Siasa vs usalama: Polisi hebu changeni karata zenu vema

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Naona mvutano wa polisi na wanasiasa umeanza mapema kuliko nilivyoutarajia! Si ishara nzuri kwa kuwa Africa hali hii imezoeleka sana nyakati za uchaguzi naa Mara nyingi Africa huwa haiwi salama kabisa kipindi hicho!
Nini kiini cha mgogoro?
Nani anawajibika?
Nini kifanyike kuhakikisha usalama wa nchi na raia wake vinaendelea kutunzwa?
Haya ni maswali ambayo IGP itampasa ajiulize, wanasiasa wanapaswa wajiulize na jamii inapaswa kujiuliza!
Kwa kuwa polisi wameshakiri kuwepo kwa tishio sababu ya mikutano ya kisiasa, then kusema tu isimamishe mikutano yote indefinitely haiwezakani kwa kuwa itaongeza tension, lkn lini waruhusu mikutano kuendelea nacho ni kizungumkuti!
Je kuna tishio kweli, hakuna anayejua?
Serikali nayo inasemaje?
Anyway, Mimi rai yangu kwa Mkuu wa jeshi la polisi nchini ni kuanza kujenga mazingira shirikishi ktk ulinzi na usalama wa nchi kwa kupitia siasa!
Kwanza, vyama vya siasa vyote vifute vikosi vyao vya ulinzi, kwa maana vianze kushirikiana na askari ktk kujilinda!
Pili, jeshi la polisi, msajili wa vyama vya siasa na viongozi wa juu wa vyama vya siasa na wawakilishi wa makundi ya kijamii wakutane kujadili juu ya usimamizi wa usalama hasa nyakati za mikutano ya kisiasa, chaguzi na shughuli nyingine za kijamii zinazowahusisha na wanasiasa pia!
Lengo kuu ktk haya ni askari kuwapa Uhuru zaidi wanasiasa huku wakitimiza wajibu wao wa kulinda raia!
Mimi ninachokiona kwa sasa ni polisi kutowaamini wanasiasa zaidi kuliko tishio halisii la uvunjifu wa amani! Wakiwa na dialogue polisi watawajua vema wapinzani, wataji ji-assess na kutazama maeneo yanayohitaji kulindwa zaidi etc!
Sisi kama raia tunataka kila kitu, Demokrasia, usalama na maendeleo, na vyote hivyo vinaweza kuwepo au kutoweka kama busara haitotumika!
 
Back
Top Bottom