Shirika la ndege la Serbia lapiga hatua katika kuboresha huduma zake

John Mwelele

Member
Apr 16, 2016
18
17
Pic 1 Air Serbia A330.jpg

Shirika la ndege la Serbia, ambalo ni shirika la ndege la Taifa la Serbia, lilisherehekea hatua nyingine katika mabadiliko kama shirika la ndege linaloongoza katika kanda, kwa kuwasili kwa ndege yake kubwa ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Nikola Tesla jana.

Ndege aina ya Airbus A330 itatumika katika ruti za shirika la ndege la Serbia kati ya Belgrade kwenda New York, Ambayo itazinduliwa tarehe 26 Juni 2016, ikiunganisha Serbia na Marekani kwa huduma ya ndege ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza katika miaka 24.

Baada ya kutua Belgrade, ndege hiyo ililakiwa kwa salamu za kitamaduni za urushaji wa maji na kukabidhiwa kwa wawakilishi wa ndege hiyo. Waliokuwa katika safari ya kwanza ya ndege hiyo ya kihistoria ni kundi la wadau wakubwa wakiongozwa na Siniša Mali, Mwenyekiti wa shirika la ndege la Serbia na Meya wa Belgrade, na Dane Kondić, Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Serbia.

Ndege hiyo ilikuwa inaongonzwa na Kaptein Davor Mišeljić, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Serbia, na sasa itasajiliwa na Idara ya Usafirishaji na Uchukuzi ya Serbia (Serbian Civil Aviation Directorate) kabla ya kurejea tena Abu Dhabi kwa ajili ya kukamilisha sehemu za vyumba vya ndege hiyo.

Bwana Mali alisema: “Hii ni hatua kubwa sana kwa shirika la ndege la Serbia na taifa kwa ujumla. Kutazama ndege yetu ya kwanza iliyochorwa picha isemayo Airbus A330 ikitua katika kiwanja chake kipya hapa Belgrade kwa mara yake ya kwanza ilikuwa ni wasaa wa faraja kwetu, kuona kuwa Ndege kubwa inakuja kuwekeza katika hatma ya shirika hili la ndege na taifa la Serbia pia.

“Ndege yetu kubwa kabisa na ndege zetu nyingine kubwa za A319, A320, ndege na A330 ni uwekezaji ulio bora zaidi ambao utaiunganisha Serbia na Marekani katika wiki chache itafungua utalii na biashara kwa ajili ya uchumi.”

Ndege hiyo ina viti 18 katika Daraja la biashara na viti 236 katika daraja la uchumi. Ndege hiyo Aina ya Airbus A330 itafanya safari zake katika safari tano mpya za kila wiki za shirika la ndege la Serbia kati ya Belgrade na New York.
Pic 3 Air Serbia A330.jpg


Kuwasili kwa A330 ni hatua mpya kabisa katika hatua za msingi za programu ya kuongeza ndege (re-feeling) ambayo ilianza mwaka 2013 na imekuwa ni kitambulishi cha ndege kumi za kawaida katika miaka kumi tu iliyopita, ikipunguza wastani wa umri wake wa ndege zake kutoka miaka 25 hadi miaka 10.

Bwana Kondic alisema: Kuwasili kwa ndege aina ya Air bus A330 mchana wa leo lilikuwa ni tukio la kihistoria kwa shirika la ndege la Serbia na ishara ya mafanikio katika siku za usoni.

“Ndege aina ya A330 ni ya kisasa na inatumia mafuta vizuri ambayo inafungua fursa nyingi za kukua kwa shirika la ndege na itaturuhusu kuzindua huduma za muda mrefu kwenda New York, inarahisisha safari kwa kiasi kikubwa huku ikiwezesha muunganiko kati ya Balkans na Marekani.

“Katika wiki zijazo ndege itakuwa tayari ikiwa na madaraja mawili ya Business na Economy ambayo zikiambatana na huduma zetu nzuri tunazotoa, itawapatia wageni wetu uzoefu wa safari usiolinganishwa kupitia Atlantic.”

Dondoo za huduma na bidhaa za ndege ya A330 inajumuisha mfumo wa burudani katika kila kiti inayokuwezesha kuchagua filamu, Muvi na burudani za Kiserbia na Kiingereza, viti vya kulala katika daraja la biashara na Menyu iliyoboreshwa, ikijumuisha huduma ya chakula pale unapohitaji kwa wageni wa daraja la Business.

Pic 3 Air Serbia A330.jpg

Kuhusu Shirika la Ndege la Serbia

Shirika la ndege la Serbia lilizinduliwa kama shirika la ndege la taifa la Jamuhuri ya Serbia Oktoba 2013. Kutoka katika kituo chake cha Belgrade, Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nikola Tesla, shirika la ndege la Serbia linafanya safari zake kwenda au ina mpango wa kuhudumia vituo 44 vya abiria na mizigo Ulaya, Mediterranean, Mashariki ya kati na Amerika ya kaskazini. Shirika vile vile linatoa safari ndefu na za kimataifa barani Asia, Australia, na Amerika kwa kupia washirika wake na washirika wake wa usawa, Shirika la ndege la Etihad ambalo linamiliki hisa asilimia 49. Shirika hili la ndege la Serbia kwa sasa linamiliki ndege kubwa moja, 14 nyembamba na ndege 6 za turboprob. Kwa maelezo zaidi tembeleawww.airserbia.com
 

Attachments

  • Pic 1 Air Serbia A330.jpg
    Pic 1 Air Serbia A330.jpg
    99 KB · Views: 24
Back
Top Bottom