Je! Umewahi kutazama watu na kwa kweli ukaitamani furaha yao, ukatamani kuwa wao?
Nikupe siri moja kile kinachokufanya utamani kuwa kama wao ni thelusi tu ya maisha yao halisi na kama ungeliona uhalisia wa maisha yao, usingelithubutu hata kutamani kuwa kama wao.
Yule uliye muona anadrive ndinga kali na ukaitamani, anasumbuliwa na kisukari, yule anayemiliki mjengo mkali hapo mtaani, hana amani na mkewe na wakati mwingine inamlazimu kupitia bar ili achelewe kufika nyumbani.
Huyo mrembo unaetamani kuwa kama yeye, anakifafa na kila usiku lazima kimsurubu hadi anajiona kuwa hana thamani.
Ukweli ni kwamba hatuna chochote. Kabla hujatamani kuwa kama yule muulize MUNGU kwanini hakukuumba yule.
Kaoge alitamani kuwa mwanamke, bahati haikuwa upande wake maana alomuumba alikuwa na kusudi, katika umri mdogo mno, leo hatuna kaoge katika uso wa dunia.
Usitamani sana kuwa yule maana kuna sehemu ya usichokijua juu yule unayetamani kuwa kama yeye.
"Shukuruni kwa kila jambo"
Biblia