Siasa is dynamic kweli: Watangaza nia 2020 wapo???

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Nimekuwa najaribu kuangalia hali ya siasa nchini kwa muda sasa. Kweli nimekubali siasa ni dynamic sana katika maisha ya binadamu.

Mwaka 2010, kila mtu alikuwa ameichukia serikali ya CCM. Malalamiko mengi yalikuwa uongozi mbovu na wanasiasa kujiweka kuwa miungu watu.

Kilichokuwa chini ya panzia ni kila mtu aliona anaweza kutumia mwanya huo kupata hata nafasi ya ubunge, kupitia hasa upinzani ili aweze kupata hela zile zilizokuwa zinazagazaga katika siasa.

Kila kukicha kulikuwa na watangaza nia ya ubunge au udiwani kupitia vyama vya upinzani, hasa CHADEMA.

Mimi ni ...... Nimesoma mpaka ..... madaftari yakatoboka yote. Natangaza 2015 kugombea ... katika wilaya/jimbo/kata ya .... Ninatarajia kufanya yafuatayo:....

Hili wimbi la watangaza nia lilileta hata visasi kati yao katika vyama.

Najaribu kuangalia 2020, nani atajitokeza tena haraka haraka kamwa 2010? Sijaona!

Maslahi ya siasa yamepungua sana na kama unataka siasa nenda kwa ajili ya kutumikia watu si kupiga fedha tena.

Asanteni.

Gaza.
 
Back
Top Bottom