japanese
Member
- Jul 28, 2015
- 13
- 16
Leo ni muda wa takribani wiki mbili zinakatika tokea uvumi na hatimae kujulikana dhahiri kuwa yule mgombea aliyeenguliwa kwenye mchakato wa uraisi ndani ya ccm mh.lowassa kuwa amejiunga na vuguvugu la vyama vya upinzani maarufu "ukawa", lakini cha kushangaza ni kwamba Yale yaliyotabiriwa kuwa nguli huyu toka chama tawala angemeguka na wale wote waliokuwa wakimshabikia pindi alipokuwa ccm bado ni kitendawili kilichokosa mteguaji.ndio kusema wanasubiri nap watoswe kwenye mchakato wa kura ya maoni ya ubunge na udiwani au ndio " kimwili wako ccm na kiroho wapi ukawa ".