hindikwetu
JF-Expert Member
- Jul 20, 2015
- 251
- 86
Taifa lolote linahitaji siasa safi, ili kufikia utekelezaji wa sera zilizopo zinazolenga kujenga taifa Husika.Siasa safi daima ni ile ya kuona vyama vya siasa vikiwa busy,kutekeleza shuguli zake za kila siku ili kufikia ustawi kamili katika kujenga chama. Siasa za Tanzania kwa muda mrefu sasa tangu kuingia katika mfumo wa vyama vingi,binafsi sijaona harakati chanya za kuhakikisha kweli siasa zinakuwa na tija,bali zimekuwa siasa za ukewenza na kuacha ujenzi wa vyama na kujenga utaifa badala yake, wimbo unaoimbwa hauonyeshi kujikosoa utendaji wa ndani ya vyama, bali ni vidole vyote vitano kwa serikali.Huku baadhi ya yale yanayokosolewa dhidi ya serikali yamo pia kwa vyama sasa hapa tija iko wapi. Hata pale yanapotokea mambo ya mamlaka husika kufanya kazi utasikia miruzi mingi ya kisiasa na kelele.Tukumbuke miruzi mingi hupoteza mbwa,chonde wanasiasa kuweni na siasa za tija kuliko kucheza na akili za wananchi kwa ufundi wa kugeuza maneno na kujihami. Pia kuweni wazalendo kwa taifa na muwe na huruma kwa wananchi.