Shule za Kiislamu Tanzania

Shule za Kiislamu Tanzania

Abuu Dharr

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
2,912
Reaction score
3,021
Katika hali ya uchungu yenye maumivu tele, tumeona baadhi ya wadau wakisema ibaya Uislam hususan Madrasa, kama kimbilio kwao na kupata sababu mama ya kufeli mashule ya Islamic.

Labda tufahamu hili; Mashule meengi yameanzishwa na Wafanyabiashara na wasio na uelewa na elimu, hii inapelekea shule nyingi kuwa chini kimaendeleo.

Mfano mdogo:
Shule ina wanafunzi zaidi ya Mia 5, Walimu walioajiriwa ndani ya Shule hizo, Imma ni mwalimu aliyemaliza kidato cha sita na kusubiri majibu, au ni wale ambao walifeli hapo mwanzo, na kukimbilia Ualimu.
Walimu wa sampuli hizi, ndio wengi walioajiriwa mashule ya Islamic.

Kwa hapa tu, sidhani uzuri wa matokeo.

Pili, Mwanafunzi hana uwezo, hajui kitu wala hataki kujua, lakini atapokelewa bila kupingwa, muhimu ni pesa tu.

Na yale magarasa yanayofukuzwa Shule kama ya FEZA, hukimbilia huko Islam Schools.

Hapa pia usitaraji furaha ya matokeo, bali utapokea vilio.

Tatu, namna na mbinu za ufundishaji, wengi wa watu, wanadhani kusoma masaa mengi kwa mtoto ndio kufaulu, utaikuta shule inafundisha kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa 5 usiku. Hakuna michezo wa kupumua, ni kusoma tu, mbaya zaidi, utawakuta wanafunzi wa la saba.

Kwa style hii, hakuna matarajio bali ni vilio tu kadhalika.

Nne, hakuna anayekataa au atakaebisha, ubaya wa mashule haya ya kata.

Yote haya, ni kwasababu ya elimu duni itolewayo ndani yake.

Ndugu zangu, kutukana na kubeza sana, si solution ya matatizo.

Tuijenge nchi yetu kwa misingi ya amani baina yetu, huku tukitaka elimu bora.

Madrasa (za uhakika) humfundisha mtoto tabia njema, na kuishi katika kujitambua.

Tusibeze Ikiwa wewe hujui faida yake

Nasaha zangu kwa Waislam wa Tanzania:

- Tuziangalieni haya mashule yetu, kiuhalisia hakuna utawala bora.

- Tujenge kwanza uzalendo na utawala bora baina yetu, nina hakika tutafanikiwa kwa idhni yake Mola.

Shukrani sana

Usiku mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana sababu zako zina mashiko kifogo. Usisahau mfumo usio rasmi ni kuonesha kuwa Waislamu ni dhaifu, hivyo kufeli ndio stahiki yao. Hili si kweli. Tunapaswa kuangalia mfumo mzima wa usimamizi wa elimu baadae tuje kulaumu. Kwa mfumo wa sasa tutafakari kwanza kabla kulaumu. Sisemi kwamba hayo uloeleza hayapo, ila yanachapuzwa na mfumo uliopo. Tuzindukeni.
 
Abuu Dharr,
Uislaam hauruhusu kuchuja na kufukuza watoto wasio na uwezo, kw shule zetu zina waroro wenye div 1 had Div 0 na hakuna tunaye shindana nae.
 
Uislaam hauruhusu kuchuja na kufukuza watoto wasio na uwezo, kw shule zetu zina waroro wenye div 1 had Div 0 na hakuna tunaye shindana nae....
Point dhaifu kabisa hii.. sema hivi nyie elimu sio kipaumbele chenu bali mnafosi tu ili kuendana na wenzenu. Ifike muda tu mchague nyie mtasoma madrasa tu maana mnaziwezea sana.
Si mnasema elimu dunia haina faida so msitafute excuse.

Shikeni elimu nyie..hamuoni wenzenu wakatoliki tunaenda na vitu vitatu Elimu,Imani na Afya. Kwenye kanisa unakuta kuna hospital na shule.

Nyie kwenu mnaishia kupanda mitende tu na maembe..Elimu inatafutwa haipewi. Ngoja niishie hapa maana povu nililonalo ajili ya nyie kupenda kulialia na kuonewa huruma ni jingi sana
 
Inawezekana sababu zako zina mashiko kifogo. Usisahau mfumo usio rasmi ni kuonesha kuwa Waislamu ni dhaifu, hivyo kufeli ndio stahiki yao. Hili si kweli. Tunapaswa kuangalia mfumo mzima wa usimamizi wa elimu baadae tuje kulaumu. Kwa mfumo wa sasa tutafakari kwanza kabla kulaumu. Sisemi kwamba hayo uloeleza hayapo, ila yanachapuzwa na mfumo uliopo. Tuzindukeni.

Matatizo ya elimu yetu ni mengi na percussion zake zinagusa kila upande, nitoe mfano wa Kinondoni Muslim ni shule nzuri tu lakini kuna wakati kuajiriwa pale ilikuwa mpaka uwe mwenzao wakati wenzao wanaangalia GPA, na kule kwetu wanachukua walimu mshahara mdogo wanafunzi darasani 120, kule Kilimanjaro mtoto wa ndugu yangu alihama shule ya kiislam kisa alidai kuwa toka saa 11 asubuhi ni busy plus swala 5 masomo ni kidogo na kwa mbali sana na somo la dini eti ni lazima
 
Point dhaifu kabisa hii.. sema hivi nyie elimu sio kipaumbele chenu bali mnafosi tu ili kuendana na wenzenu. Ifike muda tu mchague nyie mtasoma madrasa tu maana mnaziwezea sana.
Si mnasema elimu dunia haina faida so msitafute excuse.

Shikeni elimu nyie..hamuoni wenzenu wakatoliki tunaenda na vitu vitatu Elimu,Imani na Afya. Kwenye kanisa unakuta kuna hospital na shule.

Nyie kwenu mnaishia kupanda mitende tu na maembe..Elimu inatafutwa haipewi. Ngoja niishie hapa maana povu nililonalo ajili ya nyie kupenda kulialia na kuonewa huruma ni jingi sana

Nyie msiosoma madrasa, mmefaidika nini? Mbona hamjajitawla kifikra?
 
Point dhaifu kabisa hii.. sema hivi nyie elimu sio kipaumbele chenu bali mnafosi tu ili kuendana na wenzenu. Ifike muda tu mchague nyie mtasoma madrasa tu maana mnaziwezea sana.
Si mnasema elimu dunia haina faida so msitafute excuse.

Shikeni elimu nyie..hamuoni wenzenu wakatoliki tunaenda na vitu vitatu Elimu,Imani na Afya. Kwenye kanisa unakuta kuna hospital na shule.

Nyie kwenu mnaishia kupanda mitende tu na maembe..Elimu inatafutwa haipewi. Ngoja niishie hapa maana povu nililonalo ajili ya nyie kupenda kulialia na kuonewa huruma ni jingi sana
Mkuu huko huko agiza mbege!
Kikubwa hawa watu na wasisome, kwani dunia haiwi tamu kama kila mtu kasoma.Nani atapiga debe stendi, nani atabeba mizigo, nani tatufanyia kazi za ndani, bustani, ulinzi, dereva,nk
 
Ngoja bibi akukute
Point dhaifu kabisa hii.. sema hivi nyie elimu sio kipaumbele chenu bali mnafosi tu ili kuendana na wenzenu. Ifike muda tu mchague nyie mtasoma madrasa tu maana mnaziwezea sana.
Si mnasema elimu dunia haina faida so msitafute excuse.

Shikeni elimu nyie..hamuoni wenzenu wakatoliki tunaenda na vitu vitatu Elimu,Imani na Afya. Kwenye kanisa unakuta kuna hospital na shule.

Nyie kwenu mnaishia kupanda mitende tu na maembe..Elimu inatafutwa haipewi. Ngoja niishie hapa maana povu nililonalo ajili ya nyie kupenda kulialia na kuonewa huruma ni jingi sana
 
Point dhaifu kabisa hii.. sema hivi nyie elimu sio kipaumbele chenu bali mnafosi tu ili kuendana na wenzenu. Ifike muda tu mchague nyie mtasoma madrasa tu maana mnaziwezea sana.
Si mnasema elimu dunia haina faida so msitafute excuse.

Shikeni elimu nyie..hamuoni wenzenu wakatoliki tunaenda na vitu vitatu Elimu,Imani na Afya. Kwenye kanisa unakuta kuna hospital na shule.

Nyie kwenu mnaishia kupanda mitende tu na maembe..Elimu inatafutwa haipewi. Ngoja niishie hapa maana povu nililonalo ajili ya nyie kupenda kulialia na kuonewa huruma ni jingi sana
Madrasa kubwa Africa Al Azhar university ndio pia chuo kikubwa Kabisa Africa mfano wa Graduates wa Al Azhar ni kama

1. Aliko Dangote Tajiri mkubwa zaidi Africa ambaye alisomea shahada ya Biashara ya kiisilamu.
2. Ossama youssef founder wa Diwan Videos multi chanell kubwa zaidi Africa yenye views zaidi ya Bilioni 10
3. Abdulrahman Wahid aliekuwa Rais wa Indonesia
4.Maumoon Gayum Raisi wa Maldives
5. Barhhanudin Bahani raisi wa Afghanistan
6. Ahmed Yasin Founder wa Hamas etc

Naweza kuchallenge taja chuo chochote Africa kiwe katoliki ama chengine kilichotoa products zinazoinfluence dunia kuanzia maraisi wa Nje ya Africa, watu matajiri, successfull business startup etc.
 
Utakuwa na matatizo mengi kichwani!

Sent using Jamii Forums mobile app

Kisa tu i have a diffrent opnion than yours??

Umetoa hoja, nimekujibu huwezi kuta shule ya kiislam ikiongoza kwenye ranking za matokeo ya necta sababu hawafukuzi/chuji wanafunzi neither have they commercilized elimu?

Matatizo yangu mengi kichwani ni yepi hapo??

Angalia matokeo kama haya??

Kuna matokeo ya Div 1 hadi Div 4 55 students with clean results mnataka wote wapate A ndio mseme kuna wasomi?
 
Madrasa kubwa Africa Al Azhar university ndio pia chuo kikubwa Kabisa Africa mfano wa Graduates wa Al Azhar ni kama

1. Aliko Dangote Tajiri mkubwa zaidi Africa ambaye alisomea shahada ya Biashara ya kiisilamu.
2. Ossama youssef founder wa Diwan Videos multi chanell kubwa zaidi Africa yenye views zaidi ya Bilioni 10
3. Abdulrahman Wahid aliekuwa Rais wa Indonesia
4.Maumoon Gayum Raisi wa Maldives
5. Barhhanudin Bahani raisi wa Afghanistan
6. Ahmed Yasin Founder wa Hamas etc

Naweza kuchallenge taja chuo chochote Africa kiwe katoliki ama chengine kilichotoa products zinazoinfluence dunia kuanzia maraisi wa Nje ya Africa, watu matajiri, successfull business startup etc.
Chuo kingine? UDSM, una swali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom