Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi za vitu mbalimbali kwa watoto na wazee wanaolelewwa kwenye vituo saba vilivyopo mkoani Shinyanga ili nao washerehekee Sikukuu ya Eid el Fitr kwa furaha.
Zawadi hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Makao ya Watoto Yatima yaliyopo Bushushu na Makazi ya Wazee Wenye Mahitaji Maalumu Kolandoto yaliyopo Kata ya Kolandoto.
Akizungumza na TBC baada ya kukabidhi zawadi hizo RC Macha amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatambua, anathamini na kuheshimu uwepo wa jamii hiyo na kwamba anawapenda na kuwajali wakati wote.