Shinyanga: Hotuba ya Rais Magufuli uwanja wa Kambarage

NyaniMzee

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
396
727
Kwa apendaye kufuatilia yanayojiri Shinyanga fuatilieni hapa AzamTV



======

Rais Magufuli: Watu walikuwa wakiishi maisha ya ajabu ikiwemo hospitalini kulala watu kumi kitanda kimoja, nikaamua pesa ziende hospitalini.

Magufuli: Tunataka kusambaza umeme ili Tanzania ya viwanda iwezekane, viwanda vikiwa vingi vijana watapata ajira.

Tripple S alichukua kiwanda cha nyama muda mrefu na hakijaanza, siwezi kuwapa uda mwingine. Futeni huu mrani na mtafute muwekezaji mwingine, haiwezekani kumsubiri muwekezaji miaka 10. Kuna wakati tulitaka kukifuta, wakijitokeza wanasiasa wakamtetea weee, sasa niwaambie wanasiasa hakuna kumtetea tena, messege sent and delivered. Atakaewakwamisha yeyote ndani ya serkali mje mnione, ntamkwamua mimi mwenyewe.

Tumeibiwa mno, tumechezewa mno, sasa basi. Nimekaa serikalini miaka 20, nnayoyasema ninayajua.

Tanzania ni miongini mwa nchi tano Afrika zinazokuwa uchumi wake kwa haraka, wapinzani wetu hawataki kuyasema haya kwa sababu yanatupa sifa serikali.

Wanaosema hela zimeisha mifukoni, kwani zilikuwa zinagaiwa sokoni?. Ukiona hela zimeisha mfukoni ujue ulikuwa unakaa na hela ambazo sio zako.

Napenda kumshukuru sana Rais Kikwete kwa kuwavutia maji, siku za nyuma maji hayakuwepo, yameletwa mnasema bei ni kubwa. Nitachofanya hatukuleta maji ili yalete kero hata kama tunachangia kidogo, naomba mniachie hili, ntamtuma waziri wa maji aje afatilie bei ya maji. Kama bei ya hapa iko juu kuliko maeneo mengine, bei itashuka lakini kama bei ya hapa iko chini kuliko maeneo mengine basi itapanda.
======

Wameitwa mbunge wa Shinyanga na mhandisi wa maji mkoa wa Shinyanga kuja kuelezea kadhia ya bei ya maji kwenye mji wa Shinyanga. Mhandisi kasema bei ya maji mjini Shinyanga iko chini kuliko miji minane ikiwemo Dar es Salaam, Kahama na mengineyo.
 
Kwaya za makanisa ni mahsusi kwa ajili ya kumsifu Mungu. Je? Magufuli amegeuka kuwa Mungu mpaka afikie hatua ya kutungiwa nyimbo za sifa na kwaya ya kanisa?.
Kwani maana ya kwaya ni nini???
 
hv mfano hawa waliotoka kutumbuiza ss hv....wamefanya ivo kwa nia ya dhati kabisa ama kwa sbb kuna kuwa na chochote kidogo baada ya tumbuizo?
 
Back
Top Bottom