Siasa za Chuki, visasi na hatima yake

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Ni kweli kama kuna mtu alikua akiibia serikali ni vizuri ajawajibishwe kwa mijubu wa sheria, lakini mambo yanapofanywa kinyume na sheria ndipo matatizo yanakoanzia.


Sasa mtu kama Mh Mbowe ameanza kufanya biashara enzi za Mwalimu Nyerere, Mwinyi,Mkapa na Kiwete inamaana hawa wote hawakuona kua mbowe ana matatizo na biashara zake? Kwanini hawa wote hawakumgusa walimwacha aendelee kuliibia taifa? Hivi ni kweli mbowe alikua halipi kodi ilihali akijua ni wajibu wake? Kwani yeye alikua ni sehemu ya serikali hizo?


Najiuliza sana ni kwanini tunafikia huku?Nini hatima ya siasa zetu hizi?
Maana wafanyabiashara ndio wanaotuendeshea taifa! Kama mtu kesi iko mahakamani ni kwanini tusifuate sheria kumwadhibu badala ya kumkimbiza kimmbiza kama mwizi?


Nisihusishwe na fikra zozote hasi,ninejaribu tu kufikiria huko tunakoelea kwa siasa zetu hizi.
 
Back
Top Bottom