Shika hapo hapo

Shika hapo hapo

MLALUKO JR

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2015
Posts
962
Reaction score
309
NYUKI UMENING'ATA

Ewe nyuki, ewe nyuki, ewe nyuki. Itika nakuita. Kwanini lakini ewe Nyuki?

Umenifanya niumie, niteseke, niweweseke. UNANIONEA.

Asali ninaonja, kidogo na si sana. NAFURAHIA. Ila kwanini unidunge?. Unidunge kwa sindano?. Sindano kali ya uchungu. UNANIONEA.

Kwa ufundi waitengeneza, kwa maringo waikoroja, kwa machejo waipakuwa. MMMH!HATARI

Imenifanya niwe mtumwa, mateka, zezeta, punguwani na nusu ya hayawani. UMENITEKA.

Si kwa amani si kwa furaha. SIKAI niikikosa asali. NIMEKAMATIKA. Muhanga nimejitoa, BETRI UMECHOMOA. Nimekuwa teja asali kuikosa. Inanipa AROSTO kuiokosa bora NIKUFE, NIZIKWE.

Kila nitembeapo pua zangu zinaitizama na kufurahia harufu yako na ya asali yako. NIPEWE NINI?

Usiitoe hadharani, ifiche abadani. INIFAE. Nijilambe vidole kwa Utamu nivikate. NIFURAHIE!

Usinipimie kibaba usikitumie. NIJICHOTEE. Nikitosheka nibeue nishushie na harwa na si tende. NIJIDAI.

*Mtunzi: Rajabu Mlaluko (MD)*
+255 753 93 86 28
 
mtunzi hapo amejiona Michael Jackson akati sisi mabaharia tunamuona hana tofauti na msaga sumu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom