Shilam Disco Tech Dom au NK

babukijana

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2009
Posts
15,958
Reaction score
20,271
Wakulungwa mshafika humo hapo Dom enzi hizo,
Shilam Disco ilikuwa balaa la mjini.
Ilikua dakika mbili tu toka home kufika mle, tumecheza sana break dance mle ndani.
Na wale mabinti ukiwakuta mle, walikua wazuri,wazuri sana.
simu Hamna mnaandikiana barua kupitia SLP.
Unaandika leo unatuma mwenzio mpaka barua imfikie huko kijijini kaolewa mara 3 na watoto 10.
Sijui leo tuna wabunge km kina babutale,anakuja babalevo, mwanafa hawa nafkiri kipindi hicho walikua wananyonya.
Shilam mzee alifariki, Iringa Road tulikua majirani, pia Club mtaa mwingine tulikua hapo.
Nimekumbuka hayo maeneo enzi hizo hamna purukushani za kisiasa.
Una kumbuka nini toka "Dodoma" km alivyoimba Dr Remmy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…