Shimbo afungua chuo kikuu cha JWTZ

Shimbo afungua chuo kikuu cha JWTZ

Status
Not open for further replies.

bibikuku

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2011
Posts
832
Reaction score
496
[TABLE="width: 99%, align: left"]
[TR]
[TD="class: kaziBody"]CHUO KIKUU JWTZ KUANZA MWAKANI

Habari Leo: 5 Agosti 2011

MNADHIMU Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo amesema Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa kinatarajiwa kuanza Julai mwaka 2012.

Shimbo alisema hayo jana Dar es Salaam mara baada ya kufungua semina ya wadau waliokutana kwa ajili ya mchakato wa maandalizi ya kuanza kwa chuo hicho.

Alisema, wadau hao walikutana ili kuandaa mitaala itakayotumika kutoa utaalamu kwa washiriki wa chuo hicho ambacho kitabobea katika kuweka mikakati ya ulinzi na usalama wa nchi.

“Wataalamu hao watachambua mitaala mbalimbali ikiwemo ile inayoshughulikia mambo ya ndani ya nchi na hata ya nje ili kuweza kupata ambayo ni stahiki kwa chuo hiki,” alisema Luteni Jenerali Shimbo.

Aliwataja wadau waliokutana kuwa ni pamoja na majenerali wa utumishi, majenerali waliostaafu na wahadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali.

Aidha Luteni Jenerali Shimbo alisema semina hiyo ni ya kwanza kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa chuo hicho ambacho wanatarajia kuwa chuo bora duniani cha ulinzi wa Taifa.

Alisema licha ya kwamba gharama ni kubwa kwa ajili ya uendeshaji wa chuo kama hicho lakini watajitahidi kuangalia masomo yanayofundishwa katika vyuo vikuu mbalimbali ili kuyaoanisha na vilevile kuangalia matukio ya kidunia.

Alisema wadau hao ndio watakaoangalia aina ya wanafunzi watakaoingia katika chuo hicho, ingawaje kinalenga kuchukua wanajeshi pamoja na raia lakini pia kitaangalia kama kuna uwezekano wa kuchukua wanafunzi wa nje ya nchi na nchi zipi zitakazopewa kipaumbele.

Kwa upande wake, Msimamizi wa chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makakala aliyetembelea vyuo mbalimbali duniani kwa ajili ya kupata uzoefu alisema, changamoto kubwa iliyopo ni jinsi ya kutafsiri matukio ya kidunia katika masuala ya kitaifa.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: Text"]My Take: KILA LA KHERI SHIMBO[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
  • Thanks
Reactions: oba
Napendekeza hicho Chuo kiwe pale Makao Makuu ya zamani ya JKT au Ngerengere huko Morogoro. Tulitakiwa kuwa na Chuo cha jeshi tangu zamani


hasa baada ya ile vita vya Kagera. :rapture:
 
Wiki nzima hii wanajitahidi kumweka public ili kupotezea dili wenye akili za panzi watasema si walisema kazimia mbona nimemuona kwenye TV.
 
naona media zishaanza coverage yake.. bongo ni zaidi ya uijuavyo.
 
Wiki nzima hii wanajitahidi kumweka public ili kupotezea dili wenye akili za panzi watasema si walisema kazimia mbona nimemuona kwenye TV.
<br />
<br />
mkuu Q ndo hvyo kwani akiwa mtu anataka kusafishwa si ndo huwa inakuwa hivyo.

Naona wiki hii ndo yake shimbo humu jf kam siku zilizopita kwa kaka EL..
 
<br />
<br />
mkuu Q ndo hvyo kwani akiwa mtu anataka kusafishwa si ndo huwa inakuwa hivyo.

Naona wiki hii ndo yake shimbo humu jf kam siku zilizopita kwa kaka EL..

Kumsafisha sawa wanaweza bali hicho kiharusi nacho kimetibiwa na media?
 
Napendekeza hicho Chuo kiwe pale Makao Makuu ya zamani ya JKT au Ngerengere huko Morogoro. Tulitakiwa kuwa na Chuo cha jeshi tangu zamani hasa baada ya ile vita vya Kagera. :rapture:

Chuo kilishajengwa tayari pale Kunduchi, kinachofanyika sasa hivi ni utayarishaj wa mitaala ya mafunzo. Vyuo vya jeshi vipo vingi, mojawapo ni "Tanzania Military Academy (TMA)", ila hiki ni tofauti kidogo na vilivyopo ndo maana kinaitwa "National Defence College". Wanaoenda kusoma pale sio askari tu bali hata viongozi wa kiraia. Ni kwa ajili ya masuala ua Strategic Defence and Security N.K.
 
Ccm na silikali yake watahubiri san juu ya weupe wa Shimbo lakini mbele za watz bado ni mweusi tu!!
 
Wakuu habari zilizopatikana ni kwamba Shimbo hakulazwa SA. Ila alipopata habari inasemekana ni kweli pressure ilimpanda, hakupelekwa SA wala Hospitali yao ile ya Lugalo, alipelekwa ile ya usalama wa taifa ili askari wasijue. Habari zaidi zinasema pesa alizokutwa nazo zinatokana na yafuatayo:
1. Serikali ya Comoro ilitoa euro milioni 180 kama shukrani kwa JWTZ yeye amekula zote bila huruma.
2. Serikali inampangia kila mwanajeshi hela ya chakula kwa mwaka. Askari wanasema wanapokwenda vitani nje ya nchi huwa hawalipwi hela hizi, zote anachukua huyu jamaa. Anafanyia nini, haijulikani.
3. Tenda zote jeshini ni za huyu jamaa, ukiacha matrekta inasemekana amewahi kupaka rangi majengo yapatayo manne huko morogoro ambayo yangegharimu hata mil 10, yeye alitumia mil 600. Mchezo huo inasemekana pia alifanya hivyo Arusha kwa mil 800.
4. Askari wanaokwenda vitani nje ya nchi kama wale Comoro, Darfur, Liberia na Lebanon inasemekana wanatakiwa kulipwa posho ya dola 1800, lakini badala yake wanalipwa dola 600 tu.
5. Askari wanaokwenda kufanya kazi ya uangalizi nje ya nchi wanatakiwa walipwe dola 10,000 lakini yeye shimbo anawakata mpaka dola 5000
6. Wanasiasa mafisadi inasemekana wanamtumia pia huyu jamaa kuhifadhi mihela yao kwa kuwa jeshi haliguswi.
6. Huyu jamaa inasemekana haguswi hata na mkuu wa majeshi jenerali Mwamunyange kwa sababu amewekwa na rais
7. Kiujumla askari inasemekana hawampendi hatta kidogo.
 
Mwache ale tu bill Shimbo, hili shamba la bibi bwana bt ipo siku tutaingia mtaani mpaka kieleweke na utachinjwa baharini tu
 
Ipo siku yaja watayasema yote hayo hadharani
Mbarak anajibu mashtaka akiwa kitandani bado hawa wanaoifilisi nch
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom