Si wakati wa kufanya siasa nyepesi

  • Thread starter Mwanahabari Huru
  • Start date

Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,538
Likes
27,525
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,538 27,525 280
Kuanzia siku ya Jana kumekuwa na upotoshwaji wa taarifa wa makusudi kumhusu Mh. John John Mnyika aliokuwa ukisambazwa na baadhi ya wafuasi wa vyama vingine Kwa nia tu ya kuchafua hali ya kisiasa iliyopo ndani ya CHADEMA na UKAWA Kwa ujumla.

Mh. Mnyika mwenyewe ameshakanusha kuhusiana na Hilo hata Chama pia kimeshakanusha na kusema kuwa kitachukua hatua zilezile kuhusiana na sheria za kimtandao Kwa wote waliosambaza habari hiyo ya uongo.

Pamoja na hayo kuna baadhi ya watu ambao tumekuwa tukijadiliana nao kwenye mitandao mingine waliokuwa na maswali mbalimbali juu ya ukimya wake hasa ukizingatia jinsi ambavyo alikuwa amejipambanua huko nyuma na Hilo ndio hasa ninalolihitaji kulizungumzia hapa kiundani kidogo ili tuwekane sawa ili kuondoa upotoshaji huo Kwani tunajua wakimalizana na Mh Mnyika watakuja Kwa Mh Halima Mdee n.k hivyo ni bora sisi kama vijana tuliopata bahati ya kujua na kuelewa kiasi fulani kinachoendelea tuseme ili kuwekana sawa Kwa hoja zifuatazo.

Kwanzaa nianze Kwa kusema CHADEMA Kwa sasa kinaondoka katika mfumo wa kiuharakati na kuja katika mfumo wa kitaasisi baada ya kufanikiwa kukijenga vizuri kupitia harakati zilizofanywa na wanaharakati mbalimbali hasa vijana wenzangu kama mimi.

Taasisi yoyote iliyojitambua haiwezi kuwa na msemaji mmoja au wawili Kwa kila jambo linalohusu taasisi hiyo ni lazima kuwe na mgawanyo wa majukumu husika Kwa kila mtu Kwa nafasi yake kuzungumzia kile kinachomhusu katika sehemu aliyopangiwa.
Leo hii CHADEMA unaizungumzia inayoongoza majiji makubwa matatu na Halmashauri zaidi ya 26 hivyo hata utendaji kazi wake hauwezi kufanana na wakati wanayatafuta hayo majiji kuwa chini ya himaya Yao kupitia UKAWA.

Ni siasa nyepesi tu ndio iliyotumika kumchafulia taswira yake Mh Mnyika na nadhan kama asingekuwa yeye basi angekuwa Mh Tundu Lissu kama isingekuwa hii kesi ya juzi au pengine Mh Halima Mdee hiyo ni kutokana watu wahajawaona kupitia Bunge kutokana misimamo ya Ukawa na wakati huohuo hawasemi ya nje kutokana na kile nilichokisema awali mgawanyo wa majukumu.

Kama Leo hii wakina Mh Mnyika wangeendelea kuwa wasemaji wakuu wa kila jambo hata masuala yaliyokuwa yakihusu hata umoja wa vijana CHADEMA ni nani Leo angemfahamu Mh Patrick Ole Sosopi nje na vijana wa CHADEMA.
Chama kilikuwa kinafanya hivyo kwakuwa kilikuwa kinajua kuwa masuala yale anapoyaongea Mh Mnyika ni tofauti katika upokelewaji na atakapoyaongea Mh Patrobas Katambi hiyo yote ni kutokana na huyu mmoja kujijenga kupitia Bunge wakati huyu mwingine anahitaji mikutano Mingi sana ya hadhara.

Leo hii tunakosa kuwafahamu uwezo wa kisiasa makamanda kama Mh Upendo Peneza, Lijuakali, Anatropia Theonest, Lucy magereri, Jesca Kishoa, Millya N.k hiyo ni kutokana na uwanja wao kufungwa hivyo kutufanya sisi tusiwaone uwezo wao kama ambavyo wakina Zitto na Mnyika walivyoitumia vizuri fursa hiyo.

Kwamfano ilipotokea ishu ya Lugumi msemaji Mkuu alikuwa Mh Lema ambaye ndiye aliyekuwa waziri Kivuli wa wizara ya mambo ya ndani sio kwamba wakina Mdee walikuwa hawalifahamu la hasha kilichokuwa kinafanyika ni kila mtu kusimamia kile kinachomhusu watu wengine watakuwa wasemaji wa kawaida.

Ilipotokea suala la mikutano ya vijana wa vyuo vikuu kuzuiwa Mh Sosopi na wenzake wameyasimamia hayo sio kwamba Mh Mbowe halimgusi la hasha nia ni kuondoa utegemezi wa bila fulani mambo hayaendi nia ni kujenga Taasisi itakayokuwa imara kila Kona na kila Idara Kwa nguvu Ile Ile moja.

Zamani kila kesi ya CHADEMA utamuona Mh Tundu Lissu lakini sasa hivi kapunguziwa majukumu ambayo hatimaye Leo Mh John Mallya na Peter Kibatala wanaonekana ndio mawakili vijana hodari na Maarufu hiyo yote ni kupeana nafasi ili kujijenga zaidi kuwa hata kama Mh Lissu atakuwa anaumwa Mh Mallya atasimama mahakamani kukitetea chama na atashinda kesi hiyo bila ya Mh Lissu kuwepo.

Leo hii Mzee wetu Mtei sio kwamba amehama CHADEMA au hafurahishwi na yanayoendelea ndani ya Chama ndiomaana hazungumzi zungumzi kama alivyokuwa akifanya awali wakati anakijenga chama la hasha Bali kazi aliyoifanya ya kuwakusanya wakina Mh Mbowe na kuwasimamia ndio hiyo iliyozaa matunda ambayo Leo Mh Mbowe amemletea wajukuu ambao yeye si kazi yake kuwalea tena Bali ni kumpa ushauri Kijana wake pale atakapokwama katika malezi ya familia yake.

Tulipotoka CHADEMA ndipo walipo sasa hivi ACT wazalendo ndiomaana Leo kila jambo analisema Mh Zitto Kabwe sio kwamba hakuna viongozi wengine wapo wengi kama Ado Shaibu, Mama Anna Mghwira, Dr. Kitila Mkumbo lakini Je tamko atakalolisema Mh Zitto Kabwe uzito wake utakuwa sawa na atakapolitoa Ado Shaibu la hasha hiyo ni kutokana na Mh Zitto tayari alishajijengea jukwaa lake hivyo anatumiwa yeye kama njia ya kuwatengenezea na wengine majukwaa hayo hivyo utafika wakati yeye majukumu yake yatapungua kama ilivyosasa Kwa Mh Mnyika.

Muhimu zaidi tukumbuke kuwa sasa hivi CHADEMA kipo katika umoja wa Ukawa hivyo hata utendaji kazi wake ni lazima utofautishwe ili kulinda maslahi ya umoja huo Kwa vyama husika na jamii Kwa ujumla na ndiomaana mambo yote makubwa yanazungumzwa na viongozi wa umoja huo sio Chama kama Chama ni UKAWA Kwa ujumla ambao ina viongozi wake ndio huyasemea.
 

Forum statistics

Threads 1,238,214
Members 475,877
Posts 29,312,966