kuwatisha wasiongee lolote la kukosoa au kushauri, nako nikutamba pasipo kujitambua! Kuwafukuza watu kwa kubomoa nyumba zao maeneo waliyoishi kwa miaka zaidi ya 40, nako nikutamba pasipo kujitambua!

Kuendelea na kufukuza fukuza watendaji hata waliofanya makosa miaka 10 iliyopita huku wananchi maeneo tofauti tofauti ya nchi wanauwa kama mbuzi nako nikutamba pasipo kujitambua! Ushauri wangu kwa wanasiasa wote waliofanikiwa kupata nafasi ya kuliongoza Taifa hili ni kwamba watambe huku wakijitambua kwasababu ipo siku watarudi tena kuomba ridhaa ya kurudi madarakani! Litakuwa jambo la kujisifu endapo watakaporudi kuomba ridhaa tena watakuta angalau wananchi hao umaskini wao umepungua!

Kiongozi mzuri ni yule anayeweka action plan halafu kwa mbele anachora kibox ambacho ataandika neno "EVALUATION" ili litakapokamilika aandike "SUCCESSFUL COMPLETED au INCOMPLETE" ili mwenzake au yeye mwenyewe ajue ataanzia wapi au ataanza na lipi kipindi kijacho sio kufukua kila linalofukuliwa kwani mwisho wa siku atashituka kuanza kujenga wakati muda umeisha tayari!

Viongozi wetu wakumbuke muda ni sehemu muhimu ya uongozi na kichocheo cha maendeleo kuwahi au kuchelewa!
 
Wenyewe wanauhakika miaka 5 ijayo hata washinde au wasishinde wanajua ushindi ni wao na ndio maana hata wakialibu hawana wasiwasi wanajua nchi ni yao waliokota kutoka kwa mkoloni.
 
Hawa wameshafeli siku nyingi sana, akili ndogo haijawahi ongoza akili kubwa.
 
Back
Top Bottom