kuna boxer mwenzio, ila yeye ni Mhaya. inaonyesha alipendwa na abiria wa kike, ikawa kama wapenzi, maana huyo dada alikuwa akimkumbatia na kujilaza mgongni kwa boxer (bodaboda wa boxer) kila mara wakiwa wote. watu around walijua ni mpenzi wake..
Mapenzi ama ukaribu wao ulidumu kwa kam siku tatu nne hivi, baadaye ikaanza tabia yule dada anafundishwa kuendesha pikipiki na boxer. Dereva yupo nyuma, dada yupo mbele lakn anashikiwa usukani na dereva, na kwa jinsi dada alikuwa smart alijifanya slow leaner. mara zote walikuwa wakifundishana kuendesha kwnye uwanja wa mpira wa mtaani.
Sasa sijui walikubalianaje, lakn kwa maelezo ya boxer ni kuwa, dada aliomba ajaribu kuendesha mwenyewe wakt jamaa yupo chini baada ya kuwa ame improve kuendesha. Kilicho fuatia ilionyesha dada alikuwa na skills kubwa ya kuendesha kuliko jamaa, maana alitia gia mfululizo na manjonjo kibao, akatembea.. pikipiki ilienda mazima.
huwa tukimwona, tunamtania hadi leo, kikweli alichanganyikiwa sana