Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2018 kwa mara nyingine yameshuhudia shule binafsi zikitamba kwa ufaulu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa wiki iliyopita na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), hakuna shule hata moja ya Serikali iliyofurukuta na kuingia katika orodha ya shule 10 bora.
NECTA ilizitaja shule hizo kuwa ni
St Francis Girls iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa. Nyingine ni
Kemebos,
Marian Boys’,
Ahmes,
Marian Girls,
Canossa,
Bright Future,
Maua Seminari,
Precious Blood na
Bethel Sabs Girls.
Unapochambua matokeo hayo, shule ya kwanza kwa ufaulu upande wa Serikali ni
Ilboru ya mkoani Arusha, ambayo katika ufaulu wa kitaifa imeshika nafasi ya
36. Imejongea kwa nafasi tatu kwa kuwa katika matokeo ya mwaka 2017, ilishika nafasi ya 39.
Ilboru ndiyo shule iliyotoa mwanafunzi bora katika mtihani huo,
Hope Mwaibanje.
Shule nyingine zinazounda kundi la shule 10 bora za Serikali na nafasi zao kitaifa kwenye mabano ni:
Kibaha (
45),
Mzumbe (
48),
Tabora Boys’
(
67),
Kilakala (
76),
Tabora Girls (
90),
Msalato (
102),
Chang’ombe (
227),
Kibasila (
236) na
Jangwani (
239).
Pamoja na kutengeneza kundi hili la shule bora za Serikali, inasikitisha kuwa shule hizo zimeshindwa kupenya na kuingia katika orodha ya shule bora 20. Hii ni ishara kuwa shule za Serikali bado zina kibarua kizito katika ushindani wa kitaaluma na shule binafsi.
View attachment 1007720
Mwananchi