Tatizo la East Africa Federation ni moja. Wanaofanya integration ni viongozi kwa kujifungia Hilton,Kempisk, etc na kula vitumbua na chai na kujadili hiyo Federation. Lakini je mkulima wa Tandahimba anakutana na mkulima wa Meru kujadili na kufanya mipango ya pamoja ya namna ya kuinua kilimo? Tukifika hapo ndopo tutakuwa na Federationya ukweli. Hii nyingine ya viongozi ni ya kihunihuni tu. Kwa nini wanafanya federation kama vile ni project? Project ina mwanzo na mwisho, lakini kazi ya kuunganisha watu ambao wanatofauti za kisiasa na za kiuchumi na hata kifalsafa inahitaji kuwa programmatic zaidi! Mfano Kenya wametengeneza katiba mpya na wanaitekeleza sasa, na wanafanya jitihada kwelikweli. Lakini Tanzania zoezi katiba mpya limeanza kwa mizengwe, hapa wakautita ni "Constitutional Review Act" na sio "New Costitutional Act". Yaani ni uhuni tu hasa kwenye mambo ya msingi.Sasa kama jirani yako unayetaka kushiriakiana naye amefanya jambo zuri na wewe unataka kufanya jambo hiliohilo huwezi kumuuliza akakupatia uzoefu? Sasa mbona hatujawauliza wenzetu wamefanyaje kupata katiba mpya? Je kama hatuwezi kuulizana,kusaidiana na kushiriakiana kwenye mambo ya msingi kama haya tutasaidiana wapi? Sio ndio intergration yenyewe hiyo? Si ndio intergration process hiyo Tatizo la viongozi wetu ni kufikiri na kutenda kiimla na kijumla zaidi kwa sababu ya mawazo mgando. Wanataka Federation ifanyike leo au baada ya muda mfupi badala ya kuweka utaratibu ambao utazaa federation, hata kama itachukuwa miaka mia,but it has go to be done right!