Siasa ya Tanzania (J.K Nyerere na siku zetu sehemu ya 1)

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,333
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyezaliwa Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Victoria mwaka 1922 Mwezi wa 4 - Huyu ni rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "baba wa taifa". Kwa maana ya kuwa Ni muasisi wa Taifa Hili la Tanzania. Ndiye aliyeanzisha pamoja na wazee wengine Jitihada za "kuomba kupewa Uhuru kwa kupitia Chama Cha TANU na akiwa Rais wa kwanza pia mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha.

Kuna mengi ambayo watu wengi wameshazungumzia kuhusu Mwl Nyerere ambayo mimi sina haja ya kuyarudia kihistoria iwe ni kweli au si kweli. lakini leo ninalowez kusema kuwa kama tutamhukumu Nyerere tumhukumu wala sipingi. lakini kuna jambo moja la msingi sana ambalo Tulipasa kujifunza kwa Nyerere. Nyerere alikuwa ni kiongozi mwenye maono, mwenye uelekeo, mwenye imani na msimamo. "kuna usemi kuwa ni bora utende ukosee kuliko kutotenda na kukawa hakuna lolote jipya" Nyerere alijaribu kuonesha njia. alikuwa ana Tanzania anayoitizama siku za usoni. alikuwa ana imani inayomwongoza kuendesha nchi na tunaona kuwa mpaka anafariki hakuwah kuyumba kwenye misimamo yake tofauti na wengine wengi aliowaacha akina Kingunge, Kolimba, Warioba n.k ambao hawa waliingia kwenye mkumbo wa mabadiliko ya kiimani/itikadi na kujikuta wakisombwa na unyeng'enyevu wa kiitikadi na kuyumbishwa na mafuriko ya uchumia tumbo na itikadi za Kujilimbikizia Mali wao na Familia zao.

Nyerere aliamini Ujamaa na kujitegemea imani ambayo ndiyo leo hii inaiweka china kuwa moja ya Taifa kubwa Duniani. Miaka kadhaa iliyopita China nao walikuwa wakisikitika na kuumia kama ambavyo watanzania waliumia kipindi cha nyerere lakini kwa china kujitegemea waliweza kujifunza mengi kutokana na Mazingira magumu waliyokuwa nayo na kufanikiwa kuendelea kiuchumi kwa hatua waliyopo sasa. Hili lilihitaji maono kuweza kuligundua athari na faida zake.

Hali ilipokuwa mbaya sana kwa kuona kuwa siasa yake inashindikana naye hawezi rudi chini kuwasujudia hawa aliokuwa akiwapinga aliachia madaraka kwa Hiari yake mwenyewe. awapishe ambao wangeweza kuendana na ulimwengu uliokuwepo miaka hiyo. Bado aliendelea kuamini alichoamini na hakusika kuwakosoa wale waliokuwa madarakani kwa uwazi pasipo kujiuma uma. alikuwa mwanasiasa aliyeamini alichoamini.

SIKU ZETU , Tumekosa wanasiasa wenye kariba ya Nyerere, Chifu abdallah Fundikira, Kassanga tumbo wa miaka ile n.k sasa tumekuwa na WANASIASAJASILIAMALI . hawa tumewaona namna ambavyo wamekuwa wakitumia siasa kujitajirisha kupitia ulimbukeni,ushabiki na wananchi mandondocha/misukule. ni nani leo hii aliyekuwa anamwona DR Mwakyembe Shujaa na mzalendo na akamwona ni Dr Mwakyembe yuleyule? aliyemwona Samuel Sitta mzalendo akamwona vile vile? nani anamkumbuka Anne kilango malecela akifoka kuhusu suala la Richmond na mama huyu huyu ndiye aliyekuwa amenyamza kwenye suala la Escrow kana kwamba hayupo? Dr Slaa huyu aliyekuwa akiipiga vita CCM ndiye aliyekuja kushirikiana nayo kuua upinzani?

Tuna watu wengi ambao wamekuwa na misimamo ambayo ni HOMA ZA VIPINDI. wamekuwa wakiyumba kutokana na Nani yupo madarakani na atafaidika na nini kwa kuwepo huyo madarakani. wanasiasa,wananchi,wachambuzi wangapi wamekuwa wakifanya/wakichambua siasa kimi hemko? kwa kuangalia sasa ni nani yupo kwenye madaraka? Dini gani, Kabila Gani, Kanda gani, Tuna uhusiano gani n.k? tumeona hata ndani ya jukwaa letu JF watu wamebadili misimamo kwa kuwa sasa aliyepo madarakani wanatoka mkoa au kanda moja? ni mtu wa dini yao? wana undugu au ukaribu naye?

Tumeona waliokuwa wakimtetea sana Kikwete Mpaka kutoka Jasho na kuwa tayari kufa naye kisiasa sasa wakimponda Mh. Dr Magufuli kwa kuwa ni dini nyingine? Tumeona waliokuwa wakimponda Kikwete na kumwona kuwa ni mtu hopeless sasa wakimsupport Mh. Dr Magufuli

Siku hizi tumekosa wtu wenye misimamo. tumekuwa na watu wenye maslah binafsi na kuangalia siasa itawafanyia nini kiuchumi. Unapata wapi ujasiri wa kumtetea mbunge anayelipwa pesa nyingi mpaka akakusahau au akasahau kuwa wewe unalipwa 200,000 au 300,000 kwa mwezi? unawezaje sema huyu ni mwanasiasa mwenye uchungu na wewe? unawezaje kumtetea mbunge ambaye anashindwa kugoma ili adai wapunguziwe pesa wanazolipwa tena pasipo kukatwa kodi? haya ni mambo ambayo wananchi kama tusipokuwa makini tutakuwa na wakati mgumu hapo mbeleni. wanasiasa walichoweza kujifunza ni kuwa wanaongoza asilimia kubwa ya wananchi ambao walishachukuliwe Misukule, hawaoni,hawasikii,hawajitambui. kwa kigezo hicho wanaangalia zaidi maslah yao kuliko wananachi. ipelekewe hoja ya kupunguzwa mishahara ya wabunge, Hapo WAPINZANI NA WANACCM WATAKUWA KITU KIMOJA NA KUPINGA KWA NUGUVU ZOTE JAMBO HILO. kwa kuwa kiuhalisia hawapo kwa ajili ya kuwakomboa wananchi. na ndo maana huwa wanakuwa na mitaji mikubwa sana kugombea Ubunge. kiasi cha chini kabisa huwa nasikia ni Mil 50,000,000. mwanachi hujiulizi huyu Mbunge hizi pesa kwa nini azitumie kupata Ubunge? kunani huko kwenye Ubunge?

Halafu Mbunge huyu anaposimama kuongea huku mate yakiruka na akigonga meza kwa hisia unadhani anakuzungumzia wewe kama mwananchi kukusaidia. kweli nawaambia kwa Katiba hii iliyopo hata wangepita chama cha upinzani wasingebadilisha.wangetaka wakae nayo kwanza hii kwa miaka kadhaa ndo labda ije ibadilike.

Yu wapi Dr Slaa? yupo wapi Zitto kabwe, Yu wapi Dr Mwakyembe? yu wapi mama Anna Kilango Malecela? yu wapi kangi Lugola? wa wapi wapinzani wanaosema wanataka maslah bora ya wananchi? Je wanajua nani aliondoka na Viroba vya pesa za ESCROW? wamedai kujua ni nani na ameshughulikiwa vipi? IPTL,RICHMOND,EPA,MIGODI n.k

Wewe mwenzangu unatoa wapi nguvu za kumtetea mwanasiasa flani kwa Hoja za Vioja na imani kubwa kwake? SIKU ZETU ZIMEKOSA MWANASIASA MWENYE IMANI YA UKOMBOZI KWA WANANCHI. WAMEBAKI WANASIASAWAJASILIAMALI. nani alijua siku moja Mzee MM( msaka mali) atakuja kuwa ni msemaji wa CCM kutokana na makala zake za kukikosoa chama hicho? au aliyepewa zawadi ya Ukuu wa Wilaya kutokana na juhudi zake za kujitolea kwa hali na mali kukitetea chama? nani alijua Mzee Warioba aliyedhalilishwa na harakati zake kukwamishwa pamoja na katiba pendekezi kuja kusimama jukwaa moja na waliombeza na kumtweza ili kumsaidia mwanawe pia apate cheo?

NAKULILIA TANZANIA, INAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE CHOYO.
 
Back
Top Bottom