''shetani kamshinda Mungu Tz"

LEO VII

Senior Member
Feb 7, 2013
118
33
''SHETANI KAMSHINDA MUNGU TZ?
Angalia. Mafisadi Hawakamatwi,
Wauza madawa ya kulevya wanatamalaki,
Majangili Yanaongoza wanachama,
Elimu Inadorora,
Mahakama zinahujumiwa,
Rushwa imetawala,
Ajira kwa vijana ni janga,
Udini uanakua kwa kasi,
Maliasili zinaporwa..(masikini twiga wetuu..)
Ugumu wa maisha unaongezeka kila kukicha...Duuu!!!
Eti jamani, MUNGU Ameruhusu haya au amekimbizwa na mkali Ibilisi bin Shwehetwaaannnn. teh teh tehee. Ok, Tuwe serious, mambo haya si bayana hapa tanzania? kama ndivyo je! si ya kishetani, kwa hiyo...Tunaongozwa na ama Shetani au wafuasi wake..naomba kurekebishwa...
 
Haya ni Majaribu tu.Yalikuwepo tangu Enzi za Nuhu. Shetani hajawahi na hataweza kumshinda Mungu asilani sio Tanzania tu bali Ulimwenguni pote.
 
Shetani wa Tanzania ni wananchi wenyewe. Tusimlaumu Mungu kwa maovu yanayofanyika! Hao wanasiasa matapeli mliwaweka madarakani kwa kura zenu wenyewe. Ni mungu gani aliyewashinikiza mpige kura kama vipofu? Uroho wa rushwa za kanga, chumvi na vikofia vya kijani ndio unaowatafuna!!
 
images
Bila kulitoa hili joka ccm 2015 hesabuni mmeumia tena
 
Inabidi ufute kauli yako,Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote hapa duniani,hata huyo shetani anayeutesa ulimwengu hivi sasa baada ya kumwasi Mungu.

Lakini pia lazima utambue kuwa kama Taifa kwa ujumla wetu,tungekuwa tunamuomba Mungu huku tukifuata yale aliyetuelekeza kuyafanya,ni lazima Mungu angeiingilia kati.

Lakini hebu imagine waTZ wengi wanamwomba Mungu,awaepushe na hali ngumu inayolikabili Taifa hivi sasa,lakini mtu huyo huyo,kila mara anaenda kwa Kalumanzira kupiga ramli!

Hebu imagine pia mtu anamwomba Mungu,aliponye Taifa hili na dhuluma tunazofanyiwa na watawala,lakini yeye mwenyewe kila siku yupo bar akipata kilaji,kitu ambacho kimeharamishwa na Mungu,au fikiria wale watu wengine wenye pepo wa ngono,ambao wengine wapo kwenye ndoa zao,lakini kila siku utawakuta kwenye nyumba za wageni,wakivunja ile amri ya 6 ya Mungu.

Kwa hiyo kama waTZ,tunataka Taifa letu liponywe kutoka kwenye haya mabalaa yanayolikumba Taifa letu,ni lazima turejee kwa Mungu wetu na tuyatende yale tu.tunayoelekezwa kuyatenda,kama yalivyoandikwa na vitabu vyetu vitakatifu vya dini.
 
Nakuunga mkono kuwa shetani katushinda sisi na kamwe hawezi kumshinda Mungu achilia kushindana nae. Mweka uzi anapaswa akafanye toba kwa kufuru aliyoiweka hapa. Hapo kwenye red bold, inasaidia kupunguza mawazo na kusahau matatizo kwa muda
 
Mwenyezi Mungu Alimuumba Mwanadamu, Akampa Intellect And Will ( Akili Na Utashi), Hivyo Mwanadamu Yupo Huru Kuchagua Baraka Au Laana. Kosa Au Makosa Tufanyayo Ni Udhaifu Wa Kutotumia Akili Na Utashi Vyema. Tunapenda Kupelekwa Kama Wanyama Waendao Kwa Instincts. Tuelewe Kuwa Kamwe Shetani Hawezi Kumshinda Mungu, Bali Mungu Haingilii Uhuru Aliotupatia. Ukiwa Atheist Waweza Sema Mungu Kashindwa Kama Alivyowahi Sema Nietsche!
 
''SHETANI KAMSHINDA MUNGU TZ?
Angalia. Mafisadi Hawakamatwi,
Wauza madawa ya kulevya wanatamalaki,
Majangili Yanaongoza wanachama,
Elimu Inadorora,
Mahakama zinahujumiwa,
Rushwa imetawala,
Ajira kwa vijana ni janga,
Udini uanakua kwa kasi,
Maliasili zinaporwa..(masikini twiga wetuu..)
Ugumu wa maisha unaongezeka kila kukicha...Duuu!!!
Eti jamani, MUNGU Ameruhusu haya au amekimbizwa na mkali Ibilisi bin Shwehetwaaannnn. teh teh tehee. Ok, Tuwe serious, mambo haya si bayana hapa tanzania? kama ndivyo je! si ya kishetani, kwa hiyo...Tunaongozwa na ama Shetani au wafuasi wake..naomba kurekebishwa...
Huyo mungu aliyeshindwa na Shetani ni mungu tumbo. Mungu wa kweli aliyeumba mbingu na nchi hawezi kushindwa na kiumbe wake, tena kiumbe aliyelaaniwa. Huku ni kumkosea Mungu adabu. Mungu ninayemwabudu herufi 'M' ni lazima iwe kwenye upper case. Lakini kwa miungu akiwemo Shetani ni small 'm'.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom